Hii ni kitu gani wakuu?

Hii ni kitu gani wakuu?

Amon Lisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2018
Posts
464
Reaction score
1,170
Habari wana jamvi,

Takribani wiki mbili zilizopita nilikuwa nasumbuliwa na muwasho sehemu za siri; dhakari, maliwato na sehemu katikati ya mapaja na mbupu. Sikuota vipele isipokuwa tu sehemu ya kichwa cha dhakari ndio nilikuwa na vipele viwili tu ambavyo haviwashi wala kutoa uchafu. Nikajaribu kuongeza usafi sana na kupaka vitunguu swaumu vya kusaga kwenye hivyo vipele, kimoja kikapotea kimebaki hicho kwa picha. Kimeongezeka ukubwa kidogo hali inayonipa wasiwasi tatizo litakuwa ni gani.

Nilijua ni fungus, baada ya kupaka mafuta ya nazi maeneo ya maliwato sina tena muwasho ila kwenye mapaja na wakati mwingine dhakari inawasha.

Wataalamu shida itakuwa nini? Na tiba au suluhisho lake ni lipi?

Hospital sijaenda sina bima wala pesa za vipimo, life langu ni zaidi ya tia
 
Mtoa maada kasema uchumi mbovu hana Senti ya kwenda hospital watu wamekomalia nenda hospital 💔
Ila humu🙌
Uchumi mbovu kwani hapo inagharimu shilingi ngapi? Kumuelezea daktari hali ilivyo na kufanya vipimo? Humu unadhani atapata maelezo gani mkuu? Hata hayo atakayoyapata bado yatahitaji atumie fedha kupata dawa sio kwamba atapona kwa maelezo matupu
 
Habari wana jamvi,

Takribani wiki mbili zilizopita nilikuwa nasumbuliwa na muwasho sehemu za siri; dhakari, maliwato na sehemu katikati ya mapaja na mbupu. Sikuota vipele isipokuwa tu sehemu ya kichwa cha dhakari ndio nilikuwa na vipele viwili tu ambavyo haviwashi wala kutoa uchafu. Nikajaribu kuongeza usafi sana na kupaka vitunguu swaumu vya kusaga kwenye hivyo vipele, kimoja kikapotea kimebaki hicho kwa picha. Kimeongezeka ukubwa kidogo hali inayonipa wasiwasi tatizo litakuwa ni gani.

Nilijua ni fungus, baada ya kupaka mafuta ya nazi maeneo ya maliwato sina tena muwasho ila kwenye mapaja na wakati mwingine dhakari inawasha.

Wataalamu shida itakuwa nini? Na tiba au suluhisho lake ni lipi?

Hospital sijaenda sina bima wala pesa za vipimo, life langu ni zaidi ya tia
pole sana gentleman,

miongoni mwa dalili muhimu sana ya kaswende kamili, ni kuota kipele kimoja tu au zaidi kisichouma kwenye kichwa cha mshedede wako.
kumbuka, ni kwenye kichwa cha mshedede.

lakini pia,
dalili muhimu kamili ya gono ni pamoja na kutoa usaha mzito wenye harufu mbaya kupitia njia ya mkojo.

Zaidi sana,
miongoni mwa dalili dalili kamili za U.T.I sugu ni pamoja na kujiskia kama moto hivi kwenye njia ya mkojo kabla au baada ya kumaliza haja ndogo.

hata hivyo,
kwa msaada wa kitabibu wa uhakika kwa changamoto yako, tafadhali, ondoa aibu, vaa ujasiri, wahi hospitalini ukamuone daktari.

Tatizo lako linatibika na kupona kabisa, usichelewe tafadhali.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom