VERBOSE
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 8,145
- 12,743
Wakuu wa Jukwaa, leo na mimi nina swali ambalo linakua linanitatiza sana kichwani kwangu kwa muda kidogo sasa.
Nimekua napitia hali ya kujiuliza maswali mengi sana juu ya kiumbe hiki kinachoitwa BUNDI. Bundi ni ndege mwenye sifa kede wa kede. Sitaki kuzungumzia sifa za ndege huyu, leo nimeona niwaulize km mimi ninavyojiuliza imewezekanaje ndege huyu kuishi tunapoishi kwa zaidi ya Mwezi?
Yaan anakuja kila usiku unapoingia kuanzia majira ya saa 4 - 6 mpaka 7 usiku BUNDI anakua kashafika tayari kwenye mazingira yake na anakaa palepale anapokaa siku zote kwenye mti ule ule anaosimamaga siku zote na anatazama uelekeo ule ule anaotazama siku zote (anatazama mlangoni watu wanapotokea na kuingia) yaan ukifungua mlango kwa ajili ya kutoka nje unakutana na BUNDI yupo juu ya mti anakutazama na anakukazia macho haswa, na haondoki hapo mpaka kunaenda kupambazuka saa 11 kuelekea 12 asubuhi ndio BUNDI anaondoka ni km amekuja kulinda nyumba au sielewi, ukimpita anageuza shingo, hapo kabla sikua najua nilikua nasikia tu na kujionea kwenye video za kule Utube km BUNDI anao uwezo wa kugeuza shingo yake kwa jinsi anavyotaka, hii nimejionea mubashara yaani nimejionea bure kabisa bila kwenda kwenye Mbuga au Hifadhi fulani na kulipa kiingilio ili nione.
Sasa basi leo naomba tujiulize kwa pamoja au km yupo mwenye kufahamu atufahamishe inawezekanaje BUNDI kukaa sehemu moja kila unapoingia usiku kwa zaidi ya Mwezi? Na anapofika BUNDI watu waliopo ndani ya nyumba hata waliopo nyumba za jirani usiku wanaweweseka sana, utasikia mtu anaweweseka huko unajua tu tayari BUNDI yupo nje hapo kashaweka kambi, na ukisikia mtu kaweweseka ukitoka tu nje ile kufungua geti tu unamuona bundi yule pale kwenye mti anakutazama, hii ina maana gani wakuu? BUNDI kuweka kambi kila usiku anatutazama nje wakati sisi tumelala ndani, hii inamaanisha nini?