Hatimaye Masauni - UvCCM Ang'atuka

Hatimaye Masauni - UvCCM Ang'atuka

mhhh hawa si ndio wana mganga wao anasema ukitaka kufa chukua fomu ya kugombea uone..hahaaaaaaaaaa .JK mjanja sana kumbe ndo maana alikataa kwenda kufungua mkutano huu kule iringa ....
 
UV SISI M ni miaka mingapi? na huyo Shy rose ni kijana? Ni swali tu!
Kijana anatakiwa asizidi miaka 30 SHY-Rose ni kamanda wa vijana kama Filikunjombe kule Ludewa, Makamanda wa vijana ni jina walilopewa washauri wa vijana. Kwa hiyo MF ukiteuliwa kuwa mshauri wa Vijana UVCCM (W) Kinondoni basi utaitwa kamanda wa vijana wa wilaya ya kinondoni.
 
MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, sasa anatajwa waziwazi na kuhusishwa na mpango wa mapinduzi ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Tanzania Daima Jumatano imeelezwa.

Baadhi ya vyanzo vya habari kutoka ndani ya UVCCM vimeliambia gazeti hili kuwa mtoto huyo ndiye anayevuruga umoja huo.

Ridhiwani, ambaye ni mwanasiasa kinda, lakini kwa kuwa mtoto wa rais anakuwa na ushawishi mkubwa ndani ya chama, anatajwa kuwa kinara wa mkakati mchafu unaolenga kumuengua Mwenyekiti wa umoja huo, Hamad Masauni Yusuf.

Mtoto huyo, ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, anadaiwa kuwa ndiye msukaji wa mkakati wa kumng’oa Masauni katika wadhifa wake.

Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam na miongoni mwa viongozi wa ngazi ya juu wa umoja huo waliopo mkoani Iringa, zinaeleza kuwa nyaraka zilizoenea kwenye vyombo vya habari nchini kuhusu kashfa ya Masauni kuhusu tuhuma za kughushi umri wake, zimetokana na kazi ya Ridhiwani.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano umebaini kuwa viongozi hao wanabadilishana taarifa nyeti kuhusu mgogoro wa umoja huo na kumtaja Ridhiwani kama mhusika mkuu wa kuupanga na kuutekeleza.

Ridhiwani mwenyewe anakana kuhusika na mkakati wa kumng’oa Masauni, lakini anatajwa kuwa kiongozi wa kundi la viongozi waandamizi wa umoja huo linalopinga mabadiliko yanayolenga kuipeleka jumuiya kwenye maendeleo endelevu.

Habari zaidi zimesema viongozi wa UVCCM wamekuwa wakibadilishana taarifa za ujumbe mfupi wa simu ya mkononi unaodaiwa kumsakama kutokana na mkakati wake dhidi ya viongozi wema wa umoja huo.

Ujumbe huo umekuwa ukisambazwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM ambalo lilikutana jana mjini Iringa.

Ujumbe huo ambao pia umetumwa kwenye simu za baadhi ya waandishi wa gazeti hili, unasomeka:

“Ndugu Rizwan (Ridhiwani) Kikwete, tuna taarifa za kutosha juu ya mkakati wenu unaolenga kutaka kuathiri jitihada zetu za kupigania na kuchangia ushindi wa chama chetu na viongozi wake kupitia taasisi yetu iliyotulia ya UVCCM, ikiwemo mipango unayoiongoza kuandaa makala ya gazeti kumchafua Mwenyekiti wa UVCCM taifa, sisi vijana wapenda amani ndani ya jumuiya na chama, kamwe hatutavumilia hali hii, tukiamini kuwa hiyo si haki na wala si njia sahihi ya kujenga jumuiya yetu.”

Sababu za kumng’oa Masauni

Duru za kisiasa kutoka ndani ya UVCCM, zinasema mkakati wa kumuengua Masauni kwenye nafasi yake ulianza miezi minne iliyopita pale baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wenye ushawishi mkubwa, walikuwa wakifanya vikao vya siri kuibua kashfa hiyo.

Sababu inayoelezwa na duru hizo ni kutokana na msimamo wa Masauni wa kutokubali kuyumbishwa na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo waliopania kuifanya UVCCM taasisi yao binafsi ili wafanye biashara.

“Wapo wenzetu waliotaka kumtumia Masauni kufanya biashara ndani ya UVCCM, msimamo wake wa kutetea rasilimali za jumuiya ndio uliomfikisha hapo. Lakini ukiziangalia nyaraka zile unaona zinaweza kuwa na ukweli.

“Lakini swali ni kwanini hoja hiyo imeibuliwa leo?” alihoji mmoja wa wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM ambaye ameshurutishwa asitajwe gazetini.

Sababu nyingine inayotajwa na duru hizo za siasa ni dhamira ya Masauni kutaka kuwania ubunge katika Jimbo la Kikwajuni, nafasi anayotazamia kuiwania Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhani Ferouz.

“Lakini pia kuna suala la uchaguzi wa UVCCM uliopita. Kilichopo ni kwamba maumivu ya uchaguzi ule bado hayajapona. Kumbuka Masauni alichaguliwa baada ya Rais Kikwete kuamua nafasi ya mwenyekiti iende Zanzibar kama njia ya kutuliza joto la kiuongozi lililokuwa linafukuta katika jumuiya,” alisema mmoja wa wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM.

Masauni alichaguliwa Desemba 2008 katika uchaguzi uliokuwa umejaa utata hata kusababisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete, kupendekeza Masauni ambaye alikuwa amegombea nafasi ya makamu mwenyekiti ndiye ateuliwe kugombea uenyekiti.

Waliokuwa wameomba na kugombea uenyekiti wote walitoka Bara, ambao ni Hussein Bashe na Benno Malisa. Hawa waliteuliwa kugombea umakamu.

Kauli ya Masauni

Alipozungumza na Tanzania Daima Jumatano, alisema taarifa za kuwapo kwa nyaraka hizo amezisikia muda mrefu na anajua walioziandaa na kuzisambaza.

“Nipo Iringa, baadhi ya wajumbe nimewasikia wakisema wanazo nyaraka hizo, binafsi pia nimezipata lakini ni tuhuma za uongo, zinalenga kunipunguzia kasi yangu ya utendaji katika usimamizi wa rasilimali za umoja, maadili na uwajibikaji,” alisema Masauni.

Masauni ambaye kwa kuwa mwenyekiti wa UVCCM anaingia kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, - ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) – alisema kuna kikundi cha watu kilichodhani kingeweza kumburuza katika maamuzi.

Alisema mbinu za kikundi hicho zimegonga mwamba ndiyo maana wameamua kumchafua kupitia tuhuma za uongo.

Masauni ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), iliyotuhumiwa kuvuruga uchaguzi kwa nia ya kuipendelea CCM, ametamba kuwa UVCCM ni imara na itaendelea hivyo chini ya uongozi wake.

“Nitaendelea kusimamia vema matumizi bora ya rasilimali za umoja na chama kwa ujumla. Nitajitahidi kustawisha uongozi unaozingatia maadili na uwajibikaji bila ya kujali watu wanaotaka kunipunguza kasi,” alisema.

Hata hivyo, Masauni hataki kujieleza kwa ufasaha anapoulizwa kuhusu umri wake hasa kwa kujaribu kubadilisha mwelekeo wa mazungumzo.

“Nilichaguliwa kwa vikao halali ambavyo kabla ya hapo watu waliangalia rekodi zetu (wagombea wote). Waliangalia mambo ya uadilifu na yote ya msingi... katika mambo yote haya vikao vya chama na hata vyombo vya usalama vilishiriki, sasa sijui watu wanachosema,” alijibu.

Alipoulizwa kama haoni ni vema akajiuzulu ili kulinda hadhi yake, Masauni alisema hana mpango huo na badala yake anaelekeza nguvu kuwaunganisha vijana kuleta umoja na kuwajengea uwezo wa kimaendeleo.

Ridhiwani ang’aka

Kwa upande wake, Ridhiwani ambaye ameingia katika siasa za CCM kwa nguvu kubwa tangu baba yake alipoukwaa urais mwaka 2005, alishangaa kusikia madai ya kuhusika katika mkakati wa kusambaza nyaraka za kashfa dhidi ya Masauni.

