KISUTU: Ndama Shabani Hussein (Pedeshee Ndama) jela miaka 5 au faini 200 milioni

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,897
19,080
Baada ya ndama kukiri kosa la kutakatisha pesa , leo mahakama imemhukumu kwenda jela miaka 5 au kulipa faini 200 milioni.

Awali mfanyabaishara Ndama Hussein maarufu kama mtoto wa Ng’ombe alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka sita ikiwamo kughushi na kutakatisha Dola za Kimarekani 540,390 (sawa na Sh, bilioni 1.181).



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kulipa faini ya Sh200 milioni mfanyabiashara, Ndama Shabani Hussein maarufu kama Pedeshee Ndama mtoto ya Ng’ombe baada ya kulikubali na kutiwa hatiani katika shtaka la sita la kutakatisha dola za Marekani 540,000.

Akitoa hukumu hiyo leo Ijumaa, Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa amesema endapo mshtakiwa huyo atashindwa kulipa kiasi hicho cha fedha atatumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Hukumu hiyo ya shtaka la sita la kutakatisha fedha ilitolewa baada ya Wakili wa Serikali, Christopher Msigwa kumsomea maelezo ya awali (PH) Ndama na kuyakubali maelezo yote yanayounda shtaka hilo la kutakatisha fedha, akapatikana na hatiani na kupewa adhabu hiyo.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili Msigwa aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa amekubali shtaka la sita la kutakatisha fedha na maelezo yanayounda shtaka hilo.

“Hatuna kumbukumbu za nyuma za makosa dhidi ya Ndama ila ni rai ya upande wa mashtaka kuwa wakati mahakama ikitoa adhabu izingatie matakwa ya kifungu cha 13(a) cha sheria ya kuzuia utakatishaji fedha,” imesema hati ya hukumu.

Amesema pia mahakama ibebe dhana ya sheria hiyo ambayo lengo lake ni kuzuia makosa ambayo yanalenga kudidimiza uchumi wa nchi na uzito wa kosa ambalo mshtakiwa amelifanya.

Kwa upande wa Wakili Wabeya Kung’e anayemtetea mshtakiwa huyo kwa kushirikiana na Jeremiah Mtobesya, Kung’e ameiambia mahakama kuwa ni wazi mshtakiwa amekiri kosa baada ya kusomewa maelezo ya awali hivyo mahakama isitoe adhabu kali kwa mshtakiwa.

Ameiomba mahakama izingatie maombi yao kwa sababu mshtakiwa huyo hilo ndiyo kosa lake la kwanza, kitendo chake cha kukiri kosa kinaonyesha kusikitikia kosa alilolitenda na kwamba anayo familia ambayo inamtegemea ambao kwa kipindi cha mwaka mmoja ambacho amekaa ndani imepata shida kwa kukosa huduma yake.

“Kwa kuzingatia kifungu cha 13(a) cha sheria ya kutakatisha fedha ni rai yetu mahakama tukufu isitoe adhabu kali kwa mshtakiwa kwa sababu amejutia kosa alilolitenda,” amesisitiza Kung’e. Hivyo Ndama amehukumiwa kulipa faini ya Sh 200 milioni ama akishindwa kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Juni 6, 2017 Ndama aliiomba mahakama akumbushwe shtaka, akakumbushwa na Wakili wa Serikali, Esterzia Wilson na akalikubali shtaka hilo.

Akisomewa maelezo ya awali mahakamani hapo, Ndama alikubali maelezo ya awali aliyosomewa ikiwamo nyaraka zilizotumika kufungua akaunti iliyotumika kuingizwa fedha hizo, hundi 18 zilizotumika kutolea fedha hizo, maelezo ya benki ‘bank statement’ na Swift massage.

Iwapo atakamilisha kulipa Sh200 milioni atakuwa huru kuendelea katika mashtaka matano mengine yanayomkabili mahakamani hapo ambayo upelelezi wake bado haujakamilika.

