Maswali ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne hujibiwa na wanafunzi laki tatu. Lakini mwisho wa siku division Zero, Four na Three zinakuwa laki mbili na nusu.
Kwa hiyo usinambie "watu watano wametoa majibu mbona huelewi"?
Mwingine anasema fomu ya kufungulia akaunti ndio itakufunga kwa sababu benki wanauliza pesa umepata wapi. Benki gani duniani inakuuliza umepata wapi pesa? Umetembea duniani lakini wewe? ATM machine nazo huwa zinakuhoji uki deposit pesa? Hilo jibu sio ridiculous?
And what if ume deposit pesa chafu kwenye akaunti ya mkeo, na wewe huna mkataba wala ahadi na benki hiyo kwamba utaweka fedha halali, atafungwa mkeo? Na wewe utapona?
Mwingine anasema ukinununua asset kwa pesa chafu ukaja ukaiuza ndio kosa. Kwa hiyo ukinunua hoteli ukaihodhi, ukala faida ya huduma za hoteli, sio utakatishaji?
Mwingine anasema ni kuweka benki au kuwekeza. Kwa hiyo ukiituma kwa Western Union kutoka TZ kwenda UK hujatakatisha? Hivi mnajua transactions anazoshutumiwa amezifanya Kitilya wa TRA kufanya atiwe ndani bila dhamana mpaka leo?
Haya, kwa ma definition tuliyopewa yoooote hayo, Ndama Shabani kafanya lipi kwa pesa chafu, kafungua Islamic Missonary School?