Mkuu Shark, sio upendeleo, but ni "getting connected!".
Sifa kubwa ya mwandishi mzuri wa habari, anatakuwa kuwa na "nose for news", yaani pua ya kunusia habari!, baada ya kufanya kazi newsroom, hiyo pua zaidi ya kunusa habari, pia una nusa harufu ya "ankara!", hivyo mwanzo unaanza na habari na "ankara", baadae unaachana na kunusa habari, utanusa zile tuu habari zenye "ankara!", ndia maana zikifanyika semina, warsha, makongamano na mikutano, waandishi kibao kwa sababu ya "ankara!" kwenye tule tuji little brown envelopes!", ukifanikiwa kunusa "ankara" pekee, hii sasa ndio inaitwa "opportunities!", unachangamkia tenda na sio unapewa au kuletwa kwenye kisahani cha chai!, na kuna watu wanaodhani ni rahisi!, kukamata tuu microphone na kupiga blah blah!, au kukamata tuu kalamu na kuandika!, no way, ili pesa zije, lazima ufanye kazi haswa, and you have to be good!, Pinto is good kuchangamkia michongo!.
Na wengi huanzia kwenye to work hard to make money!, ukiisha zitengeneza za kutosha, you don't have to work all that hard kuziongeza ili ziziishe, but now you have to use money to work for you!, ndio ukifika mahali, unakimbiliwa kuhudumiwa, huongei wewe, pesa itaongea!, ndipo jamaa kashangaa yuko kwenye foleni, watu wanakimbizana kukimbilia mabegi, kuyapitisha off the screen!.
Ukiwa na pesa, unanyenyekewa, unageuka mfalme!.
Pasco.