Historia batili: Riwaya mpya na JK episode 02

Historia batili: Riwaya mpya na JK episode 02

STORY: FAKE HISTORY (Historia Batili)
WRITER: Jumaa Khatib Mdharuba (Jk)
+255 718 274 130
+255 756 274 130

EPISODE 10
★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Sijui ni nini kimempata huyu baba Abdul jamanii..mmmh..” Aliwaza Hamida baada ya kukata ile simu ambayo ilikua inaonekana haina majibu. Kisha akamgeukia mwanae ambaye alikua na hamu kubwa ya kufahamiana na baba yake na kumwambia..“Babaako ni mtu wa mambo mengi sana, akiwa free atanitafuta na utaongea nae usijali mwanangu”. Akaweka nukta kubwa huku akiweka sawa ukosi wa shati la rangi mbili- nyeupe na nyekundu alilokuwa amevaa Abdul.
Abdul'rahiim, kama lilivyosomeka jina lake kamili, alionekana kuridhika na maelezo haya ya mama yake akaitia ‘sawa’ kisha akauliza swali ambalo lilimfanya mama yake ahamaki na kumfanya amuangalie mtoto yule mara mbili mbili..
Licha ya kuwa na umri wake mdogo wa miaka tisa lakini alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kufikiri na akili..Hakuwa akikurupuka katika kuongea mambo, na vitu vingi aliongea kwa kufikiri akiishirikisha akili yake katika kila analotaka kulitamka. Kwa sababu hii, si wanafunzi wenzake tu, bali hata walimu wote shuleni walimpenda sana na kuwa nae kwa karibu mno, wakifuatilia maendeleo yake kwa ukaribu mno huku wakihakikisha kuwa anapata haswa kile kilichompeleka shuleni.
Ni mwaka wa tatu mfululizo Abdul akiwa anazawadia tuzo ya mwanafunzi mwenye nidhamu zaidi shuleni. Awapo shuleni, Abdul alikuwa kipenzi cha wote.
Mama yake alikuwa akimueka katika mazingira ya usafi na kumfanya muda wote aonekane mtanashati, kila anayemtazama alikua na hamu ya kumuangalia tena.
“Mama, hivi kwanini wewe na baba hamuishi pamoja? Nini kiliwafanya mkatengana?” Hili ndilo swali gumu ambalo Hamida alikuwa hapendi aje aulizwe na mwanae..Si tu kwa sababu hakupenda mwanae afahamu undani wa baba yake ni nani, bali pia hakutaka mwanae ajue kuwa yeye alikuwa mtoto wa nje ya ndoa licha ya kuwa amelelewa katika mazingira ya kinidhamu sana na msimamo mzuri wa kidini. Jambo la yeye kuwa mtoto wa nje ya ndoa asingelikubali kirahisi, na huenda angeathirika haswa kisaikolojia-jambo ambalo Hamida hakutaka litokee kwa kipindi hiki.
Mama yake Hamida, bi Nana Amiry ambaye ndio bibi yake Abdul kwa upande huu wa mama yake alikua akisikia mazungumzo haya yanayoendelea kati ya Mwanae na mjukuu wake machachari Abdul.
Hamida alikua ndiye mtoto pekee wa bi Nana, na tangu kufariki kwa mumewe, Nana amekua akifarijiwa na hawa watu wawili tu, mwanae Hamida na mjukuu wake Abdul. Walikuwa wakiishi maisha ya kawaida sana, Hamida akifanya biashara za kukopesha nguo ambazo alikuwa akizifuata Kariakooo jijini Dar Es Salaam na kuja nazo mkoani Tanga walikokuwa wakiishi na mama yake. Na nje ya nyumba yao palikuwa na duka dogo la vyakula ambalo mara nyingi bi Nana ndiye alikua muuzaji wa duka lile, likiwaingizia pesa kidogo ambayo iliwawezesha kuwasukuma kimaisha kwa kadri riziki inavyopatikana.
Khatib, alikuwa akisaidia sana kwa nafasi yake kipindi cha nyuma kabla hajahamia Morogoro na pia hajawa mtu maarufu kama alivyo sasa..
Hamida alikuwa akimpenda saana Khatib, na hata kufikia kuzaa nae mtoto, japo bi Nana hakuridhika na jambo hilo kwa wakati huo.
Baada ya maisha ya Khatib kubadilika na kuhamia Morogoro, Khatib alianza kuwa 'busy' kidogo na mawasiliano aliyokuwa nayo kwa Mama hyu wa mtoto wake yalipungua kiasi kikubwa..Saa zingine Hamida alikuwa akipiga simu inaita na hapokei, saa zingine sms zake hazijibiwi..ilimradi palikuwa na mabadiliko.
“Sikiliza mwanangu nikwambie, hiyo ndo kawaida ya PESA, pesa inambadilisha sana mtu, sasa hapo huyo yeye anaona kama wewe unataka umuombe hela au umlilie shida zako wakati mwanzo mlikuwa mnawasiliana vizuri tu..” aliongea bi Nana kumwambia mwanae Hamida na kuongeza..“Sasa mwanangu, sisi rizki yetu inatoka kwa Mungu, na si kwake yeye huyo baba Abdul, wewe cha kufanya kwa sasa usimtafute mpaka akutafute wewe, na nisije nikasikia unamwomba pesa, mtoto huyu tutamlea tu na atakua kwa kudra za Mwenyezi Mungu” hapo ndipo alipokomea bi Nana na kumfanya Hamida kutafakari kwa kina kisha akachukua uamuzi wa kubadili namba yake ya simu ili hata hapo atakapotafutwa na Khatib awe hapatikani kabisaa..
Na hiki ndicho kilichotokea kwa miaka yote saba iliyopita, na kwakua Khatib alikua 'busy' sana na shughuli zake, mara chache alizobahatika kupiga simu na kukuta haipatikani zikazidi kumnyong'onyeza na kumfanya asipige simu tena..!!
“Bado hujakua mwanangu, upo muda ambao nitakueleza mimi na baba yako tulikutana wapi, tukaishi vipi, mpaka tukafikia hatua ya kukuzaaa wewe,..kwa sasa bado kidogo mwanangu..umenielewa?” Ndo maelezo aliyotoa Hamida kwa mwanae baada ya lile swali. Abdul alikuwa mdadisi, lakini hakuwa na pupa, na alikuwa akimsikiliza sana mama yake kwa kila analomwambia, kwahiyo aliridhika na maelezo haya na akaitikia kwa kichwa akimaanisha sawa..
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Habari za kuharisha mfululizo kwa Kulwa Yassini zilipenya taratiiib katika vikundi vya watu waliokuwa wamekusanyika katika maeneo ya karibu na nyumba ya msiba.. Kila mtu alianza kuhoji ni nini hasa kimetokea, wengine wakaanza kukata tamaa na azma ya Kulwa ya kuupeleka mwili wa marehemu Sauda hospitali kufanyiwa uchunguzi. Hii ni kutokana na muda kuwa umeenda sana na ni yeye Kulwa pekee ndiye aliyekuwa analiratibu jambo hili. Muda wa zaidi ya dakika 17 sasa Kulwa alikua hachezi mbali na mlango ule ambao ulikuwa hata hausindikwi kwa wakati huu kwa ajili yake tu..apate urahisi wa kuingia na kuachia vitu bila wasiwasi😃.
Mwili wake ulishaanza kukosa nguvu, maana aliharisha mfululizo sana, hivyo alipoteza maji mengi kwa muda mfupi..
“Kwahiyo Ma Mkubwa vipi, turuhusu mwili uende msikitini au tumsubiri huyu bwana mkubwa?” Aliuliza bwana mmoja mwenye umri wa miaka ya kijana, aliyeonekana kujazia misuli yake barabara..
“Pelekeni mwili msikitini mkauswalie kisha mkazike, huyo mwacheni aendelee na kuharisha kwake, mtoto mdogo balaa tele, kutuona watu wote hapa wapuuzi maanake nini, Mungu si huyo keshamlani aharisha sasa..” Aliropoka maneno mazito Mama Sauda akionesha msimamo wake waziwazi kuwa hakubaliani na jambo la Kulwa kutaka kupeleka mwili wa Sauda kwa uchunguzi zaidi.
*******************************
“Nasikia Kulwa anaendesha sana, ni nini kimemkuta sijui..?” Alihoji mzee mmoja anayekadiriwa kufikia miaka hamsini, akiwa amekaa nje ya nyumba ya msiba kwenye jamvi liliokuwepo chini ya mti wa mjohoro..Alikuwa ameketi yeye na wazee wengine watatu kwenye jamvi lile.
Mzee mmoja alionekana kuguswa zaidi na habari ile, na kuuliza kwa shauku..
“Kulwa huyu mtoto wa mdogo wangu Muna ndo anayeharisha?” akimtaja mama wa marehemu Sauda kama Muna, jina lake la kwenye vitambulisho.
“Ndiye yeye huyo, ana zaidi ya dakika ishirini sasa, tangu atangaze kuupeleka mwili hosptal kwa uchunguzi zaidi na kuhara kukaanzia hapohapo😀” Alifunguka mzee yule kwa maelezo mazuri yaliyonyooka..
Baada ya maelezo haya mzee huyu muulizaji maswali ambaye ni kaka mkubwa wa Muna-mama wa marehem Sauda, au twaweza kumuita mjomba wa marehemu Sauda, Jina lake likiwa Jumanne Selemani, wengi wakimjua kama Mzee J4, alinyanyuka moja kwa moja mpaka uani mwa nyumba ile ya msiba, akamkuta Kulwa amejiinamia kwenye mnazi kitamli uliokuwa karibu na chooni huku ameshikilia tumbo lake, akionesha kuwa linamuuma kwani alikua analia kama mtoto mdogo.
Akamgusa begani na kumfanya astuke..
“Ndio mjomba” ndicho alichokisema Kulwa baada ya kugeuka na kumuona aliyemshika begani.
Mzee J4 alimuangalia sana Kulwa usoni, kisha akasikitika, halafu akapitisha mkono wake wa kulia katika uso wa Kulwa kisha akamwambia..
“Maiti imeshatoka, twende msikitini ukamswalie mdogo wako swala ya mwisho hii..hii vita ni nzito..HUIWEZI, wewe bado mchanga sana”
“Sasa Mjomba nitaendaje na hali hii naendesha kweli??” Alihoji bwana Kulwa ambaye hata sauti yake ilikua ya kichovu sana.
“Hapana, huharishi tena kwa sasa..”

