Kuna jambo moja ambalo ningependa wenzangu tuwe tunaliangalia kila tukio linapotokea. Tujifunze kutazama zaidi, tuhamishe macho yetu kutoka katika mtu au watu wanaohusika na kuzama kwa mampana katika maudhui yanayolizunguka tukio.
Swala la UVCCM linachekesha na vilevile linatukumbusha namna tunavyoongozwa na mazoea. Tanzania tunapata bahati saana kujifunza kwa mifano tena iliyo hai. Hili swala la watu kutafuta nafasi, cheo au uongozi kwa mbinu yoyote ile limekua ni donda ndugu.
Pia tatizo jingine ninaloliona apa ni ufinyu wa fikra na umakini wa watu wengi. Hata hawa wajumbe wa UVCCM nao wana matatizo makubwa, kama wanachagua uongozi uliokosa sifa then they are part of the problem and they have to go as well. They have failed as well.
Kufumbia macho maovu ni dhambi kubwa na mshahara wake huwa mnene na wenyewe kuambatana na bonasi nono, yaani kudumaa kwa mambo na uwajibikaji. Kuna watu pale bungeni wamethibitika kuwa na vyeti bandia, kuna watu huko kwenye maofisi na wanavyeti hadi majina feki. Tatizo ili ni kama mzizi wa mwarobaini, limeenea kote nchini na hili la Masahuni ni tone katika bahari hii pana.
Kama kweli tumeamua kuchukua hatua, tuhakikishe sasa hili swala linakuwa ni vita ya kila mtu mahali alipo, tuondokane na viongozi, watumishi na wafanyabiashara feki (wenye vyeti na nyaraka za kugushi).
Ningependa kuona na sheria inachukua mkondo wake tena kwa uwazi na kasi. Maaana imeishaonekana kuwa mtu ameghushi vyeti. Tazama benki zinavyochukua hatua pale mteja anayegushi hundi. Polisi hufika mara mojja na kumbeba mtuhumiwa na mara moja taratibu za kesi huanza.
Sitashangaa kusikia idara husika zikitupiana mpira kuhusu jinai iliyo mbele yetu.