Historia batili: Riwaya mpya na JK episode 02

Historia batili: Riwaya mpya na JK episode 02

STORY: Historia Batili-Fake History.
MTUNZI:Jumaa Khatib Mdharuba
+255 718 274 130

SEASON 01-EPISODE O4
★★★★★★★★★★★★★★
Alice, dada anayekuwa reception katika zamu ya mchana hapa Euler Hotel alikua akijiuliza maswali mengi sana juu ya huyu bwana Khatib ambaye alionekana wazi kutoeleweka..Alipendelea kuja hapa na mkewe Sauda mara kwa mara na kulala naye mpaka wakawa wamemzoea, lakini baada ya Alice kupafahamu nyumbani kwa Khatib ndo akaanza kupata mashaka nae..Nyumba ilikua kubwa ya kifahari ambayo ilikua na kila kitu au zaidi ya vile alivyokua anapata pale Euler Hotel..Sasa kwanini aache kulala nyumbani kwake na aje alipie laki 1.5 kwa Executive room per day na alikua anakaa zaidi ya wiki moja pale hotelini sometymz..
Kingine kilichompa mawazo zaidi ni kwanini Haroun ambaye ndiye Manager wa hii hoteli alikua akimuheshimu sana Khatib, na mara zote alipokuja alikua na kawaida ya kumkaribisha ofisini kwake na walikua wakiongea kwa zaidi ya dakika 30!!
Maswali haya ya Alice hakuna aliyeweza kuyajibu zaidi ya kujaribu kupotezea tu..ila leo alishtuka zaidi kwa maana hakumuona Khatib siku nyingi pale hotelini halafu pia amekuja peke yake wakati si kawaida yake. Kama hiyo haitoshi, moja kwa moja ameenda ofisini kwa Manager pale ghorofa ya tano.. Akaamua kumshirikisha Florah, ambaye walikua wote reception zamu ya mchana..!!
"Huyu Khatib ww unamuelewa Florah?"
"Kivipi Alice wee..mbona utakua mmbea mtoto wa kike wee..mi namuona kawaida tu"
"Ana dili gani na boss, mbona wanajifungia kila siku pale ofisi ya juu halafu hatujui wanaongea nini?" Alice alionekana ni mfuatiliaji mzuri sana kwa mujibu wa maelezo haya..
"Babu wee..wote hao wana mapesa yao..usishindane nao, itakua wana dili zao.." Florah alijibu kimkato tu wala hakuwa na mda wa kufatilia kwa undani juu ya kile alichoelezwa na Alice..Ila moyoni kwa Alice bado alitamani kufahamu uhusiano uliopo kati ya Haroun na Khatib..
Akaamua amsubiri Mr.Khatib akitoka ajaribu kumdodosa huenda akapata mwanga juu ya ayawazayo.
Na baada ya dakika 27 Khatib alipita reception akielekea nje alikopark gari yake..
"Samahani boss" Ilikua ni sauti ya Alice akimuelekea Khatib akionekana kutaka kumuuliza kitu..
"Yes Alice Nemhina Tupa, una tatizo?" Aliitika Mr.Khatib na kumfanya Alice ashtuke kidogo, Ni kwel anajua kuwa Khatib anamfahamu, lakin sio hadi jina la babaake na la ukoo..akabaki mdomo wazi hajui huyu mtu kajuaje jina lake kamili wakati hapa kazini yeye alijulikana kwa jina moja tu la Alice.
"Sijakuona siku nyingi boss ulikua waapi? Afu naona wife nae hujaja nae leo..nashangaa umeongea tu na boss Haroun afu unatoka, vipi kwema?" Aliuliza maswali haya Alice ambayo cdhani hata kama angejibiwa angepata faida gani..
Khatib alisimama kidogo akamwangalia sana Alice kisha akamjibu kifupi "Ntarudi baadae" akaingiza mkono mfukoni na kumkabidhi Alice sh elf 80, "Naomba tukutane Mambo pub leo saa 3 usiku" Ndio maneno yaliyofuatia baada ya kukabidhiwa pesa ile kisha akatoa business card na kumkabidhi.
Alice Kabla hajajibu chochote Khatib alishavuta hatua hadi katika mlango wa gari lake na kuzama ndani akawasha gari na kuondoka kwa kasi sana.
★★★★★★★★★★★★★★ "MORO 9pm URGENT" Ndivyo ilivyosomeka sms aliyoipata Noor A Mdharuba soon baada ya Khatib kutoka pale hotelini. Ilijieleza vizuri kuwa alitakiwa awepo Moro kabla ya saa 3 usiku na ilikua ni muhimu sana. Noor alishaelewa..na hakuchukua muda sana akawa yuko barabarani akitokea Dar kwenda Moro..
Alifika Morogoro majira ya saa 1 usiku na moja kwa moja akafikia Euler Hotel akapata chakula cha jioni kisha akazama chumbani kujipumzisha.
Khatib alikuwa nyumbani kwake muda huu akijaribu kumpa maelekezo Noor juu ya nini cha kufanya kwa kutumia sms..
"0714261861; Alice; P-Wp;Mb;21😀c" Hiyo ndiyo ilikua msg yenye maelekezo yote juu ya kipi Noor alitakiwa kufanya hapa Moro, hakukuwa na haja ya kuonana na Khatib sababu kila kitu kilijieleza katika msg ile.
0714261861 ilikua ni namba ya simu ya mkononi ya Hisham Omar Mikidadi Manager wa Mambo pub ambayo ilikua ikimilikiwa na Mr.Khatib na siri hii alikua akiijua Hisham peke yake, Hisham pia alifaham uhusiano uliopo kati ya Noor na Khatib ingawa hawakuwahi kuonana ana kwa ana hata siku moja, ilikua ni lazima Hisham atambue uwepo wa Noor Mambo pub jioni ya leo.
Alice ndo mtu ambaye alitakiwa kudeal nae.
P-Wp: Ni maelekezo kuwa picha ya Alice ataituma kupitia whatsap.
Mb: Ni initial waliotumia kuashiria Mambo Pub ambayo ndio sehemu aliyoambiwa Alice akutane na Khatib.
21: Inaashiria tatu usiku kuwa ndo muda wa promise.
Dc; Ni maelekezo kuwa Noor alitakiwa afanye nae mahojiano ya kina sana..
★★★★★★★★★★★★★★
"Vipi kazi yako mke wangu? Umeianza vizuri?" Alihoji Mr.Khatib wakati huu wakiwa kitandani na mkewe Sauda.
"Yeah, nashukuru..ila umenisuprise sana, daah siamini yani"
"Kawaida tu, mpango huo nlikua nao tangu siku nyingi ila nilikua navuta subra kwnza.."
"Ok, sawa.. thanks kwa kutambua umuhimu wangu, mi nilikua nachukia sana kukaa nyumbani muda wote, atleast now ntakua na amani kidogo"
"Ok sawa, nakupenda saana.."
"Huna lolote, ungenipenda sana ungeniwekea ratiba??" Sauda alianza utani wa kweli na kumfanya Khatib awe mpole..
Maneno haya yaliashiria leo huduma ilitakiwa hapa ndani ingawa haikuwa ratiba yake. Lakin kwa jambo alilokusudia kulifanya usiku ule, ilibidi abadili msimamo wake..
"Ucjal, usiku wa leo lazima uukumbuke"
Na baada ya ahadi hii ndipo Khatib alipoanzisha purukushani za hapa na pale katika kuhakikisha panakua na dibaji ya maana kabla ya kuanza chapter ya kwnza na kuendlea.
Ni siku ambayo bwana huyu alitoa vitu adimu sana kwa bi mdogo yule na kumfanya kupayuka mijineno mengi isiyo na maana. Usiku ukaisha vizuri kabisa wote wakiwa hoi lakini kwa furaha.
"Ikiwa hivi kila siku hata ukiondoka mwezi usipoaga mi sina neno, ila ww hunipi huduma kama hizi kwa ukamilifu halafu waondoka, mi napata wivu najua unaenda kuwapa wengine huko"
Maneno yaliyomtoka bi Sauda asubuhi baada ya kumuamsha mumewe ili akaoge.
Mr.Khatib alimwangalia kisha akatabasamu bila kuongea neno lolote.
★★★★★★★★★★★★★★
"Haya nambie boss, ni kazi gani maalum iliyokuleta hapa leo, maana najua wewe Khatib anakutumia kwa kazi maalum tu." Hisham aliongea baada ya kufahamiana na Noor kwa sura sasa, wakiwa katika meza fulani iliyozungukwa na viti vitatu ndani ya Mambo pub, ilikua ni majira ya saa 2:19 usiku.
"Kuna bint anaitwa Alice nimekuja kufanya mahojiano nae maalum".
"Vipi ameleta kujifanya kujua?" Alihoji Hisham akiwa na hamu ya kujua nini kinaendelea hapa.
"Yaah alijaribu kumuuliza boss nahis kuhusu vtu flan vilivyoashiria kumfuatilia, maana amenambia nifanye nae deep conversation."
"Okay, kama ameanza kuleta kidomodomo poteza tu" Alisema Hisham ambaye alionekana kuwa hakua hata na chembe ya huruma.
"Ntaangalia mahojiano yetu yatakavyokua maana sometymz lisilo budi hutendwa" Aliongea kwa busara kidogo Mr.Khatib.
"Wewe unaremba sana, watu hawa ni hatari sana zaidi ya Ebola, wanatakiwa kufa mapema kabla ya kuambukiza wengine.." Bado aliendelea kusisitiza Hisham Omari Mikidadi, safari hii akigonga meza na ngumi na kunyanyuka kuelekea ofisini kwake ndani ya pub ile.
★★★★★★★★★★★★★★
Don't Miss Episode O5
 
Una kipaji ambacho ukikiendeleza hautakuwa na haja ya kuajiriwa!! You will be our Hadley Chase!! Kaza buti, hadithi zako ni tamu na kuongeza suspense uzilete hivyo hivyo vipande vipande!!
 
Kama hujaelewa kausha,alafu unaqoutije hadith nzima kuandika maneno kama haya?[/ usiwe na ulewa hasi, nimeuliza ili kutaka kujua Ana maana gani . Mbona yeye kajibu kistaribu tu , wew ndo unaona umekereke sanaaa!!!
 
Una kipaji ambacho ukikiendeleza hautakuwa na haja ya kuajiriwa!! You will be our Hadley Chase!! Kaza buti, hadithi zako ni tamu na kuongeza suspense uzilete hivyo hivyo vipande vipande!!

Jiandae kusoma kitabu soon ..
 
STORY: Historia Batili-Fake History.
MTUNZI:Jumaa Khatib Mdharuba
+255 718 274 130

SEASON 01-EPISODE O4
★★★★★★★★★★★★★★
Alice, dada anayekuwa reception katika zamu ya mchana hapa Euler Hotel alikua akijiuliza maswali mengi sana juu ya huyu bwana Khatib ambaye alionekana wazi kutoeleweka..Alipendelea kuja hapa na mkewe Sauda mara kwa mara na kulala naye mpaka wakawa wamemzoea, lakini baada ya Alice kupafahamu nyumbani kwa Khatib ndo akaanza kupata mashaka nae..Nyumba ilikua kubwa ya kifahari ambayo ilikua na kila kitu au zaidi ya vile alivyokua anapata pale Euler Hotel..Sasa kwanini aache kulala nyumbani kwake na aje alipie laki 1.5 kwa Executive room per day na alikua anakaa zaidi ya wiki moja pale hotelini sometymz..
Kingine kilichompa mawazo zaidi ni kwanini Haroun ambaye ndiye Manager wa hii hoteli alikua akimuheshimu sana Khatib, na mara zote alipokuja alikua na kawaida ya kumkaribisha ofisini kwake na walikua wakiongea kwa zaidi ya dakika 30!!
Maswali haya ya Alice hakuna aliyeweza kuyajibu zaidi ya kujaribu kupotezea tu..ila leo alishtuka zaidi kwa maana hakumuona Khatib siku nyingi pale hotelini halafu pia amekuja peke yake wakati si kawaida yake. Kama hiyo haitoshi, moja kwa moja ameenda ofisini kwa Manager pale ghorofa ya tano.. Akaamua kumshirikisha Florah, ambaye walikua wote reception zamu ya mchana!!
"Huyu Khatib ww unamuelewa Florah?"
"Kivipi Alice wee..mbona utakua mmbea mtoto wa kike wee..mi namuona kawaida tu"
"Ana dili gani na boss, mbona wanajifungia kila siku pale ofisi ya juu halafu hatujui wanaongea nini?" Alice alionekana ni mfuatiliaji mzuri sana kwa mujibu wa maelezo haya..
"Babu wee..wote hao wana mapesa yao..usishindane nao, itakua wana dili zao.." Florah alijibu kimkato tu wala hakuwa na mda wa kufatilia kwa undani juu ya kile alichoelezwa na Alice..Ila moyoni kwa Alice bado alitamani kufahamu uhusiano uliopo kati ya Haroun na Khatib..
Akaamua amsubiri Mr.Khatib akitoka ajaribu kumdodosa huenda akapata mwanga juu ya ayawazayo.
Na baada ya dakika 27 Khatib alipita reception akielekea nje alikopark gari yake..
"Samahani boss" Ilikua ni sauti ya Alice akimuelekea Khatib akionekana kutaka kumuuliza kitu..
"Yes Alice Nemhina Tupa, una tatizo?" Aliitika Mr.Khatib na kumfanya Alice- ashtuke kidogo, Ni kwel anajua kuwa Khatib anamfahamu, lakin sio hadi jina la babaake na la ukoo..akabaki mdomo wazi hajui huyu mtu kajuaje jina lake kamili wakati hapa kazini yeye alijulikana kwa jina moja tu la Alice.
"Sijakuona siku nyingi boss ulikua waapi? Afu naona wife nae hujaja nae leo..nashangaa umeongea tu na boss Haroun afu unatoka, vipi kwema?" Aliuliza maswali haya Alice ambayo cdhani hata kama angejibiwa angepata faida gani..
Khatib alisimama kidogo akamwangalia sana Alice kisha akamjibu kifupi "Ntarudi baadae" akaingiza mkono mfukoni na kumkabidhi Alice sh elf 80, "Naomba tukutane Mambo pub leo saa 3 usiku" Ndio maneno yaliyofuatia baada ya kukabidhiwa pesa ile kisha akatoa business card na kumkabidhi.
Alice Kabla hajajibu chochote Khatib alishavuta hatua hadi katika mlango wa gari lake na kuzama ndani akawasha gari na kuondoka kwa kasi sana.★★★★★★★★★★★★★★
"MORO 9pm URGENT" Ndivyo ilivyosomeka sms aliyoipata Noor A Mdharuba soon baada ya Khatib kutoka pale hotelini. Ilijieleza vizuri kuwa alitakiwa awepo Moro kabla ya saa 3 usiku na ilikua ni muhimu sana. Noor alishaelewa..na hakuchukua muda sana akawa yuko barabarani akitokea Dar kwenda Moro..
