Wadau ninanukuu kile ambacho kinadaiwa kusemwa na rais wetu kuhusu sakata la kujiuzulu kwa Masauni:
Nanukuu: Hata hivyo, Rais Kikwete alimfariji kijana huyo mpole na mzito kufanya maamuzi magumu na haraka, akisema kwakuwa ni makakamavu na mchapakazi atapangiwa kazi nyingine hapo baadaye. mwisho wa kunukuu (Source: Gazeti la mwananchi la leo 20 May 2010)
Jamani naomba mnisaidie huenda mimi ndo sielewi vizuri mambo haya. Hivi kama ni kweli huyu kijana amegushi umri rais anapata wapi ujasiri wa kusema atampangia kazi nyingine? Hivi ni kazi gani nyingine ambayo haiitaji mtu kuwa mwadilifu? Kama mtu ameweza kudanganya umri na hilo likajulikana na "akalazimishwa" kujiuzulu atashindwa vipi kufanya udanganyifu mwingine kwenye hiyo kazi nyingine atakayopewa? Au atawekwa kwenye kamati ya "saidia CCM ishinde" ili afanikishe udanganyifu wa kura?
Nisaidieni mwenzenu, napata shida kuamini kuwa viongozi wetu wamefikia hapo. Au nchi hii haina kabisa watu wanaoweza kuwa viongozi hivyo inabidi wale wachache waliopo tung'ang'ane nao hata wanapoonyesha upungufu mkubwa kama wa kudanganya. Ni jambo gani ambalo mtu akilifanya ktk nchi hii linamnyima nafasi ya kuwa kiongozi wa umma?

3]mtu gani hapatii hata siku moja[/B], na huyo masauni alimteua mwenyewe baada ya songombingo za huku bara akina nape. Hajawahi kupatia hata chembe.