STORY: HISTORIA BATILI
MTUNZI: Mdharuba, Khatib Jumaa
+255718274130
+255756274130
EPISODE O15
1⃣5⃣
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Noor A Mdharuba, ambaye ndiye alikua na jukumu la kusimamia usalama wote wa mwanae huyu mlezi, kuhakikisha anafanya vile anavyotaka, na anaishi kwa amani..
Noor ndiye aliyekuwa akifahamiana na watu wote 'wazito' serikalini, katika kila sekta ambayo huenda kwa namna moja ama nyingine inaweza kumletea tabu Khatib na akashindwa kufanya mambo yake kwa ufanisi..
Naona vijana wako wanakuja kwa kasi sana kutaka kumueka Khatib mbaroni, ni wewe ndiye umewaagiza kufanya hivyo au ni wao vimbelembele tu? Noor alianzisha mazungumzo wakiwa katika baa moja maarufu jijini Dar na mkuu wa kitengo cha makosa ya jinai katika Idara maalum ya usalama wa taifa.
Wanatekeleza wajibu wao, waache wafanye kazi!! Ila endelea kuwa na amani tu kwani mimi ndiye NINAYEWATUMA..mimi ndiye mkuu wao wa kazi, mimi ndiye boss wao.. Ally Ngoswe, ambaye ndiye mkuu wa kitengo hiki ambacho anasimamia Rukia akiwapangia kazi Ahmed na Nuro, alimtoa uoga Noor kisha wakagongesha glass wakinyanyua vinywaji vyao juu ishara ya kuonyesha upendo na amani..
Ila ni muda mrefu sana kaka, sijasikia kutoka kwako Aliuliza Ally akimuangalia Noor kwa jicho la wizi akiwa amenyanyua glass yake ya kinywaji ikikaribia mdomoni.
Yaani ndio maana leo nimekuita hapa aliongea Noor na kumfanya Ally ashushe glass yake ambayo alishapiga funda moja na kuachia tabasamu pana.
Wakaongea mengi yanayohusu biashara zao ambazo alikua pia Noor akishirikiana na Ally..Wakanywa, wakapiga story zingine za kimaisha..
Kabla ya kuondoka eneo lile, Noor alitoa bahasha kutoka katika briefcase yake..na kumkabidhi Ally..!!
Safari hii naona mambo mazuri..maana naona bahasha siyo ile niliyoizoea.. Ally alimuuliza Noor huku akitabasamu wakati anapokea bahasha ile ya kaki..
Yaah..nimeamua kukukomoa kaka..hizo ni milioni 12 Noor naye aliongea huku akitabasamu..
Kweli umenikomoa, nakumbuka mara ya mwisho ulinipa 7 tu, leo 12..kuna 5 zaidi.. Kaka nashukuru sana..tuko pamoja.., keki za taifa tutakula pamoja kaka, wala usijali.. Maneno yalimtoka Ally baada ya kukabidhiwa kitita kile kinene na bwana Noor..
Asante sana, nashukuru sana kaka..ukifa wewe mi nitapata tabu sana hapa duniani Noor nae alitoa shukrani zake huku akitania na kumuacha Ally akicheka.. Wakaagana kisha kila mmoja akashika njia yake.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Hatujapata bado damu ambayo ina match..huyu aliyetoka sasa hivi hapa ana damu grup O lakini ana virusi.. Alijibu Dokta Elisha baada ya swali lile lililotoka kwa Daktari Msaidizi..Idd Fauz.
Mimi nilikua sijaelewa tatzo..basi naomba unitoe damu yangu mimi, maana hata mimi ni O..
Ok sawa..
Dr Elisha alifanya haraka akishirikiana na Dr Idd kuokoa maisha ya Abdul..damu ya Dr Idd haikua na tatizo lolote, hivyo walifanikisha zoezi lile haraka..
Unajua ni jambo la kusikitisha sana kumpoteza kijana mdogo namna hii..hizi ndizo hazina za taifa la kesho Aliongea Dr Idd wakati akitundika drip ya damu katika kitanda cha Abdul..
**********
Wakati taratibu za Abdul kuwekewa damu zikiendelea, Mama Mdharuba alikua akiendesha kwa kasi sana gari yake kuelekea Hospital ya mkoa..pembeni akiwa na mwanawe Hawa ambaye ndiye alitakiwa kuchangia damu..Hii ni baada ya Hisham kuwapigia simu waje hospitali haraka baada tu ya Regina kutoka katika chumba cha daktari.. Wakafika hospitali,moja kwa moja Hisham akawaelekeza walipokua..
Hali ya mgonjwa inaendelea vizuri kidogo kwa sasa.. Kuna daktari amejitolea damu baada ya kuona hali ni mbaya..yaani tulikua karibu kumpoteza mtoto..lakin tumshukuru sana huyu Daktari mwenye moyo wa huruma kwakweli..ni watu wachache sana wenye moyo huo.. Hisham alikua akifunguka kwa Mama Mdharuba na Hawa..
Wakakaa pamoja mpaka baadae waliporuhusiwa kumuona mgonjwa..wakati huu Hamida bado alikua katika chumba cha kupumzika licha ya kuwa alishazinduka..
Nana, Hisham, Regina, Mama Mdharuba na Hawa wote wakaongozana kwenye chumba ambacho Abdul alilazwa na kwenda kumuona..Hali yake ilikua ikiendelea vizuri tu!!
Baada ya kuridhishwa na hali yake, wote kwa pamoja walitoka na kwenda kupumzika kwenye benchi wakisubiri Hamida apate nafuu ili wamkabidhi jukumu la kubaki na mtoto hospitali ili wao wakaendelee na majukumu mengine..
Mama Mdharuba alitumia muda huu kuongea mawili matatu na bi Nana Amiry..
Mi naona ni wakati muafaka wa hawa watoto kuwa pamoja kwa sasa..washirikiane kumlea mtoto wao Mama Mdharuba alijikuta akiropoka maneno haya baada ya mazungumzo marefu..
Unasemaajee??!! Hapana, wala usifikirie hicho kitu, kwani alipooa mke mwingine Hamida hakuwepo? Au kwakuwa sasa mkewe kamuua?? Unafikiri hatuna habari kuwa mkewe kamuua? Unataka na Hamida akafe mwanangu?? Loooh ishia hapo hapo..bado nampenda mwanangu.. Nana alionekana kubadilika ghafla baada ya wazo la Mama Mdharuba.
Maneno haya yalimfanya Mama Mdharuba kuchukia, akamshika mwanae Hawa mkono moja kwa moja wakaondoka eneo lile la Hospitali kwa hasira..
*************
Hisham, alimshuhudia Mama Mdharuba akiondoka bila kuaga, tena akionekana amechukia..akamfuata Nana na kumuuliza..
Mama, kuna tatizo lolote kwani?
Mwanamke hasidi tu yule, eti anataka Hamida aolewe na mwanawe..hana haya kweli..
Duuh, nyie ni wazazi lakini, mngeelewana tu mama
Tuelewane nini banaa..hebu niondolee upuuzi wako na wewe Aliongea bi Nana ambaye alionekana kukasirika haswa..na hakutaka kukubaliana na hili jambo hata kidogo..
Ila mimi naona pia hakuna ubaya, kama boss atamuoa Hamida nadhani utakua muda mzuri zaidi wa kulea pamoja mtoto wao Hisham ambaye siku zote hakwenda kinyume na jambo la Khatib, liwe la maana au la kijinga alishauri..
Na wewe koma, tena ukome..usinitibue saa hizi.. Kwani nyinyi tabia zenu hatuzijui mnafikiri? Mama Hamida alifoka na kumfanya Hisham kuwa mpole..
Samahani sana mama, nisamehe nimekosa..
Baada ya kuomba msamaha, Hisham alijivuta pembeni na kutaka kuandika email ili amjulishe Khatib juu ya yanayojiri..
Baada ya kuiandika, wakati anaituma ndipo alipogundua kuwa MB 8 alizopewa baada ya kujiunga kifurushi kwa siku hiyo zimeisha..
Licha ya pesa alizokuwa nazo, ila Hisham alikua mgumu sana katika matumizi yake ya pesa..
Simu ambayo ndiyo muhimili wake mkuu wa mawasiliano, yeye alikuwa akitumia 500/- tu za Kitanzania kujiunga kifurushi kwa siku..
Naomba simu yako nitume e-mail kwa boss, situation haiko poa hapa.. Hisham alimuomba mkewe Regina simu..yeye hakufikiria kuongeza salio.
Ok..kama unataka kupiga dakika nimemaliza..ila kwa e-mail MB zipo Alijibu Regina na kumkabidhi Hisham simu yake..
Mimi natuma e-mail tu.. Hisham alichukua simu na kujisogeza pembeni..ila baada ya sekunde kadhaa akarudi kwa Regina..Pattern mke wng..
Ok, lete nkutolee..
Pamoja na kuishi nae kwa muda mrefu sasa, Hisham alikua hana kawaida ya kushika simu ya mkewe..Na hii ilikua ni moja ya sababu ya kumzuia Regina kushika simu yake.. Kwani mara zote Regina alipotaka kushika simu ya Hisham alipata karipio kali huku akiulizwa Mbona mimi simu yako sishiki?. Mwanzo ulikua mgumu kwa Regina ila baadae alizoea..
**
Baada ya kutuma e-mail juu ya ugomvi uliotokea pale hospitali kati ya Mama Mdharuba na Mama Hamida, Hisham alikua bado ameshikilia simu ya Regina akisubiri majibu kutoka kwa Khatib..
Haikuchukua hata dakika mbili..simu ya Regina ikavibrate huku ikitoa 'tone' kuashiria kuwa ni message.. Ila Hisham alishangaa kwani haikua ni e-mail kama alivyotegemea, bali ni message ya kawaida.. Akatafakari kwa muda ila akaamua kuisoma..
Najua safari hii nakufa, sina jinsi, bali napenda nikwambie kuwa tunakufa pamoja, ulinitambulisha kwa Jessica, aliniambukiza HIV na mimi sikuona sababu ya wewe kukuacha ingawa najua nitakua nimemuua mumeo ambaye hana hatia, lakini haya yote umeyasababisha wewe..Mi natangulia lakini najua unakuja nyuma yangu Ndivyo ilivyosomeka sms ile, Hisham alifikicha macho akiwa haamini anachokisoma.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Let's call it a day..!!
Wait for Episode O16..
Whatsapp↘
+255718274130