Mdogo wetu kaacha ualimu kisa amepata mshangazi

Zee la madawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,886
Reaction score
4,459
Dada habari, sisi kwenye familia yetu tume pata changamoto kubwa sana kiasi kwamba mama naona kabisa tuna enda kumpoteza Kwa Presha.

Iko hivi, tuna mdogo wetu wa kiume ana miaka 25, aliajiriwa mwaka juzi Ualimu wa Sekondari, na alikuwa akilipwa mshahara mzuri tu bila shida yoyote.

Kitu Cha kushangaza mwezi wa tatu mwaka huu tulisikia kuwa haonekani shuleni kwao toka shule zilivyo funguliwa, mama alimpigia simu akamwuliza kulikoni? Akasema yeye kaamua kuacha kazi anafanya Biashara zake na alisha malizana na halimashauri, mama akasema sawa kama ni hivyo.

Sasa mwezi ulio pita si ndo tukapata ukweli kutoka Kwa marafiki zake kuwa aliacha kazi kisa Kapa mmama wa huko Arusha ana pesa na ndo Wana ishi naye, na mdogo wetu unaambiwa hana kazi yoyote zaidi ya kuishi tu na huyo mama.

Sasa mama baada ya kusikia hivyo alipata Presha akadondoka chini, alikimbizwa hospital lakini mpaka Sasa Hali yake Imeshindikana kurudi kuwa sawa kuongea vizuri hawezi na Mkono mmoja hauna nguvu kama mwanzo.

Na Kila tukimfuata mdogo wetu arudi Nyumbani hataki na kasema tumuache na maisha yake yeye ndo kashaamua hivyo.

Kwakweli sisi hatuna shida naye ila mama muda wote anatoa machozi tu ishara ya kumlilia mwanae mana ndo mtoto wake wa mwisho na alimpenda sana, tuna tamani mdogo wetu arudi Ili mama tu akae sawa ila ndugu yetu naye hajali hata tukimuelezea hali ya mama.

Tulikuwa tuna omba kama serikali inao uwezo wa Kuingilia hili jambo itusaidie kwakweli.
 
Nyie sasa fanyeni kazi ya kumuhakikishia mama , kuwa dogo hana shida, ameoa mwanamke mzuri., n.k
Fanyeni ili kumuondolea hofu mama.
 
Kwanza hii ni chai.

Lakini Wazazi waache kuweka expectations kubwa kwa watoto wao.

Akili ya kiumbe binadamu hubadilika anytime.

Kila mtu ana namna yake anavyo amua kuishi.
 
Dada habari, sisi kwenye familia yetu tume pata changamoto kubwa sana kiasi kwamba mama naona kabisa tuna enda kumpoteza Kwa Presha.

Iko hivi, tuna mdogo wetu wa kiume ana miaka 25, aliajiriwa mwaka juzi Ualimu wa Sekondari, na alikuwa akilipwa mshahara mzuri tu bila shida yoyote.

Kitu Cha kushangaza mwezi wa tatu mwaka huu tulisikia kuwa haonekani shuleni kwao toka shule zilivyo funguliwa, mama alimpigia simu akamwuliza kulikoni? Akasema yeye kaamua kuacha kazi anafanya Biashara zake na alisha malizana na halimashauri, mama akasema sawa kama ni hivyo.

Sasa mwezi ulio pita si ndo tukapata ukweli kutoka Kwa marafiki zake kuwa aliacha kazi kisa Kapa mmama wa huko Arusha ana pesa na ndo Wana ishi naye, na mdogo wetu unaambiwa hana kazi yoyote zaidi ya kuishi tu na huyo mama.

Sasa mama baada ya kusikia hivyo alipata Presha akadondoka chini, alikimbizwa hospital lakini mpaka Sasa Hali yake Imeshindikana kurudi kuwa sawa kuongea vizuri hawezi na Mkono mmoja hauna nguvu kama mwanzo.

Na Kila tukimfuata mdogo wetu arudi Nyumbani hataki na kasema tumuache na maisha yake yeye ndo kashaamua hivyo.

Kwakweli sisi hatuna shida naye ila mama muda wote anatoa machozi tu ishara ya kumlilia mwanae mana ndo mtoto wake wa mwisho na alimpenda sana, tuna tamani mdogo wetu arudi Ili mama tu akae sawa ila ndugu yetu naye hajali hata tukimuelezea hali ya mama.

Tulikuwa tuna omba kama serikali inao uwezo wa Kuingilia hili jambo itusaidie kwakweli.
limshangazi limesha mfunga mtoni ,kulalanina ,hawa maveterani wananapambania mampenzi ya vijana hasa akimtest akakuta anapeleka moto kama chuma ya mjerumani.
 
Mnajipa PRESHA ZA BURE kufatilia maisha ya mtu mzima.

Endeleeni na Mitikasi yenu.

Si Bora mmesikia Yuko Kwa mwanamke.

Angekuwa Kwa mwanaume je si ukoo mzima mngekufa Kwa presha.

Achanani nae nyie fanyeni maisha yenu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom