Hatimae Pedeshee Ndama akiri kutakatisha fedha

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Screenshot from 2017-05-19 09-28-32.png
Mfanyabiashara, Ndama Shabani Hussein (Pichani katikati) maarufu kama Ndama mtoto ya Ng'ombe amekiri mahakamani kosa la kutakatisha zaidi ya billioni 1.2.

Ndama anadaiwa kuwa Februari 20, 2014 jijini Dar es Salaam, alighushi nyaraka ya kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha maboxi manne ya dhahabu yenye kilogramu 207 yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.

Chanzo: Nipashe
 
Naombeni mnisaidie maana ya hili neno "kutakatisha fedha"
Kutumia njia ya udanganyifu ili kuzihalalisha fedha zilizopatikana kwa njia haramu.

Kwa mfano:-
Unauza ngada, mapato yatokanayo na ngada unafungulia bureau de change. Sasa mapato yatokanayo na biashara ya bureau de change yatakuwa halali yenyewe pamoja na mtaji wake.

Wengine ongezeeni mifano.
 
play guilty? Itakuwa maji yalimfika shingoni au kulikuwa na evidence ya kutosha! I wonder ile miti aliyoiegemea kwa miaka mingi imekatika au?
Bashite na gambo wanacho cha kujifunza hapa.
 
Kesi ya money laundering (kutakatisha pesa) ukitiwa hatiani ni kifungo jela miaka 4 au 7 sasa huyu kama kweli amekiri atakuwa ametumia technique koz angeweza kukaa rumande kwa mrefu zaidi ya miaka tajwa kama yanayomkuta wakili msomi Mwala kule Arusha yupo rumande mwaka wa saba mfululizo mpaka sasa kwa kosa hilohilo.
 
Back
Top Bottom