★★★★★★★★★★★★★★★★★

Watch Out Episode 11

Follow IG: sir_mdharubajk

©2015
 
Mdharuba, nakupigia simu hupatikani. Kwenye namba ya tigo.
 
me siku ya msiba sikuwepo kumbe ndio ilivyokua lete mchapo ndugu dunia inamambo hii!dahh big up
 
STORY: FAKE HISTORY(Historia Batili)
WRITER: Jumaa Khatib Mdharuba(Jk)
+255 718 274 130
+255 756 274 130

EPISODE 11
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Ni siku tatu sasa tangu mwili wa Sauda upumzishwe kwa amani,Si Kulwa tu, bali hakuna hata mmoja kati ya ndugu zake pia aliyekuwa amehoji au kuulizia kuhusu kifo cha Sauda na utata ambao Kulwa alidai upo. Walishasahau.. Na ni katika siku hii hii ndio Kulwa alipigiwa simu kutoka kazini kwake na akatakiwa arudi Rwanda kwani yeye alikua mtu muhimu sana pale benki..Akiondoka kuna mambo mengi sana yanasimama yakimsubiri yeye..Na kwakuwa walishazika, akawa hana namna bali kuondoka tu. Alipanga aondoke kesho yake asubuhi sana..
“Mjomba nataka nkwambie kitu ambacho kitakusaidia maishani mwako..” Alianza kuongea Mzee J4 baada ya kumwita pembeni Kulwa, hii ni baada ya kuagwa safari na mjomba wake huyu..
“Kwenye haya maisha kuwa makini sana mjomba, usidhani kila kitu unachofikiri unaweza kufanya basi ukakurupuka kukifanya, UTAUMBUKA..” Alianza nasaha zake mzee J4 kwa kijana wake huyu ambaye alionesha waziwazi kuwa pesa ilimpa kiburi.
“Watu wenye uwezo wa kifedha(matajiri) wana mambo mengi sana nyuma yao ambayo sisi raia wengine hatuyajui..sasa unapotaka kushindana na mtu wa aina ile, wewe mwenyewe uwe umejipanga, na sio kujipanga kwa pesa, bali ujipange kwa mambo mengine..” Bado mzee j4 aliendelea kufunguka kwa mwanae huyu..
“Sasa kwa mfano kama sio mimi kukuokoa pale, wewe ulikua unaharisha mpaka kifo chako, unafikiri ingekuaje?” Alihoji Mzee J4 kumuuliza Kulwa ambaye kwa muda wote huo alikua anatafuta haswa Mzee J4 anataka kuongea kipi haswa, na sasa anaonekana kupata picha ya nini Mzee J4 anamaanisha..
“Kama mtu anaweza kumuua mkewe, atashindwa kukuua wewe?” Ndivyo alivyozidi kugongelea msumari wa moto Mzee J4 katika kichwa cha Kulwa.. Mzee J4 aliongea maneno haya mfululizi akiwa hataki kumpa nafasi Kulwa kuchangia.. Kisha akamalizia kwa kumwambia..“Jambo ambalo limeshatokea kama hivi, usipende sana kwenda kinyume na utaratibu uliozoeleka, hutaonekana SHUJAA bali KICHAA.. sasa kwa mfano ungegundua kuwa Sauda alipewa sumu akafa, na aliyemuua ni mumewe, wewe si ungetengeneza uhasama na Khatib? Na unahisi ungekua na mwisho mzuri? Hebu saa zingine weka mbali MATAMANIO ya nafsi yako, na uangalie UHALISIA ukoje, nakutakia safari njema” Alimalizia maneno hayo Mzee J4 akampa mkono Kulwa kisha yeye akawa ndiye wa kwnza kutangulia ndani..
Kulwa alibaki pale nje akitafakari kwa kina maneno aliyoambiwa na Mjomba wake, ambaye hakumpa hata nafasi ya kujieleza au kuuliza swali.
*******************************
“Hello My lovely Husband..
I miss you so much my..
I wish I could see you this weekend..
It has been a long time now..
I love you so much..bye”

Ilikua ni short and clear e-mail ambayo ilikua imetumwa kwenye e-mail address ya Mr Khatib 26th May, siku tano kabla ya Arobaini ya Sauda.. aliisoma barua pepe hii na kushika kichwa, kwani hiyo ilikua ni siku ya Jumatano, na email ilitamani ndani ya weekend waonane..Alijikuta katika wakati mgumu sana..Jumapili ilikua ndio siku ya 40 tangu Sauda kufariki, na maandalizi ya kumalizia huu msiba yalishafanyika yote na kila kitu kikiwa tayari, yeye kama Mume wa marehemu aligharamia kila kitu kinachohusu chakula kwa ajili ya siku hiyo. Alianza kujiuliza itakuaje endapo hatoonekana katika 40 ile..zaidi ya kuonekana msaliti na penginepo zile hisia za kuwa amemuua mkewe huenda zikaibuka upya. Na vipi kuhusu mtumaji wa ile email??!! Ambaye anaonyesha ni mkewe?..
“Hisham, mi naona uniwakilishe tu ifikapo Jumapili, kila kitu nimetoa, na kwa asilimia 85 za hiyo shughuli nzima ni pesa zinazotoka mfukoni mwangu, sasa kama bado wataendlea kunilaumu waache tu” Maneno yaliyotoka kinywani kwa Khatib akiongea na Hisham usiku wa Ijumaa kwani Khatib alipanga kuondoka Jumamosi asubuhi kuelekea nchini Canada kuonana na mama Camilla Hellen, Manager wa Camihel Bank of Commerce (CBC) iliyokuwepo Jijini Vancouver.
“Kusema ni kawaida ya waswahili, we nenda tu boss, mi niache nao tu hawa waswahili nitamalizana nao..” Maneno ya Hisham Omar Mikidad akimtoa wasiwasi Khatib ili afanye kama alivyotakiwa kufanya.
Kitu ambacho kilionekana hapa ni kuwa email ile haikuwa inaomba kukutana na Khatib, bali ilikua ni 'order' ya kuonana na Khatib. Kwani kama si hivyo Khatib asingekubali kuacha shughuli ya mkewe na kupanda ndege kuelekea Canada kipindi kile..lazma palikua pana zaidi ya ambavyo wtu wote wanawez kufikria.
“Sawa kaka, nashukuru sana, kila la kheri na tutaonana tena baada ya wiki mbili nadhani” ndivyo alivyoaga Khatib kwa Hisham..
Ila kabla hawajaachana, Khatib alionekana kukumbuka kitu, Hisham ambaye wakati huu alishafungua mlango wa gari yake tayari kwa kuondoka, alimuona Khatib akimnyemelea kama anayetaka kumwambia kitu..
“Vipi boss, kuna kitu umesahau??”
“Yeah Hisham, unajua ni wewe pekee ndiye unayejua siri zangu nyingi, nakuamini kama ndugu yangu, maana kwa sasa sisi tumekua si marafiki tu, au watu tunaoshirikiana kwenye biashara, bali tumekuwa ndugu kabisa.. ” Khatib kwanza alianza kueleza ukaribu wao kati yake yeye na Hisham ili kumueka tayari aweze kupokea atakaloelezwa.
“Mimi naamini hakuna siku wewe Hisham utakuja kunisaliti, na ndio maana nakutumia wewe zaidi katika mambo yangu mengi kuliko Haroun..na hata malipo yako ni makubwa zaid kuliko ya Haroun..” Khatib aliendelea kuiweka sawa akili ya Hisham kabla hajaongea kile alilolikusudia haswa..
“Can't you see? Wewe ni Manager wa Pub na unakula pesa nyingi zaid kuliko Manager wa Hotel kubwa kiasi kile..!?? Hii inadhihirisha imani yangu kwako..nakukubali sana bro”
“Boss,mi nashkuru sana kwa kunikubali, wewe ndiye rafiki pekee uliyefanya Hisham akawa mtu aliye hivi sasa..sipati picha kama si wewe mi ningekua na maisha gani sasa..hawa jamaa wajinga si wangeendelea kunifanya 'punda' mpaka leo,? Nawaingizia wao pesa nyingi mimi nakula hela ya mbuzi, kila siku nikiwa na hamu ya kurudi tena kuwakusanyia wao mzigo..Jambo baya zaidi nilikua nawaza siku hiyo vitakaponipasukia tumboni..sijui ingekuaje?.. Kaka, mi nakushukuru sana, kukusaliti wewe ni sawa na kuisaliti nafsi yangu mwenyewe..SIWEZI KUFANYA HIVYO” Hisham aliongea maneno haya kwa hisia, akimueleza Khatib umuhimu wake kwake..
“Hebu nambie boss, ni kitu gani hicho haswa unataka kunieleza boss wangu, mi ndo mtu wako pekee wa kunieleza kuhusu habari zako nyeti..”
“Kuna siri moja nzito sana nataka kukueleza kaka, maana mi nasafiri na sijui huko ninakoenda patakuaje..na huku nyuma naacha mambo mengi sana ambayo yananihitajia..majukumu yamekua mengi, mambo mengine ambayo yalikua siri yangu tu, sina budi kukupunguzia, ili kwa kipindi kama hiki ambacho sipo basi unaweza ukasimamia na ukasaidia pale panapohitajia msaada..” Alianza kufunguka Mr Khatib, kisha akaendelea..
“Mtu ukiwa maarufu na tajiri, unakua na siri nyingi sana ambazo usingependa watu wazifahamu, ni kwa sababu ya kulinda ile REAL IDENTITY yako..kwa sababu mimi binafsi naishi kwa FAKE HISTORY hapa duniani..na kama itatokea jamii ikajua historia yangu halisi, basi nitakua katika wakati mgumu sana..”
“Naelewa boss, nami naahidi kuwa pamoja na wewe mpaka kufa” Hisham alikuwa akipenda sana jinsi Khatib anavyomuheshimu na kumchukulia kama ndugu yake, hakuwa na malipo kwa Khatib zaid ya kufanya vile anavyovihitaji tu..
“Hivi mbali na umbea umbea ambao alikua analeta, unafikiri sababu nyingine ya mimi kumuua Sauda inaweza kuwa ni nini?” Khatib aliamua kuanza kile anachotaka kumwambia Hisham kwa swali lile..
Hisham akainamisha kichwa chini akitafakari nini kinaweza kuwa sababu ya kifo cha Sauda zaidi ya ile ambayo anaifahamu yeye, kuwa Sauda alihoji uhalisia wake. Alitafakari kwa muda kidogo kisha akanyanyua kichwa na kumwangalia Khatib kisha akasema “Hapana, sifahamu boss..”
Khatib akamuangalia Hisham usoni ambaye alionekana kuwa na shauku ya kujua ni nini haswa undani wa kifo cha Sauda..
“Sasa nisikilize kwa makini sana, ila kabla sijaanza kukueleza, hebu save hii namba katika simu yako..” Aliongea Khatib akimkabidhi simu yake Hisham ambayo alikua ameandika namba za simu ambazo Hisham alitakiwa kusave..
“Ok, boss..niandike Jina gani?”
“Kwani namba yangu ya simu umesave kwa jina gani?”
“Nimeandika Boss”
“Basi hiyo andika Khatib”
★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Unakosaje Episode 12??
Unajua ni siri gani nzito ipo hapo?..

Follow IG: Sir_mdharubajk

Maoni: +255718274130
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom