Hataki kuchukua mahari yake nifanyeje??

Hataki kuchukua mahari yake nifanyeje??

Status
Not open for further replies.
Kishe
Habari wanajf na heri ya pasaka.

Niende kwenye lengo la uzi...mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miezi 7 nina miaka 26. Miezi 3 iliyopita nilitengena na mzazi mwenzangu ambaye alishanitolea mahari na kunivalisha pete ya uchumba kwa sasa nipo nyumbani na mtoto wangu.

Mwanzoni nilipata wakati mgumu sana kukubali kwamba tumetengana lakini namshukuru Mungu sasa hivi nimekubaliana na hali na nipo vizuri kabisa.
Baba mtoto wangu alikataa kabisa kuchukua mahari yao na pia kuwashirikisha wazazi juu ya kutengana kwetu kwa madai tulikutana wawili tuu wakati pete tulivalishana mbele ya wazazi na ndugu wa pande zote.
Swali langu ni je naweza kuingia kwenye mahusiano mapya wakati yeye hajachukua mahari yake? Na je kwa mfano mtu akataka kuja kutoa mahari inakuwaje kuhusu mahari yao ya mwanzo haitakuwa na shida yoyote maana hataki kuchukua kabisa na watu wanasema kubaki na mahari yake itanifunga sababu kimila bado nitakuwa mke wake. Ninachohofu mbeleni asije leta shida akasema ni mchumba wake halali sababu temetengana kienyeji sana. Naombeni msaada wa mawazo juu ya hili.
Asanteni kwa mchango wenu.
Kisheria hapo huna aja ya kurudisha mahali kwa kuwa umeshamzalia mtoto mmoja so kama unaendelea na maisha yako ya mahusiano mengine aina shida kwa maoni yangu
 
Yaani nitulie nimsubiri afomart upya ubongo wake kisa kaniacha bila sababu?? Niendelee kumbembeleza sababu naogopa kuwa single maza?? Mimi mtoto wangu ni zawadi yangu kama baba aliamua kuondoka aende na mimi pia maisha yaendelee aisee
Sikulaumu dada yangu hata mm haya yalinikuta nilisema kama wewe miezi ya mwanzoni ya kutengena ila baadae akili ilipokaa vizuri ndio nikaanza kukumbuka nakuelewa ujinga tuliofanya, wakati uo itakuwa too late ,cha msingi tulia ufumbuzi utapatikana uwezi jua atakuja mwenyewe kukwambia mama tusameheane ilikuwa ni hasira tu ,sawa labda kama umpendi tena lakini hii ni vyema ukamsikilizia ameenda kujipangaje, unaweza kuta kapata mchepuko wa muda anamzuzua
 
Hivi unajielewa kweli!!!?

Yani wewe ndo tatizo na wewe mwenyewe ndo unataka suluhisha tatizo...
Wewe si ndo unaetaka kumuacha!?? Ok alikukataza uende kwenu...ukaenda kibabe...ulitegemea urudi akuchekee...!!?

Anajua tabia ya familia yako ndio maana alipokuweka ndani akataka uwe nao mbali..

Nyie wabena kwanza wengi ni washirikina jeuri na viburi.

Jishushe kwa mzazi mwenzio na uombe msamaha. Huo upumbavu ea kutaka rudisha mahari utakuwa umeshauriw na ndugu zako ndio maana jamaa alitaka ukae nao mbali.
Acha ujinga hutaolewa na Mama yako.
Hapa ndio mwarubaini nadhani ulikuwa akilini mwangu ,Dada mtoa mada ,ukisoma hapa naamini %100 jamaa kakugusa utakataa lakini ndivyo hvyo ,sasa jitafakari anagalia ni nini ulichokosea maana kama jamaa alikataa wewe kurudi kwenu alafu ukarudi kwa lazima hapo ni kumkosea heshima na hapo ndio uliloga
 
Pole. Hujitambui wewe ni nani na uko wapi. Wewe ni mke wa mtu na umemzalia
toto zuri. hili neno litakughalimu maisha yako yote. rudi mkajenge ndoa yenu. Ndoa zote ziko hivyo. Usione wamevaa vizuri ukadhani ndoa yao ni pilau na soda. Kuna zaidi ya sherehe.
 
