Usifungwe na historia yako

Usifungwe na historia yako

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
604
Reaction score
552
Hakuna kitu watesi wanakipenda kama historia. Utahukumiwa kwa maamuzi na maisha uliyoishi jana. Utatiwa unyonge kwa historia yako mwenyewe uamini kuwa maisha ya jana hayabadiliki na ukishakosea ndio basi. Watesi huamini nyakati haziwabadilishi watu. Ulivyokuwa nyakati hizo ndivyo utakavyoendelea kuwa.

Maisha hutuletea watu wema, wenye ukuu ndani yao, wasiokung’ang’ania kwa makosa ya jana. Hawa ‘wanakuhukumu’ kwa huangalia zaidi kile ulichonacho, kule unakokwenda na uwezo wako wa kubadilika.

Watu wema hutambua ni kweli shuleni ulizungusha lakini hiyo haimaanishi hukuwa na nafasi ya kujifunza maisha. Hutambua ni kweli ulizalia nyumbani, lakini hiyo haimaanishi ulikuwa mtu mbaya kuliko wasiozaa. Hutambua ulikuwa jambazi lakini hiyo haimaanishi huwezi kuwa Mchungaji.

Watu wema, kwa hakika, hutambua nguvu ya makosa na historia katika kumfundisha mtu somo muhimu linalobadilisha maisha.
 
Back
Top Bottom