Hatimaye Masauni - UvCCM Ang'atuka

Hatimaye Masauni - UvCCM Ang'atuka

Mkuu Nyambala,

Shukrani kwa point hizi na kuileta habari hiyo hapa.

Hivi rais anapotoa kauli za namna hii ikiwemo ile ya kubariki rushwa (takrima) hakuna hatua zozote za kumchukulia? Nothing can be done at all?

Hata siamini anataka wapinzani washambuliwe ati kisa ni tuhuma za ufisadi, hivi kweli rais anatoa kauli ya namna hii hadharani badala ya kutufahamisha ni hatua gani zinaendelea kuchukuliwa?

TIRED!

Yaani huyu mkulu ndanin ya huu mwezi ameshachemka big time hii mara ya tatu - hotuba ya wazee wa DSM kuhusu TUCTA, Takrima na hii!!!!!!

Nadhani tunachokichuhudia sasa ni his personal intelligence ukiondoa hotuba za kuandikiwa!!!! Kinda like anadhani ataonekana more confident kutoa hotuba bila kusoma lakini kumbe ndiyo anaharibu kabisa. Vilevile naturally yeye hakutakiwa kutaja sababu ya Masaunik kujiuzulu hasa ukizingatia for some reason ni interested part............ Si yeye aliyeshinikizas huyu kijana achaguliwe? Na as of latest mtoto wake anatuhumiwa kuwa ndiyo ameinjinia mpango huu! Hata kama si kweli kwa busara ndogo inaonekana anamkingia kifua mtoto wake!!!!!!

Rangi halisi za mkuu wetui sasa ndiyo zinajionyesha!
 
Mkuu,

Rais katoa kauli hii? Tena kwa mtu mwenye kufanya makosa yaliyo wazi? I still do not believe this!

JK abariki kung'olewa Masauni
Thursday, 20 May 2010 04:13
*Asema hakuna fitna, amejimaliza mwenyewe
*Wazanzibari sasa watishia kujitoa UVCCM

Na Waandishi Wetu, Iringa, Dar na Zanzibar

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi, Rais Jakaya Kikwete amebariki kung'olewa kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UV-CCM), Bw. Hamad Yusuf Masauni kuwa amejimaliza mwenyewe.

Akihutubia mkutano Baraza Kuu la Umoja wa Vijana mjini Iringa jana, Rais Kikwete alisema Bw. Masauni alipojaza umri wake kuwa mdogo kuliko uhalisia na ule unaokubalika katika umoja wa vijana, alikuwa anajimaliza mwenyewe na hivyo hakuna fitna dhidi yake.



Hata hivyo alisema kwa kuwa ni kijana mzuri, mchapakazi atapewa kazi nyingine.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete imekuja wakati kukiwa na madai ya chini chini kuwa anayeuvuruga umoja huo ni mwanaweza Ridhiwani, jambo ambalo limekanushwa na Ridhiwani mwenyewe pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba.

Akizungumzia uwezekano wa baadhi ya watu kupinga uamuzi huo, Rais Kikwete alisema: "Tulijiandaa kwamba kwa uamuzi huu, kama kuna watu watatunyooshea mabango tutakuwa na cha kuwaeleza."

Rais Kikwete alitumia nafasi hiyo kukemea makundi ndani ya umoja huo akisisitiza kuwa magenge yanawamaliza wenyewe.

Alisema hakuna sababu ya kugombania mambo ambayo wangeweza kuyamaliza ndani ya chama, na hapo hapo akawataka kujipanga kukabiliana na wapinzani wakati wa uchaguzi.

Wakati hayo yajiendelea mjini Iringa, wanachama wa Umoja wa Vijana Zanzibar wamekuja juu na kutishia kurudisha kadi za CCM kwa kile walichodai kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), kimesababishwa na majungu.

Wanachama haoa walisema Bw. Masauni amelazimika kujiuzulu kutokana na majungu yaliyopikwa na viongozi wa CCM Zanzibar yaliyotokana na mabadiliko makubwa ndani ya umoja huo ikiwemo kuziba mianya ya upotovu wa fedha.

Akizungumza na Majira Bw. Mohamed Juma aliyejitambulisha kuwa ni mwanachama wa umoja wa vijana katika Jimbo la Kikwajuni, alisema katika kipindi kifupi Bw. Masauni alitengeneza ajira ndani ya umoja huo na kuchunguza vyanzo vya mianya ya upotevu wa mapato ndani ya umoja huo.

"Alianza kwa kasi ikiwemo kujua mapato ya fedha yanayotokana na mali za umoja wa vijana kwa hiyo hilo limeonesha kuwakera baadhi ya viongozi," alisema.

Aidh alisema suala lingine linalojionesha hapo ni kwa baadhi ya viongozi kukerwa na maamuzi ya Bw. Masauni ya kutaka kugombea Ubunge katika Jimbo la Kikwajuni ambalo baadhi ya viongozi walikuwa wakilitolea macho.

Aliongeza kuwa moja ya dalili zinazoonesha kuwa Masauni ameshinikizwa kujiuzulu ni baada ya ziara yake ya kukagua uhai wa umoja wa vijana aliyoifanya hivi karibuni maeneo ya Unguja, ambapo Bw. Masauni alifika katika jimbo hilo na kupandisha bendera, kitu ambacho baadhi ya viongozi walionekana kutokubariki kitendo hicho.

Bw. Masauni tayari alikuwa na nia ya kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo ambalo pia Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Saleh Ramadhan Ferouz alikuwa na nia kama hiyo.

Hivi karibuni akizungumza na Majira, Bw. Masauni alisema amefanya mabadiliko kadhaa kwa baadhi ya maeneo ambao alisema lengo lake ni kuimarisha utendaji wa kazi na sio adhabu kwa mtu binafsi na hivyo aliwataka wananchi wasiutafsiri vibaya, hali ambayo pia inaonesha kuwa ni moja ya sababu za kushinikiza majungu ya kumtaka Bw. Masauni ajiuzulu.

Aidha alisema ziara yake katika majimbo mbalimbali ilikuwa na nia ya kuimarisha uhai katika Umoja wa Vijana ambao umekuwa ukiyumba na kudorora kwa kiasi kikubwa.

Baadhi ya viongozi wa umoja wa vijana waliopo Zanzibar na wanachama kwa ujumla wameelezea hofu yao kwamba kitendo cha kujiuzulu Masauni katika wadhifa huo ni sawa na kuipotezea Zanzibar nafasi hiyo na kuchukuliwa kwenda Tanzania Bara.

Source: Majira.
 
Yaani, mimi sijawahi kulalamika kuhusu huu ugonjwa wa Malaria Sugu lakini nadhani sasa imefika kikomo.

Ni jambo la msingi kabisa, hata kama mtu si muandishi, kufahamu kuwa kichwa cha habari ni utangulizi wa habari yenyewe; lazima kuwe na muendelezo na uhusiano!

Kwa hiyo Ridhwani Kikwete kaitisha kamati kuu ya CCM, au?
 
Hivi mbona viongozi wengine wa juu hawajiuzulu????? Kila siku naskia viongozi wa UVCCM ndio wanao jiuzulu tu.?!! Tatizo lao hawa UVCCM wamepachikwa kwa maslahi ya wakubwa ndo maana. Wanatolewa kirahisi!. Kuhusu swala la umri, Hii ni ajabu sana maana ukikutana na wajumbe pamoja na viongozi wengi wa UVCCM unaweza kuwasalimia. Mimi nina miaka 32 Najiona kijana mtu mzima hivi lakini cha ajabu kuna Siku nilimuona SHY ROSE uso kwa uso kidogo nimuamkie maana ni mmama kabisa! Kinachonishangaza iweje masauni aonekane ndio kijeba?!!!!
Mimi nazani Masaun kuachia ngazi ni Kafanywa kafara kwa Manufaa ya wakubwa flani. Ifike mahali UVCCM waonyeshe umri wa kila kiongozi ili tuwakamate wengi!.

Alafu wewe Masanilo unafikiri hii nchi ni ya Kifalme. hujui kuwa katika nchi ya Kifalme Mtoto huendeleza mambo aliyo fanya Baba yake. Labda baba yake awe amefariki!
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Taifa Bw.Hamad Y Masauni ,ameachia Ngazi ya uwenyekiti kwa tuhuma za Umri mkubwa/kudanganya Umri!!!!
Mimi nasema hii haitoshi tu iishie kwa Masauni kama ni kweli UVCCM na CCM wameamua kuwa makini na suala hili la kigezo cha umri katika Uongozi wa Jumuiya hiyo.
Viongozi wa juu kabisa wa CCM na UVCCM wanajua kabisa kuwa kuna wenyeviti wengi wa Mikoa,wilaya,kata na hata shina na matawi kuwa wana umri ambao si sahihi kwa wao kuwa viongozi ndani ya Jumuiya hiyo.
Sasa kama wameamua kuanzia kwa Masauni basi mimi nawaambia wasiishie hapo waende hadi kwenye Matawi.
Najua wanajua kuwa kuna watu wengi sana ambao umri wao bado ni utata sana,sasa kama hizi hazikuwa vitina basi kazi waianze na isiwe mwisho tu kwa Masauni.
 
Mimi nasema kwamba
CCM imefoji kubakia madarakani maana tulishaacha kuipigia kura miaka yote ila inashinda kwa kishindo tu kila wakati.

CCM yote ni jinai tupu na viongozi wake ndo haooo wanaumbuka peupeee!

Dawa ni moja tu kuinyima kura
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Taifa Bw.Hamad Y Masauni ,ameachia Ngazi ya uwenyekiti kwa tuhuma za Umri mkubwa/kudanganya Umri!!!!
Mimi nasema hii haitoshi tu iishie kwa Masauni kama ni kweli UVCCM na CCM wameamua kuwa makini na suala hili la kigezo cha umri katika Uongozi wa Jumuiya hiyo.
Viongozi wa juu kabisa wa CCM na UVCCM wanajua kabisa kuwa kuna wenyeviti wengi wa Mikoa,wilaya,kata na hata shina na matawi kuwa wana umri ambao si sahihi kwa wao kuwa viongozi ndani ya Jumuiya hiyo.
Sasa kama wameamua kuanzia kwa Masauni basi mimi nawaambia wasiishie hapo waende hadi kwenye Matawi.
Najua wanajua kuwa kuna watu wengi sana ambao umri wao bado ni utata sana,sasa kama hizi hazikuwa vitina basi kazi waianze na isiwe mwisho tu kwa Masauni.

Hivi huyu Masauni si walimuweka 'wao' kwa fitina dhidi ya Nape Nnauye? Leo iweje tena wamgeuke Masauni? Je wakati wanampa hayo madaraka kwa nini hawakufanya uchunguzi wa kupata taarifa zake kuhusu umri ambazo eti miaka 2 baadaye ndio wanakuja nazo. Tena walikuwa na sababu nzuri ya kuhakikisha kwamba hakuna atakayechaguliwa kwa kutokuwa na umri unaotakikana maana tayari walifanya umri ndiyo 'agenda' ya kumuengua Nape.

Hii ninadhihirisha jinsi ambavyo viongozi wa CCM na jumuiya zake wasivyomakini katika kazi zao. Siku hizi mambo yanaendeshwa kwa hisia, fitina na majungu tu na si kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
 
Rais Kikwete alisisitiza:, "Kwa hiyo hakuna aliyeonewa, aliyefitini na wala watu wasitafute mchawi katika hili. Hatua kama hii ilikwishafanyika kwa watu kama akina Nape (Nnauye)." Nape naye alienguliwa katika uchaguzi wa UVCCM uliopita.

Kwa nini atoe mfano wa Nape? Kwani Nape alifoji vyeti vyake ama ni umri wake ulikuwa umepita umri unaotakikana?
 
wanasheria mnasemaje kuhusu hili kosa la masauni kughushi umri? Je anaweza kushitakiwa? na kama atatiwa hatiani, adhabu yake ni nini?
 
Hawa Tanzania Daima wana tendency ya kuandika headlines ambazo ni childish,ukilinganisha na magazeti mengine.
 
Juzi tu kafa dada mmoja alionyesha nia ya kugombea kule mwanza...na kukubalika na wakubwa wachama. Lakini baada ya kufariki nawatu kusema kuwa kuna mkonowa mtu....nikashangaa viongozi baadhi yao wanajitokeza na kusema hapana.. Eti alikuwa na matatizo ya akili toka mdogo..!!!!!! Hivi hawa si si emu ni vichwa maji! Inamaana angepita tungekuwa tuna ongozwa na kichaa sio??? Hebu wadau nisaidieni...sasa haya ya masuni kufoji umri inamaana hawakuyaona wakati ule??/? Hii inaonyesha jinsi wasivyo makni....ndio maana hata mswada wa sheria ya uchaguzi jaamaa kausaini kwa mbwembwe..akatokea msamaria mmoja anaitwa dr slaa akastukia janja ya nyani!....kweli tutafika kwa mtaji huu???????????????????????????????????????????????
 
Kijana anatakiwa asizidi miaka 30 SHY-Rose ni kamanda wa vijana kama Filikunjombe kule Ludewa, Makamanda wa vijana ni jina walilopewa washauri wa vijana. Kwa hiyo MF ukiteuliwa kuwa mshauri wa Vijana UVCCM (W) Kinondoni basi utaitwa kamanda wa vijana wa wilaya ya kinondoni.
Mbogela . Asante kwa kunifumbua macho. Hata hivyo umeamsha maswali mengi sana. Naona picha hizi ni za wazee wa over 30 years mbona? wanatafuta nini huku kwa vijana? Au ni mwendelezo wa usaniii ule ule wa sisi M?
Funga kazi itakuja wakati wa uchaguzi utaona watakaogombea kupitia uv sisi majizi ni wale wale wa over 30!
 
Umenena Mkuu, wengi hapo ni wangangaji wa njaa tu, we miaka 42 (Kijeba)unajiita UVCCM? teh teh teh. Siasa si mahala pa kukupa hela ya kula na familia yako - siasa ni wito.
ELNINO unashangaa nini? hata wakati wa uchaguzi 2005 nilisikia wakimuita JK eti kijana! Usishangae hata sasa watamuita yeye na Lowasa vijana! watanzania kwa usanii wananiacha hoi!
 
Hakuna cha Ridhwani wala nini, kama mtu amefanya forgery ya aina hiyo basi lazima atoke. Ridhwani anaingia vipi.
 
Back
Top Bottom