Hatimaye Masauni - UvCCM Ang'atuka

Naomba kuuliza tu kwani kijana kwa mujibu wa UV SISI M ni miaka mingapi? na huyo Shy rose ni kijana? Ni swali tu!

Mie nimeshangaa haswa,nakumbuka back 1997 nikiwa Ngaza Secondary huyu mdada alikuwa pale Nyegezi Social (SAUTI) akisoma na alikuwa kama kwenye mid 20's,kama mpaka sasa bado ni kijana,basi tena.
 
yaani ccm kama si fisadi basi na usiingie chama hicho! hakuna aliye msafi!
 
Nikiangalia hizi picha sura zote zimekomaa? Hawa ni wazee au vijeba? Kiumbo wengi naona wana umri karibu sawa na Masauni

Umenena Mkuu, wengi hapo ni wangangaji wa njaa tu, we miaka 42 (Kijeba)unajiita UVCCM? teh teh teh. Siasa si mahala pa kukupa hela ya kula na familia yako - siasa ni wito.
 
ninacxhoweza kusema ni angalau hawa vijana wa CCm wamewaonyesha njia wakubwa zao kwa kuweza kuwajibishana - ingawa sababu yenyewe si niliyoitarajia. Angalau suala lingekuwa ni ufisadi ningesema naam..... wakubwa wao nao wakae chonjo. nakubaliana na wanaosema kuna watu flani wanataka kuingia -- nina wasiwasi sana na yule Msomali, kwani kuna RA ambaye ni kingmaker na ambaye bado anazo nyingi za kagoda-- za kuwamwagia akina shyRose nk.
 
Mkuu niliguswa sana. Ila pia ukweli uko pale pale kwamba hata hili dude (linalojiita chama) limeua watu wengi sana wasio na hatia makusudi au kwa sera zake za kinyang'au.

Poa mkuu, tuko pamoja.

respect na muzee wa dark city!!!
 
Na bado manyang'au yamekula kila kitu sasa yanaanza kulana yenyewe kwa yenyewe,ingekuwa skendo hii inahusu vyama vingine ingebebewa bango ile mbaya na hawa nyang'au,upo wapi TAMBO HIZO TUMEKUMISI HEBU LETE PROPAGANDA ZAKO ZA KUKANUSHA KILA KITU
 
Masauni anasema wanampinga kwa sababu ya msimamo wake wa kusimamia rasilimali za umoja. Kwa kauli hiyo utagundua ugomvi huu ni kwa sababu ya hela. Ufisadi unaanzia awali kabisa!
 
Naona kuna utata katika habari ya kwenye gazeti la mwananchi (hard paper vc online). ninaomba kunukuu sentensi zifuatazo kisha tujiulize ukweli ni upi:

Mwananchi online: "Habari zinasema kuwa Masauni alitakiwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake, lakini aligoma na kujitetea dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008"

Mwananchi hard Paper lililo mtaani: "Habari zinasema kuwa Masauni alijiuzulu saa mbili usiku baada ya kubanwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008.

Swali: ukweli ni upi?
 
Umenena Mkuu, wengi hapo ni wangangaji wa njaa tu, we miaka 42 (Kijeba)unajiita UVCCM? teh teh teh. Siasa si mahala pa kukupa hela ya kula na familia yako - siasa ni wito.

Nenda mikoani mfano angalia Mwanza M/kiti wake naye ni kijeba na inajulikana aligushi umri na sakata lake kuzimwa zimwa. Wote ni vijeba tu
 
Naona kuna utata katika habari ya kwenye gazeti la mwananchi (hard paper vc online). ninaomba kunukuu sentensi zifuatazo kisha tujiulize ukweli ni upi:
Mwananchi online: "Habari zinasema kuwa Masauni alitakiwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake, lakini aligoma na kujitetea dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008"

Mwananchi hard Paper lililo mtaani: "Habari zinasema kuwa Masauni alijiuzulu saa mbili usiku baada ya kubanwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008.

Swali: ukweli ni upi?

Ni tafsiri tu, nadhani sahihi ni kuwa awali Mwaka 2008 Masauni aliwahi kutakiwa kujiuzulu kutokana na Kashfa ya umri akagoma kujiuzulu, lakini leo amejiuzulu saa usiku kutokana na kashfa hiyo inayomkabili ambayo makamba aliwahi kumtaka ajiuzulu na kukataa. Nadhahi sahihi ni hivi kwa mawazo yangu.
 
Yes ni vema ajiuzuru na wengine je?Shy Rose Bhanji mbona kabaki??kama sikosei anakaribia ki-fifty hivi...wapo wengi tu...Nnchimbi je aliachia Uenyekiti na miaka mingapi??Hii ni mizengwe ndani ya CCM
 
Masauni anasema wanampinga kwa sababu ya msimamo wake wa kusimamia rasilimali za umoja. Kwa kauli hiyo utagundua ugomvi huu ni kwa sababu ya hela. Ufisadi unaanzia awali kabisa!

Hilo linaweza kuwa kweli lakini pia huyu bwana amefanya kosa la jinai (kughushi nyaraka).

Passport yake inaonesha alizaliwa mwaka 1973 wakati cheti cha kuzaliwa kinaonesha amezaliwa mwaka 1979. Cheti cha kuzaliwa kimetolewa mwaka 2007, mwaka ambao Masauni aliwasilisha nyaraka kwa ajili ya kuchaguliwa/teuliwa kwenye uongozi wa UV-CCM. Utaratibu ambao UV-CCM imejiwekea ni kuwa kijana anaegombea nafasi ya uongozi (katika UV-CCM) anatakiwa awe na umri uziozidi miaka 30 (wakati anachaguliwa).]

Sasa kama hizi habari za kughushi nyaraka ni za kweli, nadhani hili halitakiwi kuishia kwenye kujiuzulu tu...inatakiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
 
Yote heri na tunawatakia CCM wakubwa nao waamke na kuanza kuwekana sawa

  • ila kwa bahati mbaya sana naona CCM inachukua media coverage kubwa kutokana na kupangilia mambo yao very strategically... Kumbukeni hii story ikiisha itakuja nyingine hadi October, matokeo yake ccm itakua akilini mwa wengi wakati shida zetu hazijatatuliwa
  • mafuta bei imezidi kiwango chochote kile kilichowahi kufikiwa katika historia
  • huduma za jamii hazikidhi haja
  • mawaziri wanatumia muda, magar na allowances za serikali kuzunguka majimboni
Dawa ni media black-out kwa mkutano wa uvccm kama kweli tunataka matatizo ya wananchi yapewe kipaumbele
 
quote_icon.png
Originally Posted by kanyagio
Naona kuna utata katika habari ya kwenye gazeti la mwananchi (hard paper vc online). ninaomba kunukuu sentensi zifuatazo kisha tujiulize ukweli ni upi:

Mwananchi online: "Habari zinasema kuwa Masauni alitakiwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake, lakini aligoma na kujitetea dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008"

Mwananchi hard Paper lililo mtaani: "Habari zinasema kuwa Masauni alijiuzulu saa mbili usiku baada ya kubanwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008.

Swali: ukweli ni upi?

Ni tafsiri tu, nadhani sahihi ni kuwa awali Mwaka 2008 Masauni aliwahi kutakiwa kujiuzulu kutokana na Kashfa ya umri akagoma kujiuzulu, lakini leo amejiuzulu saa usiku kutokana na kashfa hiyo inayomkabili ambayo makamba aliwahi kumtaka ajiuzulu na kukataa. Nadhahi sahihi ni hivi kwa mawazo yangu.

nadhani ni zaidi ya hapo, mimi nadhani kwamba gazeti lilichapishwa usiku likiwa limepata hiyo habari. na inawezekana Masauni hajajiuzulu kwa hiyo Mwananchi wakaamua kurekebisha online version. Ni mawazo yangu tu na sijajua ukweli ni upi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom