Hii ndiyo maana halisi ya mwanaume ni kichwa cha familia

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
HII NDIO MAANA HALISI YA MWANAUME NI KICHWA CHA FAMILIA

Anaandika, Robert Heriel

Ukiwa kama kijana unayetarajia kuwa Baba, au ambaye tayari ni Baba na upo kwenye Familia yako. Shika Kwanza hizi nyundo;
i. Kuna mambo unapaswa kuwa nayo lakini Mkeo asijue unayo.
ii. Kuna mambo unapaswa kuwa nayo na Mkeo ajue unayo.
Iii. Kuna mambo unapaswa kuyaonyesha dhahiri Mkeo akijua umeyaonyesha.
iv. Kuna mambo unapaswa kuyaonyesha Kwa kificho lakini Mkeo asijue wewe ndiye Injinia, uliyeyafanya.

Ili hayo yote yafanyike na uyafanye Kwa ufanisi itakupasa uwe na;
1. Akili ya kutosha.
2. Machale,
uwezo wa kukisia na kutabiri matukio yatakayofuata au hatua za wanafamilia watakazochukua
3. Mbinu na mikakati.
4. Timing.
Kujua Wakati sahihi wa kufanya Jambo.

Bila kuwapotezea muda. Tuangalie mambo AMBAYO BABA unapaswa kuwa nayo kichwa cha Familia;

1. UBONGO UNAOFANYA KAZI VIZURI.
Mwanaume kama kichwa cha familia lazima uwe na ubongo unaofanya kazi vizuri. Ndani ya ubongo kuna Akili, utambuzi, ufahamu, kumbukumbu, ubunifu n.k.
Bila ubongo huwezi itwa Mwanaume. Kazi ya ubongo ni kuongoza na Kuratibu shughuli zote za mwili.

Huwezi iongoza familia kama ubongo wako haufanyi kazi vizuri.
Na hakuna Mwanamke atakayekubali kuongozwa na Mwanaume asiye na ubongo.

2. Maono..... Macho yanayoona.
Kichwa kina macho, kazi ya macho ni kuona. Baba lazima uwe na macho yanayoona. Macho ya kimwili na macho ya kwenye Nafsi AMBAYO ndio huitwa Macho ya Akilini"Maono"
Ni lazima macho ya ubongoni yafanye kazi mara mbili zaidi ya macho ya mwilini.

Mtu anaweza akawa anaona Kwa macho ya mwilini lakini ubongoni ni Kipofu, haoni.
Huwezi ukaongoza familia kama wewe ni Kipofu, huoni.
i. Huoni mbele mambo yatakuwaje, yaani huoni Kesho yako au siku zako zijazo.
Ndio maana unaweza Fanya kitu bila kujua matokeo yake. Huo unaitwa upofu wa ubongoni.
Mfano, Umepata msichana ukamuoa, anaonyesha vitabia vya ajabu, lakini Kwa vile wewe ni Kipofu huoni siku za Mbele nini kitatokea, unaamua kujipa moyo. Yakija kukutokea unapiga mayowe.

ii. Huoni Nyuma mambo yalikuwaje.
iii. Huoni mambo ya sasa.
Yaani wewe ni Kipofu.

Baba unatakiwa uwe na maono. Uyaone Maisha yako ya siku zijazo yatakuwaje.
Na hiyo itakufanya uwe na
a) Malengo, mipango na mikakati.
b) Sheria, Kanuni na miiko.
c) Misimamo kama Mwanaume.
Mwanaume asiyekuwa na maono huwa kigeugeu, hajui kipi asimamie, Hii ni Kwa sababu ya kuwa Kipofu.

Lazima uone, wanaokuzunguka, yanayotokea, kisha ubongo wako uyafanyie interpretation, evaluation and analyzing.

3. Usikivu. Masikio yenye Kusikia.
Kama utachunguza utagundua macho yapo usawa na masikio, Katika ubavu wa kichwa kushoto na kulia.
Muundo huo wa viungo vya kichwa upo katika mpangilio Kwa Makusudi na wala sio Kwa bahati Mbaya. Hili ni somo la siku nyingine linahusu zaidi Anatomy and Physiology.
Mwanaume lazima uwe na masikio ya kusikia upande huu na upande huu, sio usikilize vitu vya upande mmoja. Sikiliza wa kushoto kisha Wakulia, alafu Pima then utapata majibu na maamuzi sahihi.
Mwanaume mwenye Akili ni Yule anayepima mambo na kusikiliza Pande mbili, kushoto na kulia ndipo atoe maamuzi.
Ili nyumba yako uijenge, isiharibike usiendekeze kupendelea upande mmoja.
Kwa waliosoma Biology kwenye Mechanism of Hearing watakubaliana na Mimi kuwa moja ya Kazi ya masikio ni kuleta Balance of Body,
Mwanaume sio kila uambiwacho na Mkeo ni sahihi na unapaswa kufanya, au sio kila uambiwacho na Mzazi wako ni sahihi.
Pima, balance the Story.

4. Kunusa na kuvuta nishati ya uhai. PUA.
Baba ndiye unapaswa kuwa chanzo cha nishati ya uhai hapo nyumbani. Kuvuta pumzi ya uhai kama ilivyo kazi ya Pua.
Kwa kuhakikisha Mahitaji yote ya nyumbani yanapatikana.
Pia unapaswa kunusa hatari au fursa ambazo macho hayakuziona, masikio hayakuzisikia. Hiyo ndio kazi ya Baba.
Hukuona ndio, je hata kusikia hukusikia?
Hukusikia wala kuona, hata kunusa hukunusa hiyo hatari au fursa au baraka au mkosi.
Kwamba ubongo wako haufanyi kazi ndio maana hukushtukia, au ulipuuza?

Pua Ipo chini ya Ubongo, macho na masikio.

5. Kuonja na Kutamka..... ULIMI.
Baba lazima uwe na kauli thabiti, kile unachokisema ndio ukisimamie. Sio leo unaongea hivi Kesho unasema vile. Familia haijengwi hivyo. Kazi ya ULIMI ni pamoja na kuwezesha MTU kuzungumza.
Baba ndiye unatakiwa Watu wakusikilize wewe ndani ya nyumba.
Wewe ndio uwe chanzo cha taarifa muhimu na nyeti ndani ya familia.
Mkeo na watoto waamini taarifa zote utakazozitoa.

Baba unapaswa uwe na kauli kama sehemu ya ulimi,
a) Tamu
b) chungu
c) Chachu
Kauli zako zinatakiwa ziwe tamu kuwapa Raha na furaha Mkeo na watoto wako.
Kuwapa moyo, tumaini na faraja Mkeo na watoto. Kuwabembeza, na kuwahakikishia wapo salama.

Kauli zako ziwe chungu na chachu kama dawa kudhibiti na kufukuza maadui qa familia, kufukuza Tabia Mbaya zitakazofanya na wanafamilia ikiwemo Mkeo na watoto. Kukomesha upuuzi na ujinga ndani ya familia.
Kauli chungu na chachu bila kusita kukemea Tabia Mbaya.

Lazima uonje na kuzijaribu kauli zako Kabla hujazitamka, kauli hizo lazima ziwiane na mambo yanayotokea ndani ya familia...

Kichwa kimebeba;
1. Ubongo
2. Macho
3. Masikio
4. Pua
5. Ulimi.
6. Ngozi.
Baba unapoitwa Kichwa cha familia inamaanisha u-take Role za hivyo viungo Kwa ufanisi mkubwa.
Sio uzubae zubae.
Baba mzima unataka ubembelezwe kama demu,
Unataka wengine ndio wakufanyie kila kitu. Huo sio uanaume.

Acha nipumzike SASA.

Nawatakia maandalizi Mema ya SABATO.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hakika umeshusha madini mazuri Sana mkuu Robert,,, nina imani kwamba kijana yeyote wa kiume atayebahatika kuusoma Uzi huu bila Shaka atapata maarifa ya jinsi ya kuisimamia nyumba( ndoa) Yake Kama mwanaume.

Hongera Sana mkuu.
 
🙏🏾🙏🏾🙏🏾
Barikiwa Sana Mkuu
 
Sawa.....ila huwa viko viwili vinasaidiana.
 
Back
Top Bottom