Mleta Mada anaponichosha ni anopesema huyo mwanamme alimuacha bila kosa!
At the same time nasema chanzo cha hayo yote ni kulazimisha kurudi kwao baada ya kutoka ukweni kujifungua.


Sasa mleta maada kwanini uliondoka kurudi kwenu kibabe Huku mmeo hataki?.
Alafu ET unajiona huna kosa na baadhi ya wanawake walioshindwa na maisha humu wanakushauri ujinga.

Ushauri kaa tulia uongee nae najua tatizo anakuona wewe ni kiburi, jeuri na unawasikiliza wazazi kuliko yeye mmeo.
Wazazi muhmu lkn tambua huyo tayari mmeo.
 
Sababu za kutengana niliwahi kuweka uzi hapa...ni kwamba alitoa mahari wakati nina ujauzito wakasema inabidi nikajifungue chini ya mama mkwe. Baada ya kujifungua mtoto akafika miezi 4 ikabidi nirudi nyumbani mwanzoni alinikubalia nikakata hadi tiketi kabisa. Mama yake akamkatalia nisiondoke ndio akaniambia nikiondoka kwenda kwetu niondoke moja kwa moja. hiyo ndio sababu ya kutengana nilirudi nyumbani
Kwa nini ulirud nyumbani bila maridhiano, kwanza.. Kulikuwa na sababu ipi ya kurudi nyumbani mapema hivyo?

Je tofauti na hilo, unaona kulikuwa kuna matatizo mengine ya kimahusiano?

Wakati mwingine ni lazima kupima uzito wa tatizo, kwa kawaida sisi wanaume tunapenda kuona wake zetu wanatutii...

Kikubwa anaitaji ujifunze na wewe kutaka kurudisha mahari ndiyo unachochea kuharibu ndoa yako.

Asikudanganye mtu jitahidi kuweka mambo sawa. Si rahisi kudumu katika mahusiano mengine zaidi utakuja kuwa single mother na kuzalishwa kwa mara nyingine na kuachwa.
 
 
Kwa mini mmetengana? Ni uleule ugomvi wa kutaka kurudi kwenu na yeye anataka ukae kwao? Whatever the reason Pole sana mdogo wangu. Inawezekana mwenzio bado anajitafakari whether mnaachana moja kwa moja au mnaweza kuendelea na mahusiano yenu mlee mtoto. Na wewe nakushauri utulie kwanza usikilizie usifanye haraka kuingia kwenye mahusiano mapya kwanza mtoto bado mdogo huyo. Yaani nisivyopenda watu waliozaa pamoja kutengana basi tu
Rafiki una Roho nzuri sana. Ila hujamfikia rafiki yangu
 

Nilichogundua Sababu Ya Jamaa Kukataa Kuchukua Mahali Ni Hasira Zilizo Sababishwa Na Wazazi Wako Baada Ya Kukulazimisha Kurudi Kwenu Kinguvu.
 
Mkuu nimejaribu sana kusuluhisha lakini baba mtoto hajakubali kabisa mpaka nikamuuliza kosa langu ni kurudi nyumbani au kuna lingine nijue hana jibu. Unajua wakati mwingine huwezi jua Mungu anatuepushia nini katika maisha yetu
Inaonekana kwa kurudi kwenu bila yeye kuridhia ndo sababu kubwa(umeonyesha kiburi tena kikubwa sana) utii kwa Mumeo ni kitu kikubwa sana...wewe umetunisha msuli ukasafiri bila yeye kupenda...kwa hilo ulitakiwa kuwa mnyenyekevu na kukubali kuwa umekosa...wewe inaonekana bado unajiona una haki ya kufanya utakalo na mume wako akubali unavyotaka....Why ulienda nyumbani bila ruhusa yake??? Why japo mtoto ni bado mdogo mno .na ni miezi 2 tu toka mwachane unafikiria new mahusiano?? Je una mtu kichwani mwako tayari??? mna muda gani na huyu new mume mtarajiwa tena??? Nimesoma majibu yako kwa members wengine... na kuona kuwa wewe una kiburi,jeuri na mbabe ktk haya mahusiano na una tabia ya kiburi....jitafakari na ikiwezekana kaa mwenyewe walau miaka 3 ukiwa unalea mtoto wako...achana na fikra za kuanza mahusiano mapya itakucost
 
Sababu ni ile ile ya kurudi nyumbani. Asante sana nimeshapoa na tumekubaliana tutalea tuu mtoto pamoja. Najua hatutaweza kuwa pamoja tena sababu yeye anasema siku niliyoondoka ndio nae alivunja mahusiano moja kwa moja .

Hiyo picha ni yako? Kama ndiyo naomba swala la kurudisha mahari uniachie mimi
 
Wewe mpaka mtoto umezaa halafu unataka kurudisha mahari??? Yaani midhari ameshakuchokonoa huko chini hiyo mahari haipaswi kurudishwa
 
Mmetengana miezi 3 iliyopita,mtoto ana miezi 7 tayari unawaza kuchumbiwa!?? Aisee kweli maisha yanakwenda kasi sana!!
 
Mahari inaletwa na mshenga, ambae huzungumza na mwakilishi wa familia. Waeleze wazazi na uwaache wamalizane na hao washenga. Usijiingize kwenye kutaka kumrudishia mahari kama vile unamrudishia simu.

Endelea na maisha yako. Siku akikukuta na mtu mwingine nayo itakua kigezo kizuri cha yeye kwenda kudai mahari yake kama anataka.
 
Dada ngoja nikuambie kwamba wewe hata kama kuna shida mahali hupaswi kureact jinsi unavyoreact sasa, unataka mahali irudishwe? Kwa minajili ipi, wewe unasababisha uonekane mkorofi na usiye na busara, hata kwa baadhi ya majibu yako ya humu ndani, hata kama unasema huna shida, trust me una kashida mahali, rekebisha mwenendo wako utaenda na mumeo sawa
 
Eti 'mimi ni mvumilivu'

Miezi mitatu tu unataka kurudisha mahari!!!!!!!!!!!! Alafu unajiita mvumilivu....mvumilivu my foot.
Kweny masuala ya mahusiano jitahid sana kutatua changamoto zako bila kusikiliza watu wengine wanasema nini hata kama ni wazazi.
Nyie wabena, wasangu, wahehe kweny mahusiano mna kawaida ya kusikiliza nyumban wamesemaje, yani baba au mama kasema nini na sio kile kilichopo akilini mwenu.
Eti baba na mama wanasema najibembeleza sana kwa uyo mwanaume...aiseee!!!!
Sasa walitaka ujibembeleze kwa nan? Wenzako ndoa wanazipigania miaka wewe miezi mitatu tu chaliiii eti umechoka.
We sema tu kuwa umeshapata mtu mwengine ndan ya mda mfupi now unataka maoni ya wadau ili moyo wako upate aman wakat unajua sio sawa.
Kabla ya yote jiulize kwanini ataki kuchukua mahari yake??? .......Ni kwa sababu anajua tayari mna mtoto na kipaumbele chake ni mtoto sio wewe hivyo haoni haja kuchukua mahari ila wewe unajistukia mana tayari unataka kuleta ingizo jipya wakati jamaa amekaa kmyaaaa anakusoma tu.
mkuu yeye ndio aliniacha na miezi 3 imeshapita toka tumetengana ndio maana. Mimi asili yangu sina kiburi na ni mvumilivu sana aisee
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom