Hatimaye nipo huru

Hatimaye nipo huru

Kama ulibahatika kumfahamu Mzee Njemba na Shariff Badawi, wewe ni mmoja wa wenye bahati. Bila shaka uliitumia vyema.
Acha niweke wazi mzee, we ni moja Kati ya watu wanao ni hamasisha Sana.
👉Kuanzia uandishi wako ulio Bora, mpaka unavyo ishi na watu humu jumwaani. Hujawahi ivunja heshima yako🙏🙏🙏
 
Kuna watu humu duniani wamebarikiwa vipawa mbalimbali wakiwemo Mzee Njemba (R. I. P) na Shariff Badawi (R. I. P)

Sijui kama waliacha warithi wenye kuendeleza mazuri yao.
Hakuna 😁wana rasharasha tu sio mvua yenyewe
 
Kuna shuhuda mmoja humu JF anarudia kuandika simulizi yake akimhusisha Juma Njemba.


 
Uandishi uliotulia. Story iliyotulia. Najua umestaafu vizuri, vinginevyo unastahili kunufaika na huu uandishi na hizi simulizi zako.
 
jamaaa anaitisha,yaani maeneo yote hayo aliyo taja ,ya kuanzia kigoma hadi kabwe,nayafahamu sana,hasa hapo lyazumbi ndio kuna njia panda ya kwenda kabwe,kuna kuku,samaki na nyama ya mbuzi ya kufa mtu!!!na hicho kisiwa cha TUMBATU,kipo zanzibar unavuka na fibre kutoka MPEKETONI,kwa buku 2, unakutana na kisiwa kinaitwa JONGOWE!!ni hatari sana,kwa uchawi.
MKOKOTONI na sio mpeketoni
 
Mkuu kwanza hongera kwa simuliz nzur yenye uhalisia na maisha tunayoishi na ahsant kwa kutuelimisha na kwa wakat huo huo kutuburudisha.

Mafundisho ya dini yanatuelekeza tukiwa tunafanya tendo la ndoa tusisahau kuomba dua (kutaka ulinzi kwa allah) kutokan na shetani alie laa'niwa. Kwa sababu anakua yupo karb na wanandoa wakt wa jimai ili kutanguliza mbegu zake. Sasa hapa nahisi ndicho kilichowakuta wazazi wa panzi wakapata mtoto wa jini bila ya wao kutanabahi.

Tumepewa uwezo wa kuwatawala majini lkn kinyume na kua na taaluma ya kuwatawala wamekua wanatutawala sisi. Tunashauriwa tuwe twajilinda kwa allah kwa adh-kar (dua) mbali mbali ili wasiweze kututawala.

Wakati wa jimaai(tendo la ndoa) waweza soma hivi ww na mwenza wako( Allahumma jannibna shaitwana wajannibi shwaitana maa razaktana) tafsir (ewe mola tulinde na shetani na kilinde na shetani na kile utakachoturuzuku).

Allah aa'lam
Naomba kuwasilisha.
 
Mkuu kwanza hongera kwa simuliz nzur yenye uhalisia na maisha tunayoishi na ahsant kwa kutuelimisha na kwa wakat huo huo kutuburudisha.

Mafundisho ya dini yanatuelekeza tukiwa tunafanya tendo la ndoa tusisahau kuomba dua (kutaka ulinzi kwa allah) kutokan na shetani alie laa'niwa. Kwa sababu anakua yupo karb na wanandoa wakt wa jimai ili kutanguliza mbegu zake. Sasa hapa nahisi ndicho kilichowakuta wazazi wa panzi wakapata mtoto wa jini bila ya wao kutanabahi.

Tumepewa uwezo wa kuwatawala majini lkn kinyume na kua na taaluma ya kuwatawala wamekua wanatutawala sisi. Tunashauriwa tuwe twajilinda kwa allah kwa adh-kar (dua) mbali mbali ili wasiweze kututawala.

Wakati wa jimaai(tendo la ndoa) waweza soma hivi ww na mwenza wako( Allahumma jannibna shaitwana wajannibi shwaitana maa razaktana) tafsir (ewe mola tulinde na shetani na kilinde na shetani na kile utakachoturuzuku).

Allah aa'lam
Naomba kuwasilisha.
Swadakta mkuu.

Shukrani kwa pongezi. Nawe zikurudie kwa kumakinika nayo.
 
5. MAPENZI, WIVU, FITNA NA KUSAKA SULUHU

Kusema ukweli baada ya yale matibabu ya siku saba kutoka Mlingotini nilianza kujisikia vizuri, maruweruwe yaliisha, sikuwa na gumbizi wala kuhisi kuchanganyikiwa au kuota ndoto za ajabu ajabu.

Hali yangu iliendelea kuimarika na kuendelea na majukumu ya kusaidia baba hadi siku ile ulivyonikuta feri.
“Yaani pale nilikuwa tayari nimeimarika…” alisema

Tukacheka sana maana nilivyomuona siku hiyo Feri alikuwa dhoofu sana sasa sijui kabla ya hapo alikuwa dhoofu kiasi gani. Nilimuonea huruma sana hadi hapo lakini aliendelea kunisimulia.

Familia ya Mwinyi Mkila ilikuwa na familia rafiki na familia yangu, hivyo nilizoeana sana na watoto wake hususani wa kiume maana walikuwa wanapenda sana kuja kwangu Sanzale kuchukuwa maembe dodo, maembe sindano na mbichitamu. Ni familia iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuwasilimisha mdogo wangu na mke wake ambao ndio walikuwa makazi yao hapo kwangu Sanzale kwa ajili ya kuendeleza ufugaji wa kisasa na kilimo mihogo, mbaazi, kunde, kutunza miembe, minazi na kuna kasehemu kidogo kuna bonde ambalo tulitumia kulimia mpunga.

Basi baba, niliendelea na majukumu yangu hadi nikaamua nibakie huku huku Dar es Salaam kwenye nyumba yetu tuliyopangisha maeneo ya Kariakoo mtaa wa Livingstone na Mkunguni. Nikapewa chumba kimoja na kuanza maisha hapo. Niseme tu ukweli hadi muda huo nilikuwa sijawajuwa wanawake, sijui kwa sababu ya maradhi kunipelekesha au namna gani. Lakini nilivyohamia tu hapo kwenye nyumba yetu ya Dar mambo yalianza kubadilika.

Nilihamia nikiwa na godoro tu na stuli moja na feni ya umeme ambayo niliinunua wakati nahamia rasmi hapo. Nyumba ilikuwa ya vyumba sita yaani ukiingia vyumba vitatu upande wa kulia na vyumba vitatu vingine upande wa kushoto. Mimi nikapewa chumba cha katikati upande wa kulia ambapo mpangaji aliyekuwa humo alihama baada ya kupata kazi nje ya Dar es Salaam hivyo nikachukuwa nafasi hiyo kuwasilisha ombi langu kwa baba na akanikubalia.

Nadhani alinikubalia kwa sababu ya kwanza nianze kujitegemea na kujifunza maisha, pili inakuwa rahisi mimi kufanya kazi ya kupokea matenga ya samaki na kuyauza kwa kuwa sasa utaratibu wa usafirishaji ulizidi kuwa bora baada ya kuamua kutumia Datsun pickup za baadhi ya wamiliki hapo Bagamoyo. Hivyo badala ya kuamka saa kumi alfajiri kama Bagamoyo nilikuwa naweza kulala hadi saa moja kasoro na kuwahi Feri kabla gari haijafika na kupokea mzigo na kuuweka sokoni kwa mauzo.

Nilianza kupewa ujira rasmi badala ya posho ya kujikimu pekee na nikaanza kununua vitu vya ndani kama vile kitanda, nikachongesha kochi la mtu mmoja, nikanunua friji dogo na redio kwa ajili ya kusikilizia taarifa za habari, vipindi vya michezo saa mbili karorobo usiku na kusikiliza matangazo ya moja kwa moja ya mipira. Hakika chumba changu kilipendeza kwani niliweka na kapeti la plastiki lenye nakshi za drafti draft.

Kazi za Feri zilikuwa zinaisha mapema sana kabla ya saa sita mchana, hivyo nilikuwa napata muda mwingi wa kupumzika na kuzurura jijini. Kuzurura huku kulinikutanisha na Sinasudi binti ambaye alitokea kunipenda sana. Tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi na akawa anakuja nyumani kunifulia nguo na kunipikia siku moja moja.

Kumbe nisijuwe mle mle ndani ya nyumba, kuna mtoto (mwari) wa mpangaji wetu alikuwa akinipigia mahesabu. Mara aje kuomba maji ya baridi, mara aje kunipigisha stori lakini mimi wala sikuwa na hili wala lile, nilimchukulia kama mdogo wangu tu. Nilijuwa haya siku ambayo Sinasudi alikuja mapema na kunipikia chakula cha mchana akanifulia nguo zangu kisha akaondoka. Nilivyorudi nilimkuta binti huyo mwari akiwa amevimba kwa kununa, nikamsalimia lakini alijibu kwa sauti ya chini. Nilivyomsogelea na kumuuliza kulikoni akanijibu…

“We si unatuona wengine hatufai..!” alisema binti mwari.

“Hee, kwani vipi?” niliuliza kwa udadisi

“Watu tupo humu humu unajifanya hautuoni na kwenda kuokota mishangingi huko barabarani” alisema binti mwari kwa kulalamika.

Hapo sasa ndio nikaunganisha na matukio ya nyuma na kuelewa.

Kwa kuwa tayari Sinasudi alishanifundisha nanma ya kuwajuwa wanawake, nikamwambia yule mwari kuwa kesho nitampeleka kwa Bahresa (Kariakoo) kwenda kula ashkrim (ice cream). Alifurahi sana na sura yake ikakunjuka. Kweli kesho yake baada ya kutoka Feri nilienda nyumbani na kumkuta tayari akiwa amejiandaa.

“Mama natoka na Pazi twaenda kwa Bahresa hapo jirani” alisema kwa kupasa sauti akimuaga mama yake.

Wazazi wa maeneo ya Pwani malezi yao wanayajuwa wenyewe. Maana unaweza ukasikia ama kuona mama akimwita mwanawe wa kumzaa kama hivi…

Ashakum si matusi

“We mwana K-mamayo! Njoo hapa!”

Yani hapo ndio amemuita mwanawe wa kumzaa labda mara ya kwanza hakusikia ndio akapasa sauti, da!

Ama unaweza kusikia baba akimtukana mwanawe

“K-mamayo!” mbele ya mama yake mzazi lakini cha ajabu mama mzazi atajibu “ya shangazi yake!” na kila mmoja akaendelea na shughuli zake kana kwamba hakuna jambo liliotokea.

Tulifurahia ‘mtoko’ ule na kurudi jioni sana, maana baada ya kula ice cream tulienda ‘fete’ viwanja vya mnazi mmoja ambapo kulikuwa na mabembea yaliwekwa kwa ajili ya kufurahisha watu hususani watoto ingawaje huwa yanaondolewa na kupelekwa sehemu nyingine kwa madhumuni hayohayo ya kibiashara na ustawi wa jamii.

Nilimnunulia zawadi ndogo ndogo mbalimbali ikiwemo leso, mkufu na hela kiasi. Alifurahi sana. Tukiwa huko matembezini nilimueleza kuwa Sinasudi ni mchumba wangu, hivyo asinivurugie maana yeye nilimuona mdogo hivyo wala sikumuweka akilini, alikuwa ana miaka 16 hivi.

Mwari alitulia kidogo na kutuachia nafasi lakini alihakikisha nimemtoa ‘utepe’ wake wiki chache zilizofuta na fujo za hapa na pale siku moja moja.

'Udongo' wa kizazi cha maeneo ya pwani huwafanya mabinti wadogo katika umri wa miaka 15 tu kuwa na maumbile makubwa hususani matiti, na imekuwa kawaida kwao (siyo wote lakini) kuanza ngono mapema sana.

Uhusuiano wangu na Sinasudi ulizidi kuimarika hadi ikabidi ahamie kwangu kienyeji. Tukawa tunapika na kupakua.
***********

Maisha yalienda vizuri kwa miaka miwili hapo Dar es Salaam, nikiendelea kuwa na uhusiano na wanawake wawili kwa wakati mmoja huku mmoja akiwa hamjui mwenzake.

Kwa kuwa nilidhamiria kumuoa Sinasudi basi bidii za kumpatia ujauzito zilikuwa kubwa lakini bila mafanikio, hadi nikaona bora nijaribu kwa binti mwari kama atashika maana nilianza kupata wasiwasi na afya yangu ya uzazi.

Basi ile kujaribu tu kufanya naye katika siku zake za uchevusho, haikupita wiki mbili akaniambia hajisikii vizuri, anahisi kichefuchefu sana asubuhi akipigwa mswaki na akila baadhi ya vyakula.

Miezi miwili ilipopita alimshirikisha mama yake, mama yake wala hakushtuka sana bali alikuwa kama amefurahi hivi.

Siku moja katika maongezi yangu na Sinasudi nikagusia kuhusu mimi kumpa ujauzito binti mwari. Alishtuka sana na kuanzisha varangati ndani. Nilijitetea kuwa sikuwa na uhusiano naye bali nilimshawishi tu ili mimi nijaribu kuona kama mbegu zangu zipo vizuri...

Haikusaidia kitu, vurugu ilikuwa kubwa hadi nami ikabidi nianze kupandisha sauti.

"Kwa kawaida mimi ni mpole kama unavyo nifahami mzee... "Alisema

" Lakini ikabidi nianze kupaza sauti kwa kumlaumu yeye kuwa mwanamke gani asiyeshika mimba licha ya kuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka miwili." Alisema Pazi.

Sinasudi ni mwanamke rika langu lakini yeye alitangulia kuyajua mapenzi kabla yangu, hivyo alishakuwa na uhusiano na wanaume wawili kabla yangu.

Hakika ndiye aliyenifundisha kuwajuwa wanawake hadi nami nikawa mwalimu kwa binti mwari.

Varangati lilipokuwa kubwa mle chumbani kwangu upepo ulimgeukia nilimuona akijirudi na kianza kuwa mpole kisha kuniomba msamaha na kunieleza ukweli.

"Samahani Pazi, kutokushika mimba si kwa makusudi, mimi wala siyo tasa, nilishawahi kushika ujauzito..." Aliongea Sinasudi kwa sauti ya kutia huruma.

"Baada ya kuachana na bwana niliyekuwa naye kabla yako, niliumia sana na wakati huo nilikuwa nina ujauzito wake wa miezi mitatu. Tuligombana, alinipiga sana na kuniumiza, makovu haya unayoaona siyo ya kuanguka na baiskeli kama nilivyokuambia awali, nilikudanganya, hiki ni kipigo kutoka kwa yule baba wa kikurya ambaye alikuwa mwanajeshi" Sinasudi aliendelea.

"Mimi nilikuwa ni mwanake wake wa pembeni na yeye alikuwa ameoa na alikuwa akiishi na mke wake kijiji cha Mwenge kwenye Maghorofa ya Jeshi... "Aliendelea

"Nilipatwa na hasira sana kiasi kwamba nikaamua kuachana naye na wala sikutaka kubaki na kumbukumbu yake hivyo nilienda Mwananyamala kuitoa Mimba" Alitulia kisha akaendelea...

"Nakumbuka kwa hasira nikamwambia yule daktari anichome sindano ya kuzia nisipate ukauzito, nadhani alinichoma ya muda mrefu ndio maana sijapata ujauzito kwako na hata siku zangu huwa sizioni" Aliongea akiwa amejiimamia na kulia kwa kwikwi.

Basi ikawa ndio mwisho wa varangati tukasameheana na kuamua kuendelea na maisha.
***********

Wiki mbili baadaye mama wa binti mwari akaniita na kuniambia kuwa ana mazungumzo na mimi.

Nilivyorudi kazini baada ya kuoga na kubadili nguo nilienda kumgongea chumbani kwake, alifungua mlango na kuniambia nimsindikize Al Uruba Hotel.

Al Uruba hotel haikuwa mbali na nyumbani ni kiasi cha dakika tano tu kufika.

Ni hoteli ambayo wakati huo wasomali wengi walikuwa wakifikia hapo na kuna mghahawa (restaurant) ipikwayo vyakula vizuri sana.

Tulienda na kufika hapo mara moja na kukaa kwenye viti vya pembezoni. Mhudumu alifika na kuagiza maziwa ya ngamia na mama aliagiza mishikaki ya samaki.

Mama akanifungukia kuwa eti anajuwa kuwa mimi nampenda mwanaye, hivyo nimtunze vizuri nisimchezee...

Mama akazunguka zunguka weee mwisho ndio akalipasua jipu kuwa...

"Mwenzako Salma ujauzito umeporomoka!" Alisema

"Tangia jana usiku aliona damu zikimtoka na asubuhi ulipokwenda kazini kwako sisi tulienda hospitali na kuambiwa kuwa mimba imetoka. (Miscarriage)

Nilipatwa na ganzi fulani hivi na kuzubaa hadi aliponistua kwa kuniita jina...

"Pazi, we Pazi!..." Aliita

"Naam mama" nilitikia kwa unyonge.

"Mbona nakusemesha hujibu kitu... Nakuuliza swali hujibu, umezubaa tu vipi kwani?!" Aling'aka

"Hapana mama, nipo sawa, kwani umeniulizje?! " Nilihoji.

Akaniambia kuwa aliniuliza, je Sinasudi hahusiki katika kuporomoka kwa mimba ya mwanaye?!

Akaniambia "mimi nitafuatilia na nitajuwa tu"

"Ole wake" alionya.

Basi tukamalizia tulichokuwa tunakula na kila mmoja alirudi nyumbani kivyake.

Siku hiyo nililala nikiwa na mawazo sana kiasi ya kuhisi kuchanganyikiwa.

Asubuhi nikamwamuru Sinasudi arudi kwao kwanza, alikuwa akiishi Sharifu Shamba.

Asubuhi nilijivuta kazini lakini nikatoa taarifa kwa Mzee Muhisani ambaye ndiye aliyekuwa dereva na mmiliki wa Datsun pickup iliyokuwa inatuletea samaki Feri kuwa hali yangu kiafya haipo vizuri hivyo kesho aje na mtu wa kunisaidia.
*********

Wiki ile yote haikuwa njema kwangu maana nilianza kuona maruwerue kama ya miaka ya nyuma baada ya kutoka Mkwaja .

Hali ilipoendelea kuzidi niliamua kurudi Bagamoyo nyumbani.

Tulienda tena Mlingotini, mzee wa tiba akafanya dawa zake wee lakini sikuwa napata nafuu...

Wazazi wakaamua tujaribu kwa watu wengine.

Tukaenda kwa Mwalimu Mwaloki, amabaye inasadikiwa ni mmoja wa walii wa Mwenyezi Mungu, yeye akatusomea dua kutoka vitabu vitakatifu na kutuambia yataisha Mwenyezi Mungu akitaka.

Mwalimu huyu alikuwa ni Mwalimu wa Madrasa (chuo) maarufa sana maeneo ya Dunda hapo Bagamoyo. Alikuwa ana kila sifa ya kuitwa mcha Mungu.

