Kuachana/kutengana kwa wazazi mkiwa tayari mna mtoto/watoto ni ubinafsi.
Kama wote mngeweka ubinafsi pembeni na kumfikiria mtoto wenu mdogo (ndo kwanza miezi saba) hakika mngeyasuluhisha na maisha yaendelee.
Fikiria mtoto anaenda kulelewa na mzazi mmoja, atakuwa na malezi gani? Atafikiaje malengo yake ukubwani? Atakuwa mtoto wa aina gani? Kwa nini mnamkatili mtoto haki yake ya msingi ya kulelewa na wazazi wote wawili kwa upendo?
Mnaanza kumjengea mazingira magumu ya ukuaji kwa kujifikiria nyinyi (ubinafsi) aje alelewe na mzazi wa kambo, apate mateso, akue kwa shida na taabu nyingi, akose elimu bora, upendo wa wazazi kisa tu nyie mnashindwa kutatua matatizo yenu? Ni kweli hayatayuliki na mkaendelea kupendana na kulea mtoto wenu?
Hebu mfikirieni huyo malaika kwanza kabla hamjarudishiana mahali