Alifika Morogoro majira ya saa 1 usiku na moja kwa moja akafikia Euler Hotel akapata chakula cha jioni kisha akazama chumbani kujipumzisha.
Khatib alikuwa nyumbani kwake muda huu akijaribu kumpa maelekezo Noor juu ya nini cha kufanya kwa kutumia sms..
"0714261861; Alice; P-Wp;Mb;21😀c" Hiyo ndiyo ilikua msg yenye maelekezo yote juu ya kipi Noor alitakiwa kufanya hapa Moro, hakukuwa na haja ya kuonana na Khatib sababu kila kitu kilijieleza katika msg ile.
0714261861 ilikua ni namba ya simu ya mkononi ya Hisham Omar Mikidadi Manager wa Mambo pub ambayo ilikua ikimilikiwa na Mr.Khatib na siri hii alikua akiijua Hisham peke yake, Hisham pia alifaham uhusiano uliopo kati ya Noor na Khatib ingawa hawakuwahi kuonana ana kwa ana hata siku moja, ilikua ni lazima Hisham atambue uwepo wa Noor Mambo pub jioni ya leo.
Alice ndo mtu ambaye alitakiwa kudeal nae.
P-Wp: Ni maelekezo kuwa picha ya Alice ataituma kupitia whatsap.
Mb: Ni initial waliotumia kuashiria Mambo Pub ambayo ndio sehemu aliyoambiwa Alice akutane na Khatib.
21: Inaashiria tatu usiku kuwa ndo muda wa promise.
Dc; Ni maelekezo kuwa Noor alitakiwa afanye nae mahojiano ya kina sana..★★★★★★★★★★★★★
"Vipi kazi yako mke wangu? Umeianza vizuri?" Alihoji Mr.Khatib wakati huu wakiwa kitandani na mkewe Sauda.
"Yeah, nashukuru..ila umenisuprise sana, daah siamini yani"
"Kawaida tu, mpango huo nlikua nao tangu siku nyingi ila nilikua navuta subra kwnza.
"Ok, sawa.. thanks kwa kutambua umuhimu wangu, mi nilikua nachukia sana kukaa nyumbani muda wote, atleast now ntakua na amani kidogo"
"Ok sawa, nakupenda saana.."
"Huna lolote, ungenipenda sana ungeniwekea ratiba??" Sauda alianza utani wa kweli na kumfanya Khatib awe mpole..
Maneno haya yaliashiria leo huduma ilitakiwa hapa ndani ingawa haikuwa ratiba yake. Lakin kwa jambo alilokusudia kulifanya usiku ule, ilibidi abadili msimamo wake..
"Ucjal, usiku wa leo lazima uukumbuke"
Na baada ya ahadi hii ndipo Khatib alipoanzisha purukushani za hapa na pale katika kuhakikisha panakua na dibaji ya maana kabla ya kuanza chapter ya kwnza na kuendlea.
Ni siku ambayo bwana huyu alitoa vitu adimu sana kwa bi mdogo yule na kumfanya kupayuka mijineno mengi isiyo na maana. Usiku ukaisha vizuri kabisa wote wakiwa hoi lakini kwa furaha.
"Ikiwa hivi kila siku hata ukiondoka mwezi usipoaga mi sina neno, ila ww hunipi huduma kama hizi kwa ukamilifu halafu waondoka, mi napata wivu najua unaenda kuwapa wengine huko"
Maneno yaliyomtoka bi Sauda asubuhi baada ya kumuamsha mumewe ili akaoge.
Mr.Khatib alimwangalia kisha akatabasamu bila kuongea neno lolote.★★★★★★★★★★★★★
"Haya nambie boss, ni kazi gani maalum iliyokuleta hapa leo, maana najua wewe Khatib anakutumia kwa kazi maalum tu." Hisham aliongea baada ya kufahamiana na Noor kwa sura sasa, wakiwa katika meza fulani iliyozungukwa na viti vitatu ndani ya Mambo pub, ilikua ni majira ya saa 2:19 usiku.
"Kuna bint anaitwa Alice nimekuja kufanya mahojiano nae maalum".
"Vipi ameleta kujifanya kujua?" Alihoji Hisham akiwa na hamu ya kujua nini kinaendelea hapa.
"Yaah alijaribu kumuuliza boss nahis kuhusu vtu flan vilivyoashiria kumfuatilia, maana amenambia nifanye nae deep conversation."
"Okay, kama ameanza kuleta kidomodomo poteza tu" Alisema Hisham ambaye alionekana kuwa hakua hata na chembe ya huruma.
"Ntaangalia mahojiano yetu yatakavyokua maana sometymz lisilo budi hutendwa" Aliongea kwa busara kidogo Mr.Khatib.
"Wewe unaremba sana, watu hawa ni hatari sana zaidi ya Ebola, wanatakiwa kufa mapema bla ya kuambukiza wengine.." Bado aliendelea kusisitiza Hisham Omari Mikidadi, safari hii akigonga meza na ngumi na kunyanyuka kuelekea ofisini kwake ndani ya pub ile.
★★★★★★★★★★★★★★
Don't Miss Episode O5
 
Mdharuba mbona umeirudia ep 04??!
Pia utakuwa unaweka ep ngapi kwa siku?!

Ila safi sana simulizi tamu sana

Itakua nimejichanganya..ngoja niweke ya 5..
Kwa siku naweka moja tu
 
STORY: HISTORIA BATILI-Fake History
MTUNZI: JUMAA KHATIB MDHARUBA(JK)
+255 718 274 130

SEASON O1-EPISODE O5
★★★★★★★★★★★★★★
"Haloo, kama zali yani, Khatib amenipa pesa na kunambia tukutane Mambo pub saa 3 usiku wa leo.." Ni sauti ya Alice katika sikio la bwana Ahmed Khamis Hamad.
"Mwanzo mzuri huo" Aliongea Ahmed na kuongeza.."Nenda nipo nyuma yako" kisha akakata simu.
Ahmed Khamis alikua kijana mmoja shupavu aliyekuwa anafundisha Somo la Stadi za kazi katika shule ya Msingi Mazimbu na pia alikua ndio Mwalimu wa Michezo katika shule hii.
Ila Ahmed alikua akifanya kazi pia kama Afisa usalama wa serikali ya Tanzania. Aliifanya kazi hii kwa miaka saba sasa lakini hakuna aliyekuwa anatambua hilo.
Baada ya kukabidhiwa jukumu la kufuatilia juu ya utajiri wa Mr.Khatib, ndipo alipokutana na Alice na njia pekee ya kumrubuni Alice ilikua ni kumtongoza awe mpenzi wke ili aweze kumtumia vizuri katika harakati zake.
Alishampa HISTORIA BATILI Alice kuhusu yeye(Ahmed) na Khatib na kudai kuwa Khatib aliwahi kutumia pesa zake nyingi kumrubuni mkewe mpaka wakafikia hatua ya kuachana. Kwahy kwa sasa alitaka kujua undani wake ili amchongee polisi aje amkamatishe katika mikono ya dola. Alice, kwa sababu ya uaminifu aliokuwa akionyeshwa na Ahmed na jinsi alivyokuwa akipewa pesa kila alipohitaji na saa zngne hta kabla hajaomba, alijikuta akimpenda sana mwalimu yule wa michezo. Akawa anafanya vile ambavyo Ahmed alimtuma kufanya.
Alice alikua akifanya mambo kwa upande mmoja akiwa hajui kuwa alikua akitumika vibaya. Upofu wake katika kupenda ulimfanya awe ----- sana na hakuwa hata na muda wa kufikiria katika alichoambiwa. Mwenzie Ahmed alishajua kuwa Khatib ni mtu hatari na anaweza kufanya chochote, kwahyo Alice akishindwa kumsaidia kufanikisha kazi angetafuta mtu mwengine ambaye angemtumia kama msaada. Hata kama Alice angeuawa hilo si jambo geni kwake, alishazoea..
********************
Alice alifika pale Mambo pub majira ya saa 2:56 usiku na moja kwa moja akatafuta meza ambayo ilikua haina mtu akafika na kukaa kwenye kimoja kati ya viti vilivyoizunguka meza ile.
"Unatumia kinywaji gani?" Swali lililotoka kwa mmoja kati ya wahudum wa pub ile..
"Naomba Kuku nusu"
Akakaa pale kwa muda wa dakika 6 na kushika simu yake na kuanza kupiga namba za Khatib. Simu haikupokelewa na badala yake ilikatwa kisha meseji ikaingia ikisomeka "Am driving, on my way to Mambo Pub, plz wait for me..i'll be there within 15 minutes" . Baada ya kusoma msg hii akaifoward kwa Ahmed kisha akaweka simu katika pochi yake ndogo na kuendlea kugonga kuku wake bila hata woga.
"Naweza kukupa kampani,? naona upo peke yako" Aliulza bwana Noor baada ya kufika katika meza ya bi Alice huku akimuangalia vizuri usoni kuhakikisha"
"Mmmh...aaaah.. kuna mtu namsubiria bado hajafika, unaweza kunipa kampani mpka atakapokuja" Alijibu Alice, tatizo lake kubwa Alice alikua hajui kukataa hasa pale anapoona dalili za pesa.
"Ok, asante sana.."
Alikaa pale bwana Noor na kuanza story za hapa na pale na bi Alice.
"Umesema unamsubiri nani vilee maana nshasahau eti mara moja hii.." Noor aliuliza swali la kimtego akijidai kama vile aliyetajiwa jina mwanzoni..hapa alikua anatafta pa kuanzia..
"Yaani nina promise na Mr.Khatib yule wa Saukhat Investment Company.. si unamjua??" Aliingia mzima mzima Alice pale alipokusudiwa kufika.. akiwa hajui kuwa maongezi haya yanasikika moja kwa moja katika sikio la Khatib kupitia earphone alizovaa akiwa kitandani na mkewe.
"Nasikia yule bwana ana pesa vibaya sana ila watu hawajui anafanya biashara gani haswa" Alianza kuchochea Noor.
"Yule ni balaa..kama sio unga sijuuii.. , maana nina waswas ile Euler hotel pia anamiliki yeye" Alijiachia Alice akiwa hana hili wala lile.
"Labda alirithi mali nyingi sana, maana nasikia babaake alikua tajiri mkubwa sana halafu alizaa watoto wawili tu" Noor Alijaribu kuigusia fake history kuangalia Alice anaichukuliaje..
"Sidhani, hata kama ni hivyo itakua bdo ana kitu cha ziada yule..Unajua kwanin nakwambia hvyo?? Yule anaweza akapotea hata mwezi nasikia hajulikani yuko wapi? Afu mbaya zaid hadi mkewe hajui..Naskia anapata tabu kweli mtoto wa watu anatafta mpka anakoma" Maelezo haya ya Alice yalianza kumpa picha flani Noor..lakin bdo akaendelea kuchimba zaid..
"Kwahyo unataka kunambia hyu mtu anaweza kuwa ni mafia?"
"Inawezekna maana nasikia pia ni mbabe, akitaka lake ndo hilo hlo..kwa mfano mi yule boyfriend wangu alishamgombanisha na mkewe..halafu baadae yule mwanamke alimtumia watu wamuue.." Maneno haya ya Alice yakampa picha Noor kuwa huyu Alice yupo nyuma ya mtu flani..Sababu Historia hii anayompa sasa ni ya kutunga-FAKE HISTORY. Mpaka hapa hakukuwa na sababu ya kumuacha Alice mzima, ingawa alitakiwa kufanikisha kumjua nani hyo yuko nyuma ya Alice..
"Yaaah nshawahi kusikia kitu kama hicho, ila huyo jamaa tu ndo simjui..na nasikia yupo Morogoro hii hii.." Noor aliongea kwa kujiamini na kuonyesha kuwa si mgeni na hizi habari ili apate kujua undani wa habari hii..wkati huu Noor alishamnunulia Alice pombe kali na kujikuta ameshasahau pia kuwa alikuja pale kwa madhumuni yapi.!!
"Boyfriend wangu ni mwalimu wa Michezo shule ya Msingi...." Kabla hajamalizia sentensi hii Alice alianguka pale alipokuwa amekaa huku damu nyingi zikimtoka kichwani..
★★★★★★★★★★★★★★
Mama Mdharuba, alianza kutilia mashaka juu ya mwanae Khatib kuhusu mambo anayoyafanya hivi karibuni. Na kabla mambo hayajawa mabaya aliamua kumuita mwanawe na kumpa onyo.
Pamoja na ubabe wke wote, Khatib hakuwahi kumdanganya mama yake kitu chochote..hivyo alipouliza kitu chochote na mama yake alikua hana option zaid ya kuongea ukweli!!.
Jumapili hii aliamua kuja kumuuliza maswali mawili matatu yahusuyo maisha yake kwa ujumla na mwenendo wke wa sasa.
"Nasikia sasa hivi umeanza kujiingiza katika biashara haramu mwanangu, ni kweli?" Aliuliza Mama Mdharuba wkat wako mezani wakipata chakula cha mchana..wakiwa na mdogo wake Khatib, Hawa ambaye alikua akiishi na mama yake katika jumba lile kubwa lililopo maeneo ya Mbezi.
Khatib alikaa kimya kana kwamba hajasikia swali hili..
"Siku zote nimekuwa nikikwmbia kuwa mimi sipendi niongee halafu ukae kimya..Naomba unijibu, unafanya biashara haramu au hufanyi?" Mama Mdharuba alianza kufoka.
"Mama nisikilize, hizo biashara sio zangu, ni za watu, mimi sina hata fungu katika hizo biashara mama!" Alijaribu kujitetea Mr.Khatib huku mamaake akimsikilza kwa makini.
"Siku zote nakwambi kuwa sitaki ushirikiane na watu wanaofanya biashara za haramu, sipendi na sitaki!! Kwanini hunisikilizi?? Mali zote hizo ulizokuwa nazo unatafuta nini tena mwanangu??"
Hapa Khatib alikuwa kama aliyemwagiwa maji ya baridi.
"Sasa ni hivii..ukirudi tena hapa nisikie umeacha hizo biashara zako za kipuuzi, la sivyo mimi na mwanangu tutakuachia nyumba yako turudi kuleee tulipotoka, nadhani unapakumbuka vizuri".Aliweka kituo kikubwa Mama Mdharuba na kumfanya Khatib azidi kutahayari.
"No mama plz usiseme hvyo.."
"Nasema hivyo sababu ya ujinga wako, mtoto mdogo namna hyo hata miaka 30 hujatimiza umekua na tamaa ya pesa kiasi hicho mpka unafanya biashara haram?? Sasa mi ntakukimbia..nakwambia hivyo.."
"Nimekuelewa mama, ntaachana nayo".
"Huyo mwenzio wa Canada ndo alokushawishi mfanye hiyo biashara??" Aliuliza swali la kizushi mama Mdharuba.
"Hapna mama, yeye hata hajui"
"Sasa ni nani mwengne mwenye uwezo wa kukushawishi?? kumbe wewe umekua mpuuzi siku hizi eeh?? Pumbaaavu" Alipatwa na hasira mama Mdharuba na kumzaba Khatib kibao cha shavu la kushoto.
★★★★★★★★★★★
Watch out epsode 06
 
STORY: Historia Batili
MTUNZI: Khatib Jumaa Mdharuba.
+255 718 274 130

SEASON O1-EPISODE O6
★★★★★★★★★★★★★★
Tukio la Alice kupigwa risasi ya kichwa lilimshangaza sana Noor sababu hakutegemea.. Alipigwa risasi kutoka katika bunduki iliyokuwa imewekwa kiwambo cha kuzuia sauti. Hivyo hawakuweza kusikia mlio wa risasi na hawakujua imetokea wapi..
Wakati bwana Noor amemuita Hisham wakiwa wameduwaa wakijishauri cha kufanya huku baadhi ya wateja wa Pub ile wakiwa wameshajua nini kinaendelea..Ghafla ikaingia gari ya polisi aina ya LandCruiser na kubeba mwili wa marehemu huku wakimchukua bwana Noor kwa mahojiano zaidi.
"Sheenzi kabisa, hawa Mbwa sijui wamepata wapi taarifa za haraka namna hii" Alilalama Bwana Hisham huku akielekea Ofisini kwake kujiandaa kuelekea kituo kidogo cha Polisi cha Msamvu ambapo ndipo Noor aliachwa pale na polisi wakaelekea katika hospital ya Mkoa Morogoro kwa ajili ya uchunguzi wa maiti ya Alice..
"Nani ndio mkuu wa zamu kati yenu??" Swali aliloanza nalo Hisham punde tu baada ya kufika kituon hpo na kukutana na askari watatu wa kituo kidogo cha Msamvu.
"Aisee hii mijitu mingine sijui ikoje jjamani, jitu rinakuja hapa rinakuta watu hata saramu harina.." Alilalama polisi mmoja na kuelekea ndani ya kituo kile na Hisham kufuatia nyuma..
"Wewe umekuja hapa kusalimiwa au kufanya kazi?? Kama unataka kusalimiwa tembelea Nursery huko au shule za msingi" Alibwabwaja Hisham akionesha ujeuri wake na yeye..Kikubwa kilichomshaua bwana Hisham ni pesa alizokuwa nazo katika biashara zake haramu walizokuwa wakishirikiana watu wawili, yeye na Manager wa Euler Hotel Mr.Haroun Rashid na kwa sasa wakiamua kumshirikisha Mr.Khatib kama mtu wa tatu ambaye alikua na urahisi wa kuzitoa cocaine na Heroine Canada na kuzivukisha boda bila wasiwasi mpaka Tanzania kwani alishasafirisha mizigo kwa muda mrefu sasa kati ya nchi hizi mbili hivyo alikua na urahisi katika kazi yake.
"Sema shida yako sasa nakusikiriza" Aliongea askari yule ndani ya kituo kile kidogo cha polisi..
"Nahitaji kumwekea dhamana Mr Noor A Mdharuba ambaye ameletwa hapa kituoni muda si mrefu" Hapa Hisham alionekana kuongea kwa busara kidogo.
"Huyu muuaji??" Aliuliza askari yule akimkodolea macho Hisham na kumfanya Hisham ahamaki..
"Muuaji?? kwani mmeshafanya uchunguzi na kubaini kuwa yeye ndiye aliyeua?"
"Hapana, ila yeye ameletwa hapa kwa kesi ya mauaji na tunahitaji kufanya mahojiano naye zaidi"
"Sasa wewe una mamlaka gani ya kumuita kuwa ni muuaji wakat hata mahojiano bado?? Au umechanganyikiwa??" Safari hii Hisham alishapanic..
"Mimi sijachanganyikiwa, ila huwezi kupata dhamana ya hyu mtu mpaka tufanye naye mahojiano kwnza"
"Fanyeni basi mahojiano mimi namsubiri hapa" Aliongea hivyo Hisham akidhani taratibu za kipolisi ni za rahisi kiasi hicho.
"Hapana, huyu ataandika maelezo kesho asubuhi halafu ndo tuangalie utaratibu wa dhamana, kwa leo atalala hapa" Alimalizia maelezo yule askari na kumuamuru Hisham atoke nje ya kituo kile..
Hisham akatoka na kuingia katika gari lake akiwa hajui nini cha kufanya..
Akaamua amtumie ujumbe Mr Khatib juu ya tukio lile.
Mara simu yake ikaita, akapokea na kuweka sikioni.
"Nafahamu kila kitu Hisham, rudi nyumbani kapumzike" Kisha simu ikakatwa, hiyo ilikua sauti ya Khatib akiongea akiwa nyumbani kwake.
Kisha akapiga simu ya mkononi ya mkuu wa kituo kidogo cha polisi pale Msamvu..
"Haloo Mkuu, kuna kijana anaitwa Noor yupo hapo kituoni kwako ndio ameletwa usiku huu, huyo ni wangu"
"Ok boss, nko nje ya kituo sina taarifa samahani sana" Alisema askari yule kisha akakata simu.
Simu kituoni ikaita na akapokea askari aliyekuwa mkuu wa zamu siku hiyo akaonekana kukubaliana kitu kisha akakata simu.
Akaelekea moja kwa moja katika chumba kimoja kidogo kilichokuwa na giza sana na mlango wa chuma, akafungua na kumruhusu Mr Noor atoke.
★★★★★★★★★★★★★★
Ilikuwa ni jumapili moja ambayo bi Sauda alikuwa nyumbani akifanya usafi na kujaribu kupanga panga vizuri vtu vya nyumbani baada ya kumaliza kufua kazi ambayo aliianza tangu saa 11 alfajiri na kuikamilsha saa 1 asbuhi. Licha ya kuwa ofisi yao ilifunguliwa pia siku za Jumapili na kufungwa mapema, lakini Jumapili hii Sauda aliamua amuachie majukumu yote Nira ili aweze kusimamia maendeleo ya pale sehemu yeye akifanya majukumu haya ya nyumbani siku ya leo.
Akaamua kuzitoa nguo zote kabatini ili azipange upya. Akaanza na za kwake ambazo alizitoa zote na kuzikung'uta vumbi na pia akafuta vumbi pale kabatini kisha akazikunja upya na kuzirudisha kabatini katika mpangilio mpya!!.
Akahamia upande wa nguo za mumewe na kuzitoa zote na kuzitupia kitandani na ili azikunje upya. Ndipo alipohisi kama kuna ktu kimeanguka kutoka katika zile nguo alizozitoa pale kabatini. Akajaribu kuangalia vizuri pale chini akaona kitu kama kitabu kidogo hivi cha kijani. Akakishika na kuangalia vizuri akagundua kuwa ni pasi ya kusafiria. Akaweka pembeni kisha akaendelea na zoezi lake la upangaji nguo.
Alipomaliza akachukua ile pasi ya kusafiria na kutaka kuirudisha mle kabatini, lakini kabla ya kuirudisha akaamua kuifungua na kuikagua mle ndani.
Akaipitia kwa makini sana na kujikuta akihamaki kwa nguvu..Laahaaaulaaa!! Akiweka mkono wake mdomoni huku mdomo ukiendelea kubaki wazi akiwa haamini anachokiona hapa!!
Pasi hii ilionesha kuwa muhusika alionekana kusafiri kutoka Tanzania kwenda Canada na baadaye kutoka Canada hadi Norway wiki 5 zilizopita.. Akajaribu kukumbuka kilichotokea, akanyong'onyea.
Wakati bado anaendelea kutafakari huku akiichunguza vzuri hii pasi, akagundua kitu kingine ambacho kilimstua zaidi.
Pasi ilikua na picha ya mumewe-Khatib, lakini majina yaliyokuwepo katika pasi ile ni Mwatete Mwandaro Mwinjuma!! Akazidi kuduwaa mara hii akiegemea kioo cha kabati lile taratiib akielekea kukaa kitako sakafuni huku macho kodo katika 'Passport' ile.
Wakati yupo hapa chini amekaa kitako, likaja wazo moja kichwan kwke ambalo aliamua kulifanyia kazi..
Akanyanyuka kutoka pale chini na kurudi pale juu kabatini kisha akatoa nguo zote za Khatib akazitupa kitandani na kuanza kufanya 'search' ya maana..
Alikutana na vitu viwili vingine ambavyo vilizidi kumuumiza kichwa..
Kwanza, alikutana na kitambulisho cha kupigia kura ambacho kilikuwa na picha ya mumewe na jina lile la Mwatete Mwandaro Mwinjuma kitambulisho kilichotolewa katika kijiji cha Kiwavu Kata ya Tongoni, Wilaya ya Tanga mjini, Mkoani Tanga miaka 8 iliyopita.
Pili, alikutana na Cheti cha kuzaliwa kikiandikwa Jina mtoto kuwa ni Mwatete na jina la baba kuwa ni Mwandaro Mwinjuma, cheti kikionesha mtoto amezaliwa Hospitali ya Mkoa ya Bombo Mkoani Tanga tarehe 14/10/1987. Hapa aliduwaa zaidi maana hii ndio tarehe aliyozaliwa mumewe.
"Mwatete?? Mmmmh..na hii Khatib imekujaje? Mbona sielewi hapa?" Alijiuliza moyoni bi Sauda baada ya kujiridhisha kuwa hivi vitambulisho vyote ni vya mumewe.
★★★★★★★★★★★★★★
Don't Miss Episode O7.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom