Changamoto za Ndoa: Kufungua Mlango Mpya au Kuendelea na Safari ya Majaribu?

ephen_

JF-Expert Member
Oct 28, 2022
3,627
14,788
Habari! Wakuu,

Ipo hivi, imetimia miaka 8 tangu ndugu yangu aolewe kama mnavyojua ndoa ni baraka lakini hii mmmh hapana...

Mwaka flani hio familia ilikuja nyumbani kuomba kijana wao amuoe ndugu yangu, hakuepo mama wala baba wa huyo kijana sababu wamefariki. Kipindi hicho ndugu yangu alikua amemaliza form 6 anasubiri kwenda chuo.

Akaambiwa kuhusu ndoa japokua hakuwahi kua na mahusiano na huyo kijana hapo kabla, ndo mara ya kwanza wanakuja nyumbani kuomba ndoa na yeye akakubali kuolewa.

Kijana alikua na miaka 36 ndugu yangu 19. Kwasababu ndugu yangu alikubali kuolewa kwa masharti ataendelea na chuo akiwa ndani ya ndoa.

Lakini kuna swali liliulizwa kwenda upande wa waoaji kwamba " mnataka vipi kumuoa ijapokua kijana wenu hana kazi, hana nyumba anaishi kwa kaka yake?"

Jibu walilotoa ni kwamba wameshajipanga kuhusu ajira na nyumba, baada ya kutoka honeymoon watafikia kwenye nyumba yao.

Upande wetu tuliridhika na ninahisi ndugu yangu alikubali kuolewa labda alikua anakimbia shida za kiuchumi kwetu, upande wa mwanaume wapo vizuri japo sio sana.

Ndoa ilipita vizuri lakini walivyotoka honeymoon walienda palepale kwa shemeji mtu ambaye ni kaka wa bwana harusi.

Tulioji hii imekaaje tukaambiwa wataenda kwao muda si mrefu, lakini ndugu zangu! sasa hivi imeshatimia miaka 8 ya ndoa bado wapo palepale, ndugu yangu hakupelekwa chuo.

Mbaya zaidi mume wake hataki kujiajiri kwa chochoteeee! Yeye anasema anatafuta kazi aajiriwe alisomea ualimu, kazi yenyewe hatafuti akiamka asubuhi ni kuoga ataanza kuzunguka facebook asubuhi mpaka muda wa kulala.

Ndugu zake wamejitahidi kumtafutia kazi lakini akienda kwenye interview anaharibu. Kuhusu chakula, mavazi mpaka nauli za hapa na pale kaka mtu ndo anawapa.

Ndugu yangu amechakaa sanaa wakati alikua pisi kalii mnoo. Mwanaume hataki kazi yoyote zaidi ya kwenye kiyoyozi anasema yeye ni msomi hawezi kufanya kazi ya uwakala wa fedha, kuna kipindi aliambiwa afunguliwe ofisi.

Ndugu yangu anapata manyanyaso kutoka kwa mke mwenzake (mke wa kaka wa bwanaharusi) ameshawachoka kabisa sababu hawachangii hata kitunguu.

Ndugu yangu alipewa mtaji na mama ake afungue restaurant ili apate hela ajikimu sababu gharama za kumrudisha chuo mke wa mtu mama huo uwezo hana lakini biashara ilifilisika mume wake anataka hela ya vocha kila siku. Miaka yote ya ndoa mke ajashika ujauzito.

Tulimpa ushauri arudi nyumbani asiendelee kubanana kwenye hiyo nyumba sababu hapo kwao wageni kila siku awakauki watu wanawashangaa, wanawadharau kukaa kwa watu lakini ndugu yangu alikataa kurudi akasema hawezi kumkimbia mume wake kwenye dhiki halafu akipata hela arudi tena.

Mna ushauri gani kwenye hili sekeseke?
 
Wanaoweza kutatua hilo tatizo ni wanafamilia upande wa mumewe maana wao ndio waliolitengeneza na wanalifuga!, Kuhusu ndugu yako mwacheni kwanza akili ikimkaa sawa ataamua yeye. Isijekuwa mnataka kuamua ugomvi wa pipa na mfuniko wake!.
 
Usikute huyo kaka mtu kamfanya ndondocha au ndo chuma ulete wake. Kibinadamu haiwezekani ukae na mdogo wako hana issue yoyote ile halafu muende mkamuozeshe mke kitu ambacho hakipo. Halafu mbaya zaidi miaka yote hiyo amekaaa tu kama boya.

Watu wengine huwa wanafungwa ufahamu wasijue wala wasiwe na maamuzi katika maisha yao.
 
Kuna siku ulinijibu kuwa...huwezi jibu swali la kitoto kana kwamba hujui kuwa siyo single mom wote hupenda kuwa na mtoto kabla ya ndoa...hudanganywa na wanaowaamini....mlidanganywa na mliye mwamini.....haya ni maisha bro...nikipigwa na hili utapigwa na lile
Mimi mwenyewe single mama😂 scenario ile na hii ni tofauti.
 
Usikute huyo kaka mtu kamfanya ndondocha au ndo chuma ulete wake. Kibinadamu haiwezekani ukae na mdogo wako hana issue yoyote ile halafu muende mkamuozeshe mke kitu ambacho hakipo. Halafu mbaya zaidi miaka yote hiyo amekaaa tu kama boya.

Watu wengine huwa wanafungwa ufahamu wasijue wala wasiwe na maamuzi katika maisha yao.
Exactly
 
Usikute huyo kaka mtu kamfanya ndondocha au ndo chuma ulete wake. Kibinadamu haiwezekani ukae na mdogo wako hana issue yoyote ile halafu muende mkamuozeshe mke kitu ambacho hakipo. Halafu mbaya zaidi miaka yote hiyo amekaaa tu kama boya.

Watu wengine huwa wanafungwa ufahamu wasijue wala wasiwe na maamuzi katika maisha yao.
Mbona kafunguliwa biashara hataki.
Ila la kukaa kwa ndugu na mke miaka ndo Nashangaa Leo.
Ukioa means umeweza kujibeba
 
Muache ndugu yako aishi anavyotaka MAISHA ni zaidi ya Kazi kula na kulala Maisha ni peace of mind Kama huyo dada yako anapata Amani ya moyo na Akili hizo chuki za hazina maana tena katika hii Dunia .


Hoja za mme wa dada yako zinamashiko Sana kiukweli.


Nyie ndugu mnapenda kuharibu ndoa za watu hasa sisi tunoishi na Kaka zetu wanatupenda Sana so waache watu waishi wanavyotaka
 
Back
Top Bottom