Hatimae Pedeshee Ndama akiri kutakatisha fedha

Hatimae Pedeshee Ndama akiri kutakatisha fedha

Hela alitumiwa tayari ili asafirishe dhahabu.. Lakini dhahabu hakuwatumia.

Kama alilipwa hela lakini dhahabu hakutuma kwa nini ahangaike kupeleka serikalini nyaraka feki zinazoonyesha kampuni yake inaruhusiwa kusafirisha dhahabu ajikamatishe?
 
Hivi nikiokota dhahabu shambani kwangu ya kilo ishirini nikaenda kuiuza kwa wanunua madini na mimi sina efd ya kuwapa kuwa nimeauzia dhahabu lakini tukaandikishana kwa karatasi za kawaida ! Na mimi ela zangu zitakuwa chafu!?
Katika mazingira hayo hayo kama hujaenda kukutana na maofisa wa kodi unakuwa kwenye mazingira halali ya kuhusika na utakatishaji. unatakiwa ufike ofisi za TRA ukaeleze ulichovuna na serikali wapate chao.
 
Naombeni mnisaidie maana ya hili neno "kutakatisha fedha"
Chukua mfano huu,
Mtu akiiba pesa za uma na ikawa bahati mbaya kwake kabla hajaziwekeza akakamatwa hapa atakuwa ameshikwa na kidhibiti.Ila kama atafanikiwa kuzitumia pesa hizi kuwekeza biashara yoyote maana yake ni kwamba atakapoonekana ni tajiri chanzo cha utajiri kitaonekana ni biashara na si wizi wa pesa za uma.Kwa msingi huu pesa chafu zimefanywa zionekane safi kwa kivuli cha biashara.Hio ndio mqana ya kutakatisha fedha.
 
Wizi ni wizi tu na dhulma ni dhulma tu hata kama utafanya kimya kimya UTALIPA TU SIKU MOJA
asilimia 99 ya wanadamu hawana maadili,wengine wezi,dhulmati,tapeli etc
so why wengine hawalipi,
mobutu alikuwa mwizi sana wa pesa za umma,lakini alikufa kwa uzee na ugonjwa,
idd amini alikuwa anasemwa anakula roho za watu,amemu outlive nyerere,kafa kwa uzee.
George bush kaua wairaq milion moja bado anadunda licha ya kuwa ana zaidi ya miaka 80.
Kuna watu wema sana hapa duniani ambao mwisho wao ulikuwa mbaya sana.
Japo pia wapo walioishi kwa amani mpaka mungu akawachukua,
kwahiyo sio lazima alipe,ni mipango ya mungu tu
 
Duh huyu ndio yule Ndama Mtoto wa Ng'ombe aliyekuwaga anamwaga pesa kwenye majukwaa ya muziki?! Aisee kweli jela mbaya
Tangu lini Ndama aliwahi kuwa mnene zaidi ya hapo? Kama hamuwafahamu watu kaeni kimya!
 
kama atafanikiwa kuzitumia pesa hizi kuwekeza biashara yoyote maana yake ni kwamba atakapoonekana ni tajiri chanzo cha utajiri kitaonekana ni biashara na si wizi wa pesa za uma.Kwa msingi huu pesa chafu zimefanywa zionekane safi kwa kivuli cha biashara.Hio ndio mqana ya kutakatisha fedha.

Lazima uwekeze?

Ukizikalisha benki hujatakatisha fedha?
 
Wapigaji ni wengi sana..ndio maana hapo awali comment yangu nilisema..hii industry..ina watu wengi sana...na ikichimbuliwa ipasavyo..watakao pona ni wachache sana...

Hakuna ambaye si mpigaji sema umepata bahati mbaya uko nje ya system siku mfereji wa sarafu ukipita miguuni kwako ndio utanielewa,viongozi wetu WAPIGAJI kiwango cha lami mpaka wa dini wapo kwa sasa pambana na hali yako mzee na hakuna wa kuondoa upigaji wakati tunanufaika wote nakuombea zamu yako ifike uone mema ya nchi.
 
Sikumaliza darasa la saba, uko sahihi.

Haya, tuachane na kumjadili mtu ambae hata la saba sijamaliza.

Kutakatisha fedha maana yake nini?
Sikumaliza darasa la saba, uko sahihi.

Haya, tuachane na kumjadili mtu ambae hata la saba sijamaliza.

Kutakatisha fedha maana yake nini?

Walimu wako wa darasa la pili walipata shida sana.

Watu zaidi ya watano wametoa maana ya kutakatisha fedha na mifano juu ila wewe bado tu unarudi na hilo swali.
 
Walimu wako wa darasa la pili walipata shida sana.

Watu zaidi ya watano wametoa maana ya kutakatisha fedha na mifano juu ila wewe bado tu unarudi na hilo swali.

Maswali ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne hujibiwa na wanafunzi laki tatu. Lakini mwisho wa siku division Zero, Four na Three zinakuwa laki mbili na nusu.

Kwa hiyo usinambie "watu watano wametoa majibu mbona huelewi"?

Mwingine anasema fomu ya kufungulia akaunti ndio itakufunga kwa sababu benki wanauliza pesa umepata wapi. Benki gani duniani inakuuliza umepata wapi pesa? Umetembea duniani lakini wewe? ATM machine nazo huwa zinakuhoji uki deposit pesa? Hilo jibu sio ridiculous?

And what if ume deposit pesa chafu kwenye akaunti ya mkeo, na wewe huna mkataba wala ahadi na benki hiyo kwamba utaweka fedha halali, atafungwa mkeo? Na wewe utapona?

Mwingine anasema ukinununua asset kwa pesa chafu ukaja ukaiuza ndio kosa. Kwa hiyo ukinunua hoteli ukaihodhi, ukala faida ya huduma za hoteli, sio utakatishaji?

Mwingine anasema ni kuweka benki au kuwekeza. Kwa hiyo ukiituma kwa Western Union kutoka TZ kwenda UK hujatakatisha? Hivi mnajua transactions anazoshutumiwa amezifanya Kitilya wa TRA kufanya atiwe ndani bila dhamana mpaka leo?

Haya, kwa ma definition tuliyopewa yoooote hayo, Ndama Shabani kafanya lipi kwa pesa chafu, kafungua Islamic Secondary School?
 
Okay.

Kwa hiyo ukitumia pesa chafu kununua asset kama hoteli, halafu ukabaki nayo, isiiuze. Hapo ni poa, huna kosa la kutakatisha?
Duh! What do you "ukabaki nayo!? " simply ni kuwa Pesa itayotokana na hiyo hotel itakuwa imetakatishwa!
 
Walimu wako wa darasa la pili walipata shida sana.

Watu zaidi ya watano wametoa maana ya kutakatisha fedha na mifano juu ila wewe bado tu unarudi na hilo swali.

Maswali ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne hujibiwa na wanafunzi laki tatu. Lakini mwisho wa siku division Zero, Four na Three zinakuwa laki mbili na nusu.

Kwa hiyo usinambie "watu watano wametoa majibu mbona huelewi"?

Mwingine anasema fomu ya kufungulia akaunti ndio itakufunga kwa sababu benki wanauliza pesa umepata wapi. Benki gani duniani inakuuliza umepata wapi pesa? Umetembea duniani lakini wewe? ATM machine nazo huwa zinakuhoji uki deposit pesa? Hilo jibu sio ridiculous?

And what if ume deposit pesa chafu kwenye akaunti ya mkeo, na wewe huna mkataba wala ahadi na benki hiyo kwamba utaweka fedha halali, atafungwa mkeo? Na wewe utapona?

Mwingine anasema ukinununua asset kwa pesa chafu ukaja ukaiuza ndio kosa. Kwa hiyo ukinunua hoteli ukaihodhi, ukala faida ya huduma za hoteli, sio utakatishaji?

Mwingine anasema ni kuweka benki au kuwekeza. Kwa hiyo ukiituma kwa Western Union kutoka TZ kwenda UK hujatakatisha? Hivi mnajua transactions anazoshutumiwa amezifanya Kitilya wa TRA kufanya atiwe ndani bila dhamana mpaka leo?

Haya, kwa ma definition tuliyopewa yoooote hayo, Ndama Shabani kafanya lipi kwa pesa chafu, kafungua Islamic Missonary School?
 
Back
Top Bottom