Hataki kuchukua mahari yake nifanyeje??

Hataki kuchukua mahari yake nifanyeje??

Status
Not open for further replies.

trudie

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
4,546
Reaction score
11,134
Habari wanajf na heri ya pasaka.

Niende kwenye lengo la uzi...mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miezi 7 nina miaka 26. Miezi 3 iliyopita nilitengena na mzazi mwenzangu ambaye alishanitolea mahari na kunivalisha pete ya uchumba kwa sasa nipo nyumbani na mtoto wangu.

Mwanzoni nilipata wakati mgumu sana kukubali kwamba tumetengana lakini namshukuru Mungu sasa hivi nimekubaliana na hali na nipo vizuri kabisa.

Baba mtoto wangu alikataa kabisa kuchukua mahari yao na pia kuwashirikisha wazazi juu ya kutengana kwetu kwa madai tulikutana wawili tuu wakati pete tulivalishana mbele ya wazazi na ndugu wa pande zote.

Swali langu ni je naweza kuingia kwenye mahusiano mapya wakati yeye hajachukua mahari yake? Na je kwa mfano mtu akataka kuja kutoa mahari inakuwaje kuhusu mahari yao ya mwanzo haitakuwa na shida yoyote maana hataki kuchukua kabisa na watu wanasema kubaki na mahari yake itanifunga sababu kimila bado nitakuwa mke wake.

Ninachohofu mbeleni asije leta shida akasema ni mchumba wake halali sababu temetengana kienyeji sana. Naombeni msaada wa mawazo juu ya hili.

Asanteni kwa mchango wenu.
 
Kwa mini mmetengana? Ni uleule ugomvi wa kutaka kurudi kwenu na yeye anataka ukae kwao? Whatever the reason Pole sana mdogo wangu. Inawezekana mwenzio bado anajitafakari whether mnaachana moja kwa moja au mnaweza kuendelea na mahusiano yenu mlee mtoto. Na wewe nakushauri utulie kwanza usikilizie usifanye haraka kuingia kwenye mahusiano mapya kwanza mtoto bado mdogo huyo. Yaani nisivyopenda watu waliozaa pamoja kutengana basi tu
 
mahari ilipokelewa na ndugu na wazazi wote
Washirikishe ndugu na wazazi wa upande wako juu ya kuvunjika kwa uhusiano wenu alafu mtamtafuta mwanasheria inacordance to customary laws atawapa utaratibu wa kurudisha hiyo mahari.
 
Mmeachana miezi 3 tu unataka kuingia kwenye mahusiano mapya? Haraka ya nini dia? Mbona ni muda mfupi sana....tulia tuloza akili yako kwanza ulee mwanao.
 
Sababu ni ile ile ya kurudi nyumbani. Asante sana nimeshapoa na tumekubaliana tutalea tuu mtoto pamoja. Najua hatutaweza kuwa pamoja tena sababu yeye anasema siku niliyoondoka ndio nae alivunja mahusiano moja kwa moja .
Kwa mini mmetengana? Ni uleule ugomvi wa kutaka kurudi kwenu na yeye anataka ukae kwao? Whatever the reason Pole sana mdogo wangu. Inawezekana mwenzio bado anajitafakari whether mnaachana moja kwa moja au mnaweza kuendelea na mahusiano yenu mlee mtoto. Na wewe nakushauri utulie kwanza usikilizie usifanye haraka kuingia kwenye mahusiano mapya kwanza mtoto bado mdogo huyo. Yaani nisivyopenda watu waliozaa pamoja kutengana basi tu
 
Wewe mama embu lea mwanao ndiyo kwanza ana miezi saba ushafikiria dushe la mwanaume mwingine kwann usitulie na kulea mwanao
Hivi mkuu umeelewa swali hapo wapi nimesema nafikiria dushe la mwanaume mwingine?? Swali langu ni mahari yake anayokataa kuchukua haitakuwa na effect baadae kama nitakuwa na mahusiano au mtu atataka kutoa mahari....Halafu kulea mtoto na dushe hakuna uhusiano maana unaruhusiwa baada ya siku arobaini tuu akishazaliwa
 
Washirikishe ndugu na wazazi wa upande wako juu ya kuvunjika kwa uhusiano wenu alafu mtamtafuta mwanasheria inacordance to customary laws atawapa utaratibu wa kurudisha hiyo mahari.
asante kwa ushauri
 
Pete mlivalishana mbele ya ndugu zake... mahari ina utaratibu wake wa kupeana...

Cc: mahondaw
 
Mmeachana miezi 3 tu unataka kuingia kwenye mahusiano mapya? Haraka ya nini dia? Mbona ni muda mfupi sana....tulia tuloza akili yako kwanza ulee mwanao.
Swali ni kuhusu madhara ya kubaki na mahari yake asiyoitaka kama nitakuwa na mahusiano mengine au pia kutoa mahari tena....sio kwamba nnataka kuingia. Nimeuliza sababu ndugu wanasema mahari hiyo itanifunga sitaweza kuendelea mbele kama itabaki sababu ni mke wake kimila
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom