15. NGUVU ZA TIBA KUONDOLEWA
Baada ya siku thelathini na kitu hivi nilipata ugeni wa yule binti kutoka Kiwalani, ambaye kwa jina anaitwa Behat. Lakini mimi nilianza kumuita Bahati maana niliona ni bahati sana kukutana naye, na yeye alipata bahati sana kufika kwangu akiwa na mama yake baada ya mihangaiko mingi ya kitiba.
“Karibu Bahati…” nilisema huku nikimuonesha sehemu ya kukaa kusubiri maana nilikuwa nachukuwa maelezo ya mteja mwingine. Baada ya kuwahudumia wateja wote na kuondoka, tulibaki mimi na wasaidizi wangu na Bahati ambaye hakuja kama mgonjwa kwa siku ya leo ingawaje yeye alijuwa amekuja kwa kuangaliwa anaendeleaje.
“…Mama hajambo? Anaendeleaje na miguu yake?” niliuliza maana mama yake alipataga shida ya miguu kwenye magoti na alitibiwa kwa tiba za kimagharibi (western medicine)
“Anaendelea vizuri, anakusalimia…” alijibu Bahati.
Behat alikuwa ni mtoto wa mwisho kwa baba na kwa mama na ndio kwanza alikuwa amemaliza kidato cha nne miezi michache iliyopita. Nilianza kumchambua na kumvua nguo kwa macho na kuona uzuri uliojificha katika nguo alizovaa za kujihifadhi vyema.
Nilimuambia kuwa atabaki kwa siku tatu kisha arudi kwao halafu arudi tena baada ya miezi miwili. Basi nikamwacha achanganyike na wale wasaidizi wangu nami nikawa na shughuli zangu zingine.
Usiku kama saa tatu baada ya chakula, nikamwelekeza kile chumba ambacho ndicho alichoogeshewa ile siku ya kwanza, alipoingia nikamfuata na kumwambia…
“Jisikie upo nyumbani, ukichoka utajipumzisha…” nilimwambia.
Baadaya kama dakika arobaini hivi wakati nimehakikisha wasaidizi wangu wameingia kupumzika nilienda chumba alicholala Behat ambacho kilikuwa mkabala na master bedroom yangu mbali kabisa na upande wa vyumba vya wale wasaidizi wangu.
“Ngo ngo ngo….” Kwa ubisho wa sauti ya chini niligonga mlango na kujaribu kuufungua kumbe ulikuwa wazi…
Behat alikuwa bado anajisomea kitabu alichokuja nacho…
“Kumbe bado upo macho…?” niliuliza.
“Eee bado namalizia sehemu hii ndio nilale…” alijibu.
Nikasogea na kukaa pembeni ya kitanda maana chumba kile hakukuwa na kiti.
“Samahani, ujio wangu ni tofauti leo, sikuja kwa ajili ya tiba, bali kwa ajili ya mazungumzo mimi na wewe.
Behat alibaki ananiangalia tu, sijui alikuwa anawaza nini…
“Behat..!” aliitika “Abee”
“Nakupenda sana, nilikupenda tangia macho yako yalivyo gongana na macho yangu siku ya kwanza…”
Pakawa na ukimya….
Kiumri Behat nilimzidi miaka isiyozidi sita, hivyo tulikuwa tunaendana na yeye alikuwa ameshapevuka. Niliendelea kumpa maneno matamu pale na kumuahidi kuwa nataka nimuoe. Alishangaa maana alidhani mmoja wa wale wasaidizi wangu ni mke wangu.
“Kumbe bao hujaona..!” alisema huku bado akiwa ameshika kitabu chake, akiwa ameegemea ukuta juu ya kitanda.
“Ndiyo sijao lakini tayari mimeshapata mchumba ambae ni wewe” nilijibu na pakawa na ukimya.
Baada ya machombezo ya muda mrefu hatimaye tukajikuta sote tupo kama tulivyo zaliwa…
“Mie sijawahi kufanya…” alisema Behat wakati nikiendelea kumtomasa kwa minajiri ya kumuandaa akionesha ushirkiano usio na ujuzi.
Usiku huo nikajikuta nimefanya ngono baada ya muda mrefu, ngono ambayo hata sikufaidi maana Behat alikuwa ni mgeni na kwa kuwa nilikuwa na hamu ya muda mrefu nilijikuta sijafungua njia sawasawa.
Siku ya pili nikashangaa hapakuwa na wateja kabisa pale nyumbani. Nikatumia muda mwingi kuongea na Behat mtoto wa Kidigo. Na usiku wake tukarudia tena mchezo wetu na safari hii nilifungua njia vizuri na kurudia mara moja.
Tukaoga na nikamwacha alale nami nikarudi chumbani kwangu.
Saa sita za usiku chumba changu kikajaa mwanga mkali na sauti yenye mitetemo ikasikika…
“Umefanya nini sasa mwanangu!...”
“Umeharibu kila kitu…”
“Hukupaswa kulala na huyo binti…”
Nikapigwa na butwaa huku nikisikiliza…
“Huyo binti ni nusu jinni kama wewe, lakini yeye amezaliwa na jinni mwanamke, huyo aliyemleta kuja kutibiwa siyo mama yake, mama yake mzazi alifariki binti akiwa mdogo, Mama Behat alibadilishiwa mtoto akiwa hospitalini Ilala, mtoto wake halisi aliugua ghafla na kufariki lakini kabla manesi hawajatambua ndipo aliwekewa Behat na jopo la Majini waliotumwa kwa kazi hiyo…”
“Umeharibu kila kitu…”
“Tulikuandalia mke mzuri ambaye ni jinni kamili uli uzao wenu uweze kuishi huku moja kwa moja, lakini kwa kuwa umetembea na nusu jinni mwenzako umefunga milango yote ya ninyi kurudi ujinini!...”
Sauti ile iliendelea kutoa risala pale kwa masikitiko sana na mwisho akasema…
“Kuanzia sasa wewe si mwanangu tena na nguvu zako zote zimetoka tangia ulipoweka mbegu zako za uzazi ndani ya mfuko tumbo wa huyo Maif bint Shariff wa Kaskanini….”
Mwanga ulipotea na sauti sikuisikia tena, nikapitiwa na usingizi mzito hadi niliposhtuka ilikuwa saa moja kasorobo asubuhi.
Nikaenda kwenye chumba cha matibabu nikakuta hakuna chochote, nikajiangalia mikononi sikuona hata pete moja, nikatafuta ile fimbo bila mafanikio, nikatafuta unyoya na usinga wala sikuviona. Moja kwa moja nikajuwa hapa nguvu zangu za utabibu zimeisha.
***********
Nikaitisha kikao cha dharura na kuwapatia ujira wao wale wasaidizi wangu na kuwapa likizo hadi nitakapowatafuta tena, maana majumbani kwa ndugu zao napajuwa.
Nikaenda chumbani kwa Behati na kukuta ameshaamka na kuniambia aliona mwanga mkali sana usiku lakini ukapotea.
“Bahati…” nilimwita kama ninavyomwitaga, akaitika
“Mimi na wewe asili yetu ni moja…”
“Wewe ni wa Kaskazini na mimi ni wa Magharibi…” nikasema
Nikamshika mkono wake na kuanza kumchunguza, ndipo nikaona pattern ya ngozi yake ipo kama yangu na si kama ya binadamu wengine.
“Inabidi tuoane haraka” nilisema.
*********
Baada ya kumuelezea kwa kirefu ndio akaelewa na yeye akaanza kufunguka kuhusu maono yake. Basi moja kwa moja nikaamua arudi kwao kwanza kisha mimi nifanye utaratibu kwa kufikisha posa kwao.
Nikaenda Bagamoyo na kufanya kikao na wazazi wetu kisha nikafanya kikao na mama, kilikuwa kikao kirefu sana maana ilibidi nifunguke kuhusu mwanzo wa ujauzito wangu na kwamba mzee Mwinyi hakuwa baba yangu wa kunizaa bali nilikuwa mtoto wa Shariff kutoka Magharibi na nikaelezea kisa chote mwanzo mwisho kitu kilicho wafanya Baba na mama kupigwa na butwaa,Mama akaanza kulia huku Baba akiwa amejiinamia.
“Kama nguvu ndio zilikuwa za hivyo mwanangu, basi nadhiri yangu bado sijaitimiza, mimi nilitaka umtumikie Mwenyezi Mungu na wala siyo kumtumikia ama kuwatumikia majini…” ilikuwa kauli ya mama yangu wakati akilia
“Kwa hakika mama, mimi sikujuwa, nilidhani ndio namtumikia Mwenyezi Mungu…” tuliendelea kulia sote pale lakini mwisho wa siku tukatulia na vikao vya ‘kujenga’ vikaanza.
*********
Tarabibu za posa zikakamilika, na ndoa ikapangwa haraka haraka ndani ya miezi miwili tukafunga ndoa mimi na Behat ambaye ndiyo huyo niliye kutambulisha asubuhi na wale ndio watoto wetu.
Baada ya ndoa mimi na Behat tukafanya safari ya kwenda Utete Rufuji kwa mcha Mungu ambaye nilihadithiwa habari zake siku za nyuma.
**********
Itaendelea…