Akatupatia na maji kwenye chupa ya 'orange squash' ambayo alisema ameyasomea (ameyaombea) ili niwe nakunywa kidogo kila nikihisi hali ya mvurugano inataka kunijia.

Hali ilitulia kwa wiki kama tano hivi mambo yakarudi tena...

Shangazi yangu akaaye Morogoro akapewa habari zangu na akafunga safari kuja kunijulia hali.

Shangazi " Huyu niachieni, nitazunguka naye atarudi mzimaa!" Alisema kwa sauti yake nyembamba na kali.
*********

Safari ikaandaliwa ya mimi na Shangazi kwenda Morogoro.

Tulianza Turiani, haikufaa, tukaenda Mbingu haikufaa, tukaenda Ifakara haikufaa, kote tulikuwa tunapata nafuu tu lakini baada ya siku 2 au tatu mwendo ni ule ule.

Shangazi akawasiliana na shoga yake aishie Kinondoni Dar, hivyo safari nyingine ya kwenda Dar ikaandaliwa.

Kufika Dar baada ya maongezi yao ya kina, ikaamuliwa tuende Mbwewe.

Ya Mbwewe ikawa kama Morogoro.

Tukaenda Handeni, ikawa kama Mbwewe tu.


Tukaenda Tanga mjini.

Kwa kweli tulizunguka sana, japo sikupata nafuu lakini nilijifunza mengi ya dunia.

"Baba, nimeona mengi sana, hakika hujafa hujaumbika, na wengine husema hujafa hujaumbuka." Alisema Pazi

Tanga tulielekea njia ya kwenda Mombasa sehemu wanaita Kikiboni, kweli tulimkuta mganga lakini alasema yeye hatibu maradhi hayo bali anatibu mifupa pekee lakini akatuelekeza turudi kama tunaenda Tanga mjini kisha tuingie ndani kulia kwenye machimbo ya chokaa jirani na Amboni twende ndani ndani huko hadi tukute mashamba ya mkonge kisha tuulizie.

Kwakuwa tulikuwa hatuna usafiri ilibidi twende hadi Tanga mjini kisha tukodi gari ya kutupeleka.

"Mnataka kwenda kwa Mukulu... Mie napajuwa, nimeshawahi kumpeleka mama moja kule, ila mbali, nijazieni mafuta tu full tank tukifika mtanipatia chochote baada ya kuona safari yenyewe.

Hakika watu wa Tanga wakarimu sana, hawana makuu labda uwakirofishe.

Yule dereva alitupeleka hadi kwa huyo Mganga, ni kweli palikuwa mbali maana tulifika hapo kwenye kambi ya mkonge na kuvuka daraja refu jembamba na kuelekea huko kwa Mukulu.

Baada ya kupokelewa tukakaribisha kwenye sehemu ya kusubiri, ni kwa nje palitandikwa mkeka.
Mganga Mukulu alikuwa na mteja mmoja ndani na mweingine tulikmkuta pale nje mwanamke.

Zamu yetu ilipofika, Mukulu akapiga ramri zake weee na kurudia rudia mara nyingi sana kisha akasema kuwa kuna mwanamke amenichezea... Akasema inahusiana na mambo ya mapenzi.

Shangazi akaniuliza kuhusu mahusiano (uhusiano) wangu na wanawake nikamueleza historia nzima nikaona ananiangalia kwa huruma tu

"Hao hao wanawake zako ndio wamekuchezea" alisema shangazi.

Lakini moyoni haikuniingia akilini kabisa maana maradhi yangu yalinjjia hata kabla sijawajuwa wanawake.

Lakini pia nikakumbuka kauli ya mama Salma na jinsi nilivyo muondoa Sinasudi nikahisi labda nao wanachangia kuumwa kwangu.

Tukapewa dawa za kutumia na vitu vya kufanya ikiwemo kuwasha kibatari (koroboi) bila kukizima na kuchoma makaratasi aliyotupatia yenye maandiko yasiyojulikana na kutamka manuizo wakati wa kuchoma karatasi hizo, dawa za kuoga na kupaka.

Huku hapakuwa na chale, nilishangaa sana maana kote tulipopita ilikuwa ni mwendo wa kuchanjwa tu, bahati nzuri zilikuwa chale ndogo ndogo ambazo hupotea baada ya siku kadhaa.

Siku ya tatu tulirudi wa usafiri wa kuunga unga hadi tukafika Tanga mjini maeneo ya Chumbageni jirani na mwembe mawazo sijui mwembe tayari sikumbuki vizuri.

Hapo palikuwa ni nyumbani kwa rafiki yake shoga yake Shangazi.

Ilibidi kupiga kambi hapo ya wiki moja kwa ajili ya kufanya yale mambo ya kibatari.

Siku ya kwanza kulikucha salama, lakini siku ya pili usiku ilikuwa ni vurugu mechi.

Inasemekana maeneo hayo ni makutano ya wanga usiku hivyo huenda kulikuwa na miingiliano ya masafa ya kibatari na mambo yao.

Vishindo usiku vilikuwa vingi hadi jirani nyumba hiyo hiyo tulimofikia akapandisha mashetani.

Kupandisha mashetani ni kupagawa ama kupatwa na mapepo na kuanza kuongea ongea yenye mantiki na yasiyo na mantiki.

Yule rafiki yake shangazi nikamsikia akimsemesha yule aliyepandisha usiku uleule...

"Taratibu taratibuu, njooni taratibu..." Shoga wa shangazi alisema

"Akina nani nyie na mwatoka wapi" aliuliza kama vile anaona hao anawao waongelesha ilhali hapo alikuwa huyo mama jirani aliyepandisha mashetani.

Sauti ya kiume kutoka kinywa cha yule mama ilisikika akisema wao wametoka mbali, wamekuja kuokoa jahazi, vinginevyo tutampoteza kijana wetu.

Eti tiba yangu si ya kuwasha moto bali ni ya majani tu tena inapatika bara na wala siyo pwani.

"Mpelekeni Pangani atapata njia ya kufika bara" sauti iliishia hivyo

Sasa nikawa najiuliza, Pangani na bara wapi na wapi! Maana Pangani kutokea tulipo ni mwendo wa masaa mawili au matatu tu kwa kuwa ni chini ya kilomita 80.

Shangazi na shogaye na wenyeji wetu, maana sasa watu walijaa kushuhudia wakashauriana ikaonekana nipelekwe Pangani kule kwa wajuzi wa tiba asili na Mashariff.

Jambo la koroboi likaishia palepale na asubuhi yake sote, mimi, shangazi, shogaye na rafiki yake shogaye tukaelekea Pangani.

Tukavuka mto Pangani na kufika eneo liitwalo Kikokwe.
***********

Itaendekea kesho panapo majaaliwa
Ni Mwembe mawazo ,mwembe tayari ni mombasa!
 
Nilibadilisha majina herufi moja au mbili ama tatu kwa sababu maalum (siyo code)

Nimefurahi umewajuwa hao

Basi na wengine wawatambue hao wengine kuleta uhalisia.
Binafsi nilifahamu hili na nilikuja kuona hii stori ya kweli baada ya kumtaja yule bwana wa pale border ya Horohoro japo nadhani hata kampuni ya mabasi umeitaja kivyengine au labda hapo zamani ilitumia hilo jina ila jamaa bado yupo hadi sasa pale border na kampuni ile ambayo ofisi zake ziko Kariakoo.
 
Binafsi nilifahamu hili na nilikuja kuona hii stori ya kweli baada ya kumtaja yule bwana wa pale border ya Horohoro japo nadhani hata kampuni ya mabasi umeitaja kivyengine au labda hapo zamani ilitumia hilo jina ila jamaa bado yupo hadi sasa pale border na kampuni ile ambayo ofisi zake ziko Kariakoo.
Kuchengesha kidogo inaleta ufikiri.

Ahsante kwa kushuhudia
 
Back
Top Bottom