Hatimaye Masauni - UvCCM Ang'atuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye Masauni - UvCCM Ang'atuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Prodigal Son, May 18, 2010.

 1. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Wakuu kwa mujibu wa Mdau Francis Godwin kutoka Iringa mwenyekiti wa UV CCM na makamu wake wamejiuzulu jioni hii

  [​IMG]
  Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete

  [​IMG]

  Wajumbe wa baraza wakisikiliza kwa makini kikao cha baraza ambacho kinadaiwa kuwa moto kwa mwenyekiti wa UV-CCM Hamad Yusuph Masaun ambae ametangaza kujiuzulu usiku huu

  [​IMG]


  [​IMG]
  Wajumbe wa baraza wapigwa na butwaa ukumbini

  Mpenzi mdau wa mtandao huu habari hii ni kutoka ndani ya kikao hicho ambapo inadaiwa kuwa mwenyekiti wa UV-CCM taifa na makamu katibu wa UV-CCM Bw.Moyo wamejiuzulu nafasi zao ,hizo ndizo tetesi za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho japo ukweli halisi utaupata mapema asubuhi ili kujua sababu hasa na maelezo yao kabla ya kujiuzulu kwao japo Masauni ni juu ya sakata la kudaiwa kufoji veti huku Moyo ni hatua yake ya kuendeleza makundi Visiwani

  [​IMG]

  Habari hizi ni kwa msaada wa Blog ya Francis Godwin
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na kife tumechoka loh!
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kisa hasa mbona sijakielewa? Huu ni mwendelezo wa mmeguko nini?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ndipo watamkumbuka Nape!!
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kweli Ulaji ni kitu cha hatari sana. For internal health of CCM tunahitaji kuwa na Chama kingine chenye nguvu sawa na CCM ili Hawa jamaa wagawanyike, ila kwa sasa wanajirundika wote waroho ndani ya CCM matokeo yake ni kuuana (Kama tulivyoona kule mwanza wiki iliyopita), kufukuzana kazi kwa kukosa uweza wa kuongoza ya UWT. Nakumbuka mtoto wa Malecela Mkwawi alidumu kwenye nafasi ya Uenyekiti wa UV-CCM kwa siku tatu au nne kabla kifo cha ghafla hakijamkuta.

  Wasipoangalia watamalizana wenyewe kwa wenyewe na hiyo ndiyo itakuwa nusura kwa Tanzania, Kwani majambazi wanapodhulumiana na kuchapana huwa ni nafuu kwa raia wema maana huenda wakaacha wizi hasa kama watatoana macho au kukatana viungo
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nadhani mbado sana!

  Hili kokoro limezidiwa sana. Tatizo ni kwa nini halizami kabisa likapotelea mbali huko baharini?
   
 7. J

  Janejo Member

  #7
  May 18, 2010
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  MV Bukoba iliua watanzania...labda hukuguswa na hiyo ajali!
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  May 18, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,427
  Trophy Points: 280

  ....kuhusu nape kama ..huyu masauni amejiuzulu kwa swala la umri ....basi hata nape umri umekata kidogo!!...nadhani hili ni fundisho..hasa kwenye jumuia hizi .... watu wanakaa mpaka wanafikisha miaka 40
  bado wanajiita vijana...sanasana wanawazibia vijana wachanga kuingia siasa...

  nadhani pia umakini mkubwa unaitajika kwenye kuteua wagombea ubunge[vijana]...kuzuia vijeba basi kila mgombea aweke umri wake hadharani...asije akateuliwa na baada ya muda tukaambiwa ni kijeba...kama wale vijeba wa COPA COCA COLA!!!!
   
 9. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amejiuzulu huko Iringa ambako kuna kikao cha UVCCM na bado kinaendelea; nimepata habari hii kutoka TBC-1 saa nne kamili; mwenye habari zaidi atuhabarishe zaidi; kumbukeni JK alipiga debe sana apatiwe Mzanzibar; huenda alimjua kabla ila sasa ndio hivyo inaonekana maamuzi yake hapa hayakwenda kwa undani wa ki-inteleginsia maana faking age means you can fake anything on you front and implies CCM yote ilikuwa faked for almost 3 years chini ya Masauni.
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Naomba kuuliza tu kwani kijana kwa mujibu wa UV SISI M ni miaka mingapi? na huyo Shy rose ni kijana? Ni swali tu!
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  inawezekana huna nia mbaya but this has gone way over board and please edit unaweza kuumiza waliopoteza vipenzi vya mioyo yao
   
 12. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2010
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Wewe umenena.......

  Ajabu ni kwamba kuna watu wanaombea na kuota kuwa JK, Msekwa, Makamba, Rostam, Makala, Chenge, Mkuchika na Chiligati watoke/waondelewe kwenye uongozi wa juu wa CCM bila kutambua kwa kina kuwa kuwepo kwao hawa katika uongozi wa juu wa CCM, ndiyo itapelekea kuanguka na hatimaye kufa kwa CCM kama tuijuavyo.

  Nadhani Tanzania kwa ujumla itafaidika sana kwa hawa kuendelea kubaki na uongozi (utawala??) wa CCM kwa kipindi kingine cha miaka 5, na baada ya hapo CCM itakuwa imekula makinda yake kiasi kwamba itawawia vigumu kujipanga upya na kwa nguvu.

  Na bado, kipindi cha kura za maoni tutaona mengi tu.

  Adui yako muombee njaa...............................
   
 13. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nikiangalia hizi picha sura zote zimekomaa? Hawa ni wazee au vijeba? Kiumbo wengi naona wana umri karibu sawa na Masauni
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Hawa mapandikizi wa UVCCM wachache sana ni vijana. Hilo liko wazi ila mtu mwenye umri mkubwa na asiyetakiwa huwa suala la umri linakuwa disqualification ya kwanza
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,239
  Trophy Points: 280
  Habari hizi ni kweli. Nimethibitishiwa toka kikaoni.
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kiongozi mbona hata TBC1 wamerusha !!
   
 17. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Haya ni makubwa sasa, Ningependa kuwaambieni kitu, wanompiga vita masauni na kumnyooshea vidole ningependa kuwauliza ndani ya UVCCM je kila mmoja wenu nae atupe umri wake wa kweli basi maaana najua fika ndani ya UVCCM ni wachache sana wenye umri mdogo kwani hii sheria nayo hajazingatiwa ukitizama ni vijana wachache sana katika nchi hii ndio wako UVCCM na wenye umri mdogo na wengi wao ni umri mkubwa sasa pia UVCCM nanyi hili mkalijadiri na umri uwe mwisho 35.

  nimeona matukio mengi ya viongozi wa UVCCM ndio wanao jiuzulu lakin cha ajabu Masaun anachia ngazi kwa kosa la Umri je hao Viongozi wakuuwa CCM wano kutwa na kashafa nyingi na bado wako wanang'ang;ania madaraka ndani ya CCM au NEC je mbona hawaachii ngazi?

  CCM kuna tatizo na inapaswa wakaechini wajichunguze sana na kwa makini wasije jisahau wakadhani hao viongozi wao ndio CCM hata kidogo wasije jidanganya yatakuja wakuta tu huko mbeleni.

  Nilisha wambieni UVCCM ni hawana hata kauli mbiu NAPE alisema saaana na waka mdharau hao hao UVCCM hata kumuunga mkono wao wakapiga kimya hizo pesa za mafisadi na zinawachanganya sana na hamtokuja iongoza hii nchi amini nawambieni ninyi viongozi wa UVCCM mliopo kwasasa simameni na mjisimamie msingojee kuambiwa na mfanye jinsi hao wakubwa zenu watakavyo mtaburuzwa mpaka lini

   
 18. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  kinacho nikela sana UVCCM ni kuwa baadhi ya Viongozi waliochaguliwa ni walipitishwa kwa nguvu ya viongozi wakubwa ndani ya CCM na viongozi wenye majina makubwa ndani ya CCM kwa dhumini la kuwalinda katika chaguzi ambazo hao viongozi wakubwa watakapo gombea hizo nyadhifa na ndio maana utakuta hawa UVCCM wanakuambia kiongozi fulani ni mzuri sana kumbe hapo ujue kuna jambo na pesa ilipita mlango wa nyuma, Agalieni sana wenyeviti wengi waliochaguliwa si wa wilaya au mikoa ni lazima kuna mkono wa kiongozi mkumbwa wao ni kuangalia akipitishwa A au B ninani atakuwa mtu wa kuwalinda? Wao wanachagua B na wanamwacha A wakijua fika A angechaguliwa wanajichimbia kaburi kabisa kwani A hanamzaha ni yupo kwa ajili ya maendeleo ya vijana na sio kwa ajili ya huyo kigogo kumshangilia ktk uchaguzi wake au kumpigia kampeni katka uchaguzi zake, mifano mizuri ni kwa uchaguzi huu ulipo jirani angalia viongozi wengi ni wale wale na sio viongozi to UVCCM sasa sielewi UVCCM inajijengea nini wakati najua fika wao ndio makamanda wa vita katka kampemi za chaguzi nyingi kwanini wao wasiweke mgombea wao wanemwamini na hato wanyanyasa, Iweje wao wawe watumwa kwa viongozi waliko juu i mean wakubwa??

  Inafika mahali UVCCM wanapaswa kuja na KAULI mbiu yao na kujikomboa katika hili la sivyo watakuwa ni watu wa kuburuzwa kila kukicha ndani ya UVCCM na CCM yeneyewe.

  UVCCM badilikeni sasa nawambieni muache fitna chuki unafki na roho chafu ndani yenu, zaidi ni nini mpaka mwekeana vinyongo na wivu kati yenu. kwamfano tokea mlivyomaliza chaguzi zenu za kuwachagua W/viti na wajumbe wa baraka kuu na wajumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya mikoa na taifa siju kama mlisha wahi kaa tena na kujadiri nini Mustakabri wenu wa UVCCM na mwaenda wapi na mwatoka wapi? hakuna hata siku mmoja mwadai labda katiba au kanuni fulani ibadilishwa ni sikuzote ndio muzeee yaanai na elimu yenu yote hamuwezi kukaachini na kujaribu kuweka mabadiliko? ni chama gani au umoja gani usio ona mapungufu au kifungu fulani kibadilishwe? siku zote katiba na kanuni za Umoja wenuziko sawa tu kadri siku ziendavyo no way mwatudanganya kuna lenu jambo ndani ya UVCCM kuweni wawazi na wakweli. Nasema haya kwani najua fika ni Pesa inawafanya mtengane nasi chochote kweli njaaa ni mbaya sana tamaaa nayo haifai siju mwajua neno COUNTRY FIRST au ni basi kila apatae chake basi asi mguse mwenzie.

  Kujiuzulu kwa M/kiti mie sishangai sana kwani najua fika ndani yenu kuna watu walitegemea hilo sana na walikuwa wanaliombea sana na hii yote ni nyie wenyewe wasio mwingine mchawi ni nyie na hakuna mchawi wa kutoka nje kaja ati kuwa tibulia ni nafsi zenu na zita wasuta.

  MKITAKA SHINDA HII VITA NI KUSIMAMA IMARA NA KUONGEA LUGHA MMOJA NA KUWA NA KAULI MMOJA NA MSHIKAMANO NDIO MTASONGA MBELE
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ridhiwani uko wapi hebu chukua mikoba ya Masauni......!
   
 20. G

  Godwine JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kijana kwani ni ufalme huu
   
Loading...