Akijibu kwa kifupi tuhuma hizo kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi, Ridhiwani, badala ya kujieleza vizuri, aliandika tu: ‘Ahahaha.’

Hata alipobanwa na mwakilishi wetu aliyeko mkoani Iringa kabla ya kuingia ukumbini kuanza kikao cha Baraza Kuu, Ridhiwani alisema anatarajia kujibu tuhuma hizo baada ya kikao hicho ambacho kilikuwa kikiendelea hadi usiku jana.

Wajumbe Zanzibar wacharuka

Katika hali inayoonyesha kuwapo mpasuko baada ya kuibuliwa kwa kashfa dhidi ya Masauni, wajumbe wa Baraza Kuu kutoka Zanzibar wamecharuka na kusimama kidete kumtetea.

Zaidi ya wajumbe 50 waliokutwa wakishuka kwenye boti bandarini Dar es Salaam juzi na jana kwa ajili ya kuunganisha safari ya Iringa, walisikika wakiimba nyimbo za kumtetea Masauni na kupania kwenda kumtetea.

“Tuachieni Masauni wetu, tumekuja kumchukua kwenda naye Z’bar…, kumbe mlimpa kwa shingo upande...,” yalikuwa baadhi ya maneno waliyotoa kwenye wimbo wao.

Habari zaidi kutoka mkoani Iringa, zinasema kuwa baadhi ya wajumbe waliozungumza na gazeti hili wametaka iundwe tume kuchunguza nyaraka hizo ili kubaini ukweli.

Wakizungumza bila kutaja majina yao, wajumbe hao walisema endapo itabainika kuwa kweli Masauni alighushi umri wake, lazima awajibike.

“Kama anasingiziwa, basi walioandaa mpango huo wawajibishwe hata kama ni Ridhiwani,” alisema mmoja wa wajumbe kutoka Pemba.

Masauni anadaiwa kughushi umri wake ili kupata nafasi hiyo nyeti ndani ya umoja huo.

Nyaraka zimeenezwa kwenye vyombo vya habari tangu mwishoni mwa wiki zikidai kuwa Masauni ametaja umri tofauti wa kuzaliwa kutoka kwenye cheti chake cha kuzaliwa na nyaraka za kuombea pasipoti ya kusafiria.

Waraka huo unaonyesha alizaliwa Oktoba 3, 1973, wakati fomu zake za kuomba hati mpya ya kusafiria zinaonyesha alizaliwa Oktoba 3, 1979.

Masauni anatarajiwa kumaliza muda wake wa kikatiba wa uongozi ifikapo mwaka 2012. Akilazimika kujiuzulu au kuondolewa, atakuwa amekosa pia nyadhifa zote za kisiasa.

Wakati huohuo, Rais Kikwete amelazimika kuitisha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya dharura kesho, pamoja na mambo mengine, kujadili kashfa na mzozo ulioibuka ndani ya UVCCM


SOURCE: TANZANIA DAIMA
 
Hivi ni asilimia ngapi ya hawa wanachama wana nia ya kufanya kazi njema ya siasa au just opportunist ?
 
yah acha waumbuane ,duh na hawa wazanzibar watamgeuka JK wanasema kumbe alipewa uongozi kwa shingo upande! ahaa ukizingatia mtoto mtu ndio ka-injinia
 
masauni.jpg

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana CCM (UVCCM) Hamad Yusuph Masauni ambaye inadaiwa kuwa amekalia kuti kavu katika jumuiya hiyo

Ramadhan Semtawa, Dar na Leon Bahati, Iringa

JOTO la kisiasa ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM sasa limefikia nyuzi 100, baada ya naibu katibu mkuu wa jumuiya hiyo visiwani Zanzibar, Nassoro Moyo, kuamua kujiuzulu, huku mwenyekiti wake, Hamad Yusuph Masauni, akiwa amekalia kuti kavu.

Tangu juzi, vijana hao wa CCM wamejichimbia mjini Iringa kwa ajili ya mkutano ho muhimu wa baraza kuu, ambao ulitanguliwa na semina na kamati ya utekelezaji lakini ukiwa umegubikwa na msuguano ambao unakiweka chama katika wakati mgumu katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba.


Kabla ya kwenda Iringa, tayari wajumbe walishaingia kwenye vita baada ya kusambazwa waraka uliokuwa ukimtaka Masauni ajiuzulu huku wajumbe wengine kutoka kambi ya mwenyekiti huyo nao wakimtaka Moyo aachie ngazi.


Hadi jana jana jioni, hali ilikuwa ni ya wasiwasi baada ya kufanyika kikao cha kamati ya utekelezaji ambacho inaelezwa Moyo aliandika mwenyewe barua ya kujiuzulu kwa maslahi ya umoja huo.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, Moyo aliandika barua hiyo ikiwa ni sehemu ya kunusuru jumuiya katika kipindi hiki ambacho imekumbwa na mparaganyiko mkubwa.


Wakati wote jioni, ukumbi wa Siasa ni Kilimo ulikuwa umedhibitiwa vema na polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakishirikaina na wana usalama wengine.


Habari zinasema kuwa Masauni alitakiwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake, lakini aligoma na kujitetea dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008.


Hali tete ilianza kwenye kikao cha sekretarieti ya umoja huo ambayo iliwajadili viongozi hao wawili kwa muda mrefu, kuliko hata ilivyokuwa imekadiriwa kwa mkutano huo kufanyika.


Masauni anaweza kusubiri maamuzi ya kamati kuu ambayo yatatakiwa kuwasilishwa kwenye kikao chas halmashauri kuu ya CCM kwa ajili ya kupata baraka. Uamuzi huo unaweza kufanyika kunusuru umoja na chama baada ya kujiuzulu kwa Moyo.


Mkutano huo ulianza saa 2:30 asubuhi na ulipaswa uwe umekamilika kabla ya saa 3:30 ili kupeleka ajenda zinazotakiwa kujadiliwa na kikao cha baraza kuu, kwenye kikao kingine cha kamati ya utekelezaji ili zipitishwe.


Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, kuchelewa kukamilishwa kwa kikao hicho kulitokana na mvutano mkubwa ulioibuka kutokana na pande mbili kupingana, kila moja ikotoa sababu za kutaka mmoja kati ya viongozi hao wawili ajiuzulu.


Baraza kuu lilikuwa lianze saa 4:00, lakini kutokana na kikao cha sekretarieti kumalizika saa 6:20, iliamuliwa kuwa kikao cha baraza kianze saa 8:00 na kuwataka wajumbe wajiandae, wakati huo ndipo wajumbe wa kamati ya utekelezaji wakakutana.


Mkutano wa kamati hiyo ulipokea taarifa za sekretarieti juu ya mada za kujadiliwa kwenye baraza kuu na kabla ya kuanza kwa kikao, Moyo aliwasilisha barua ya kukubali kujiuzulu kupisha uchunguzi wa kile kinachoitwa ni kuvuruga chama.


Katika tuhuma hizo, Moyo anatajwa kuzusha vurugu ndani ya umoja huo, akidaiwa kushiriki kusambaza nyaraka za kumpinga Masauni.


Mvutano mkali pia ulielezwa kuzuka ndani ya kamati ya utekelezaji na hadi saa 12:00 jioni kikao hicho kilikuwa hakijamalizika na taarifa zikawepo kwamba baraza hilo lianze kwa semina ndogo kuhusu mada ya ugonjwa wa Ukimwi ili kuweka sawa mambo.


Taarifa nyingine zinadai kwamba, kundi linalopinga Masauni kulazimishwa kujiuzulu liliibuka na hoja kwamba kuna kundi la mafisadi ambao wanataka aondolewe kwenye madaraka yao ili wamuweke mtu wao ambaye atajenga mazingira mazuri ya ushindi wa rais kwa mwaka 2015.


Hadi jana mchana ajenda za kikao cha baraza kuu zilikuwa bado hazijajulikana huku baadhi ya wajumbe, akiwemo Makamba akichia jukumu hilo viongozi wa jumuiya hiyo.


Makamba alipoulizwa alichukuaje kitendo cha kutojulikana kwa ajenda za mkutano saa chache kabla ya baraza kuanza kikao, alijibu: "Mimi ni mjumbe tu, ajenda wanapanga wenyewe watendaji, muulize katibu mkuu wa UVCCM."


Lakini, vyanzo vingine vilidokeza kwamba juzi usiku Makamba alimtaka Masauni ajiuzulu, hatua ambayo mwenyekiti huyo aliipinga na kutaka kwanza arudi kwa wapiga kura wake akawaeleze.

Kuhusu madai kuwa wanachama wanaomuunga mkono Masauni walipanga kuandamana, Makamba

alisema:" Kwanza waandamane kwenda wapi? Mimi nasisitiza siwezi kumwambia mtu ajiuzulu kwa tuhuma... halafu wanamtaja na Ridhiwani (Kikwete, mtoto wa rais)... yeye ana mamlaka gani kumshinikiza Masauni ajiuzulu?


"Huku ni kumwonea tu kijana huyu na kutaka kumhusisha katika mambo ambayo hahusiki wala hajatenda. Waache kumchafua kijana wa watu, sijakuwa naye popote kushinikiza mtu ajiuzulu. Ni uongo mtupu.


"Ridhiwan ni mjumbe kama nilivyo mimi; sisi sote ni wajumbe tu ndugu yangu; tuna mamlaka gani ya kumshinikiza mtu ajiuzulu. Waache fitna; waache kumchafua; kijana wa watu hajatenda chochote."


Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, jana jioni wajumbe 38 wa Baraza Kuu kutoka Zanzibar walitanda eneo la ukumbi wa mikutano wakitaka kumuona kwanza mwenyekiti wao Masauni akiwa amekalia kiti, ndipo waingie ukumbini.


Chanzo: Gazeti la Mwananchi
http://www.mwananchi.co.tz/componen...ia-kuti-kavu-ffu-watanda-eneo-la-mkutano.html
 
Lakini mkuu kuna taarifa kuwa ameshajiuzuru kutoka kwenye thread nyingine hapa ,anybody anaweza unganisha haya!!?
 
Hivi na mtoto wa JK si yuko kwenye UVCCM? Sio kuwa wanataka njia kwa ajili ya watoto wao?
 
Ridhiwani ni moja ya watu wanaoongoza kundi na kampeni za kungoa masauni, nadhani nae sasa roho yaje kwatu sasa...........................haya sasa makanu mwenyekiti si ndio ulikuwa wajiita Mwenyekiti? ..........yametimia sasa
 
Mwenyekiti wa UV-CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete
Huyu jamani sio M/kiti UVCCM
Shy Rose ni mjumbe bwana maana makamanda wa vijana ni vyeo vya kugombea ubunge tu haviko kikatiba lakini mdada kala chumvi ya kumwaga :yuck:
 
MV Bukoba iliua watanzania...labda hukuguswa na hiyo ajali!
Mkuu niliguswa sana. Ila pia ukweli uko pale pale kwamba hata hili dude (linalojiita chama) limeua watu wengi sana wasio na hatia makusudi au kwa sera zake za kinyang'au.
inawezekana huna nia mbaya but this has gone way over board and please edit unaweza kuumiza waliopoteza vipenzi vya mioyo yao

Poa mkuu, tuko pamoja.
 
Bwana JK anataka familia yake yote iwe na madaraka ya juu kwenye serikali ya nchi, mkewe ndio kukicha kutembelea miradi ya maendeleo na kupewa taarifa na watendaji wa serikali wakati uwezo kichwani mdogo na si kiongozi wa serikali (mwalimu wa grade B ambaye awezi kufundisha zaidi ya STD one), mwanae huyu ndio hivyo tena, pale mlimani amepata LLB yake kwa kubebwa kwa hali ya juu, nasikia alikwisha disco Makandara akambeba. JK mwenyewe hata aieleweki alipataje hiyo BA Economics, pia alifanya MA ikamshinda!
 
Back
Top Bottom