Pasco wa JF,hiyo post uliyoitoa kumsafisha pinto imekuvunjia heshima humu JF ya kutetea wauza unga,kama pinto na michuzi wametoka kwa kulamba miguu ya la profeseli na wewe unafuata njia hiyo hiyo ya kulamba miguu ya wauza unga na mafisadi wa nchi hii,acha hiyo tabia mara moja,hapa napata picha hata deal za kampuni yako ya utangazaji inayopata project za 77 na 88 na halfa za ppf/nssf/tpdc kwamba umetumia njia hiyo hiyo ya kuwalamba miguu,nyie ndio waandisha makanjanja mnaodidimiza tansia ya uandishi kwa kuwafanya wale wanaoandika ukweli na wasionunulika kupata shuruba kama kina kibanda na kubenea!
Mkuu King Kong, kwanza asante kwa hii, hili la kuambiwa nimejivunjia heshima, kila siku linaibuka humu, siku zote jibu langu huwa ni moja tuu, ili hiyo heshima nitakayo jivunjia, ivunjike, kwanza ni hiyo heshima yenyewe lazima iwepo ndipo ivunjwe!, kwa bahati mbaya sana, Pasco wa jf, hata hiyo heshima yenyewe hana!, haipo, hivyo hakuna heshima iliyovunjika kwa sababu hata hiyo heshima ya kuvunjwa haipo!.
Sitetei mtu, ila huu ndio ukweli halisi, Tanzania ya sasa, pesa ndio kila kitu!, na haijalishi umezipataje, wala unafanya nini to make them, as longo as una pesa, utapata kila utakacho, na ukipata, the end justify kila kitu!.
Mimi wa Pasco wa JF nilikuwa mwandishi tangu enzi za rais Mwinyi, tukiwa Tambaza, japo sio darasa moja, sisi tukiwa O Level, mtoto wa Mwinyi na mtoto na mtoto wa Malecela na tulijua pale Tambaza, kama ni lobbying si ninge lobby?!.
Kwenye Tambaza hiyo hiyo tena darasa moja!, same class, tumesoma na mtoto wa Ben!, Ben anaingia madarakani tunamuona hivi na huku mtoto wake ni rafiki!. Kwa nini nisilobby?!. Kwa Ben mimi nimepelekwa hadi kwa baba na mama na kuwa formerly introduced kuwa huyu "tumesoma nae!", nyie Ben mnamuita rais, sisi tunamuita "baba so and so!", kama ni ku lobby, si ningelobby!.
Nimeacha journalism nikaenda UDSM, kitivo cha sheria, pale nimekutana na mtoto wa Jakaya he is like a friend!, kama ni ku lobby hapo si ndio pangekuwa penyewe?!. Na kama hujui, baada ya kumaliza UD nilipata kazi ya maana sana FCO, nikiwa ndie mshauri wa siasa wa Balozi wa UK hapa nchini, a well paying job!, niliacha mwenyewe kwa ridhaa yangu, huku nikibembelezwa!, just to pursue my "idea" ya PPR!.
Zile project za 77 na 88 na hafla za ppf/nssf/tpdc etc, zote zinatangazwa kwenye GPN watu wanaomba, tena kwa hili ningepaswa kupongezwa ni mimi ndio nilianza kutangaza kama mtangazaji "private!", sasa unaniona nikipungua wamekuja vijana kina Kibonde, Jerry Murro, na watangazaji kibao sasa ni private, hivyo soon nitatoweka na kuibukia mahakama kama advocate wa High Court, nakuhakikishia hakuna lobbying yoyote wala halam,biwi mguu mtu yoyote!.
Hata utetezi wangu kwa EL, right hand man wake anaitwa Abou ni dam dam na mimi, lakini amini usiamini, sijawahi hata kusalimiana nae hata shikamoo tuu, tangu ameanza harakati za kuitafuta ikulu, japo kila kukicha natia timu ofisini kwake kumuona Abou!.
Ni kwa kuto lobby huku kumenipelekea mimi kubaki masikini, ila amini usiamini, kuna masikini jeuri, wako radhi kulala njaa, huku jirani next door akimwaga chakula!. Bora kufa njaa kuliko kuwa omba omba!. Mimi ni masikini jeuri wa type hiyo, na enjoy umasikini wangu lakini halali, kuliko ku lobby popote!.
Wapo matajiri wenye utajiri mkubwa wa mali, lakini ni masikini wa roho, wana mali lakini hawana furaha, na wengi huonyesha furaha machoni, lakini mioyoni ni huzuni kutokana na walichofanya kupata huo utajiri, lakini tuna masikini wengi, wenye umasikini wa mali, lakini ni matajiri wa roho, wenye furaha ya kweli moyo na maishani, licha ya kuishi kwenye lindi la umasikini uliotopea!.
Pasco.