STORY: HISTORIA BATILI(Fake History)
MTUNZI: Jumaa Khatib (Jk)
+255 718 274 130
+250 726 023 140
EPISODE O7
★★★★★★★★★★★★★★★
Baada ya kujihakikishia kuwa mumewe ni mtu tofauti na wengi wanavyomjua, Sauda aliamua kutunza maswali yake ili aje amuulize mumewe 'live' atakaporudi..
Kwanini ananifichaficha vitu?? Alijiuliza swali hili moyoni mwake, akiamini alistahili kujua kila kitu kuhusu mumewe..
Leo lazima atanieleza, au sivyo anipe talaka yangu, nimechoka mi, mwanaume gani asiyeeleweka?, kila siku nagundua mambo mapya tu..aaaghh Bado alizidi kujipa tabu za mawazo bi Sauda akiupa tabu sana ubongo wake na kutaka kujua undani haswa wa mumewe..
*******************************
Kifo cha Alice kiliwashangaza wengi sana, kwa maana hakuna maelezo yoyte yaliyotolewa polisi juu ya nani aliyempiga risasi na kwanini apigwe risasi.. Kila mtu alibaki kuduwaa tu na kukosa kujua nini hasa kisa na mkasa..
Shoga yake Alice, Flora, alikua akilia saana pale msibani, akiwaza mambo mengi sana yaliyotokea jana tu alipokua na shoga yake Alice pale Euler Hotel, na mpaka wanaagana akimwambia kuwa ana promise na Mr.Khatib, akakumbuka pia maongezi yao mchana wa jana kuhusu Mr Khatib na jinsi Alice alivyomtilia mashaka, alibaki kulia tu!!. Wazo la haraka kichwani mwake ni kuwa Mr Khatib alihusika na kifo cha Alice, lakini atamwambia nani maneno haya?? Khatib alikua mpole sana mbele za watu, na alikua mtu wa watu haswa,, nani atakuelewa kuwa yeye alihusika na mauaji ya Alice wakati hata hakuepo kwenye tukio usiku ule..!!
Ukweli kuhusu kifo cha Alice waliufahamu askari, kwani aliyewapigia simu alikua ni Ahmed Khamis, afisa usalama wa Taifa,, na aliwaeleza pale ambapo Alice alifikia kutaka kutoa siri za Ahmed baada ya kulewa!! Kwa Ahmed, Alice alishakua useless, maana alifika pabaya, na dawa wakati ule ilikua moja tu-Kifo!! Na ndo kilichotokea, huo ukawa mwisho wa safari ya uzima wake aliyoianza miaka 25 iliyopita, RIP Alice ni maneno aliyoyatamka Ahmed kabla hajamfyatulia Alice risasi ya kichwa usiku ule..
Hakuna aliyehoji sana, kila mmoja alionekana si mhusika juu ya kifo cha Alice Tupa Nemhina, ni Florah pekee ndiye aliyeteseka na mawazo ya kila siku, na kila alipomuona Mr Khatib alikua akikumbuka maneno ya mwisho ya Alice juu ya promise ya kukutana na Mr Khatib na ndo ukawa mwisho wa Alice.. Aliteseka sana kimawazo, ila baadae alizoea, akibaki na siri ile moyoni mwake.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Nataka unieleze ukweli, kuhusu hivi vitambulisho vyako Alihoji Sauda baada ya kutoa vitambulisho kabatini na ile pasi ya kusafiria akimuonyesha Mr Khatib aliyekua amekaa mbele ya 'screen' ya Computer pale ndani ya chumba chao..
Khatib alionekana kushtushwa sana na taarifa hii, akaangalia vizuri documents zile za siri, kisha akamuangalia saana Sauda pasi na kumjibu chochote, akageukia screen ile na kuendelea na kazi zake..
Khatib, naomba uniambie hivi vitambulisho mbona vina majina tofauti wakati sura ya kwako,?? Vipi haya mambo??. aliendelea kuhoji Sauda alipoona Khatib hajangea kitu mwanzoni..
Vitambulisho vina sura ya nani?? Alihoji Khatib baada ya 'kupata moto'
Sura yako Alijibu Sauda ambaye alikua haelewi kuwa kufahamu kuhusu vile vitambulisho ni kosa ambalo haliwezi kumbakiza tena duniani, yeye alikua anaona ana haki tu ya kuhoji chochote kuhusu mumewe..
Sasa kama vina sura yangu wewe vinakuhusu nini mpaka kutaka kujua?
Mimi ni mkeo, nina haki ya kujua kila kitu kuhusu wewe, sababu ni mume wangu..
Pole sana, haki hiyo hapa kwangu umeikosa
Khatib naomba unieleze vizuri, sababu unavyoendelea kunificha utanifanya niondoke hapa bila kuaga
Nisikilize vizuri wewe mwanamke, tena nisikilize vizuri sana.. Alianza kuongea kwa msisitizo Mr Khatib na kufanya Sauda akodoe macho huku akitega masikio yake vizuri kutaka kujua Khatib anataka kuongea nini!!
I was born ME, I and MySelf, you are now trying to change the word "ME" to be "US" something that will NEVER happen..
Anhaaa, kwahiyo mimi unanichukuliaje? Unanichukulia mimi mwehu, mwendawazimu, mpuuzi au malaya tu nsiyejielewa hapa? Alihoji Sauda ambaye alishapanic wakati huu..
Mimi nakuchukulia vyote vinne ulivyotaja, na cha tano ni kuwa wewe ni ---- pia, hiyo umeisahau
Majibizano haya makali yaliendelea na kumfanya Sauda aone kuwa mumewe amebadilika saana siku hiyo tofauti na alivyomzoea.. Alipata tabu sana, alijitahidi 'kuchimba biti' vya kutosha lakini Khatib wala hakujali.. Akabaki analia tu. Mwishoni akanyamaza akapanda kitandani akiwa na hasira na mawazo tele, baadae akapitiwa na usingizi, akalala akimuacha Khatib katika kioo cha Computer pale chumbani..
Khatib alifikiria sana juu ya hatma ya yule mwanamke pale kitandani, akaanza kumuonea huruma, akakumbuka maneno ya babaake mdogo Noor akawa hana option.. Kulibaki jambo moja tu kutekelezwa mda ule, Sauda auwawe..
Alikaa pale mezani kwa mda mrefu sana akitafakari..baada ya muda mrefu kupita akanyanyuka na kufungua kabati, akazama chini kabisa akatia mkono akapapasa papasa akatoka na kikaratasi kidogo kilichofungwa vizuri..akakifungua akatoa unga uliokuwemo mle ndani, akikamata na vidole vyake viwili,cha gumba na kinachofuatia..akaenda kumpaka Sauda karibu na tundu zake za pua..
*******************************
Kosa kubwa ambalo alilifanya sauda ni haraka ya kutaka kujua mambo yanayomuhusu huyu mumewe..Licha ya kuwa alishaona dalili za wazi kuwa huyu si mtu wa kawaida..hakujali, alidhani anaweza kucontrol maisha yao na wakaishi kama mke na mume wanaopendana sana..Kumbe alikosea..kwa Khatib haikua hivyo, ni tofauti sana..,, Khatib alikua anamuona kila mtu ni adui yake, yeyote anayetaka kujua undani wa maisha yake basi hakuwa na mwisho mzuri, na ndo kinachomkuta Sauda kwa sasa..Khatib aliona dalili za wazi za Sauda kutaka kufuatilia maisha yake, na ndio maana kwa miaka yote miwili aligoma kabisa kuzaa nae..Angewezaje kumuua mama wa mtoto wake?? Baadae atajibu vipi maswali ya mwanae kuhusu mama yake??!! Aliamua kumchunguza kwa undani kwanza.. Na haya ndo matokeo ya uchunguzi..ameamua kumuua..kwa sumu ya unga ambayo anaivuta kupitia pumzi anazoingiza mwilini..ndani ya dakika 10 tu tangu kupakwa ule unga Sauda alishafariki
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Dont Miss Episode O8