Ndama anatakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika na atoe fedha taslimu kiasi cha Dola za Marekani 270,200 ambacho ni sawa na zaidi ya Sh600 milioni mahakamani hapo na mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.


Chanzo: Mwananchi

1. Pedeshee 'Ndama mtoto wa ng'ombe' kortini kwa kutakatisha fedha
2. Hatimae Pedeshee Ndama akiri kutakatisha fedha
3. Pedeshee Ndama akiri tena kutakatisha fedha kiasi cha $540,000
 
Aina mpya ya wahalifu waungwana, hawaisumbui Mhakama kwa kukataa makosa waliyotenda bali wanakiri. I wish na wezi wa serikalini wangeiga mfano huu!
Kwa kesi ile ya kutakatisha pesa ndama hakua na namna maana haina dhamana hivyo akaona haina maana kuendelea kukaa mahabusu.

Pili wanasheria wake watakua walimshauri baada ya kuona labda udhaifu wa sheria.

Hiyo adhabu ndama atailipa fasta tu na kutoka maana hata kama hana mapedeshee wenzake hawatamuacha.
 
Aina mpya ya wahalifu waungwana, hawaisumbui Mhakama kwa kukataa makosa waliyotenda bali wanakiri. I wish na wezi wa serikalini walioingia mikataba ya madini na IPTL wangeiga mfano huu!
Mkuu hiyo ilikua ni mbinu tu ili apate hii hukumu yenye option ya faini au kifungo , nina uhakika anakusudia kulipa hiyo faini watachangishana wapigaji wote watamtoa magereza atarudi barabarani kuendelea kuwapiga wazungu.
Naifahamu hii shuhuli yao vema.
 
Mkuu hiyo ilikua ni mbinu tu ili apate hii hukumu yenye option ya faini au kifungo , nina uhakika anakusudia kulipa hiyo faini watachangishana wapigaji wote watamtoa magereza atarudi barabarani kuendelea kuwapiga wazungu.
Naifahamu hii shuhuli yao vema.
Hiyo kesi tulijua tu lazma huyo mpigaji achomoke mana ukiona mtu kakiri kosa ni kua anajua nini kinafuata..kuna jamaa yangu alinunua gari yke mwez umeisha kwa bei ya kutupa
 
Tz ya siku hizi raha sana.
Unakataa kosa unapewa dhamana.
Unaenda kwa loyer Au hakimu anakwambia hapo ni kifungo au fain ya xxxx utamwambia poa.
Kesho mahakamani unakubaliharaka hakuna kupoteza muda tena.
Unasomewa hukumu unawapa hela yao unasepa.
UUnaiba mil 100 fain lak2 au miez 6.
Hatamjinga vp anajua ch kufanya
 
Mkuu hiyo ilikua ni mbinu tu ili apate hii hukumu yenye option ya faini au kifungo , nina uhakika anakusudia kulipa hiyo faini watachangishana wapigaji wote watamtoa magereza atarudi barabarani kuendelea kuwapiga wazungu.
Naifahamu hii shuhuli yao vema.
Ndio maana nikasema 'muungwana', kwamba kuanzia sasa hata mtaani atatambulika kama mtakatisha pesa. Isije ikawa kama yule jamaa aliyewahi kuiba pesa za umma na kufungwa jela alafu alivyomaliza kifungo akakata rufaa na kufutiwa maskosa then akatumia hiyo gear kugombea ubunge na akaupata aisee!
 
Ndio maana nikasema 'muungwana', kwamba kuanzia sasa hata mtaani atatambulika kama mtakatisha pesa. Isije ikawa kama yule jamaa aliyewahi kuiba pesa za umma na kufungwa jela alafu alivyomaliza kifungo akakata rufaa na kufutiwa maskosa then akatumia hiyo gear kugombea ubunge na akaupata aisee!
Nani huyoo?
 
Back
Top Bottom