Hataki kuchukua mahari yake nifanyeje??

Hataki kuchukua mahari yake nifanyeje??

Status
Not open for further replies.
Muwe na huruma mtoto miezi saba mmetengana miezi mitatu tayari unafikiria kupokea mahari ya wengine hapo hesabu za kawaida we ndo ulivunja mahusiano....kwa nini usifikirie kuwa amekupa muda ujitafakari??
 
Wewe ni mwanamke malaya... Ndoa si stahili yako.

Na huyo mwanaume unayehisi ni bora..unaenda kanyaga moto. POLE SANA.
Hee yamekuwa hayo?? Hivi kweli huwa mnasoma na kuelewa mtu alichoandika??
 
Mkuu naomba usome vizuri swali langu. sio kwamba nnapokea mahari nyingine....nahitaji kujua jee kubaki na mahari yake haitakuwa na madahara kwa baadae
Muwe na huruma mtoto miezi saba mmetengana miezi mitatu tayari unafikiria kupokea mahari ya wengine hapo hesabu za kawaida we ndo ulivunja mahusiano....kwa nini usifikirie kuwa amekupa muda ujitafakari??
 
olewa tu ila weka mahari ya watu pembeni, ili siku akija unamtuliza na mahari mlangoni.
 
Kwani wapi hajaeleweka mleta mada kajipambanua jinsi alivyo!
Kuna sehemu kasema anapokea mahari au swali lilikuwa hataleta shida baadae sababu uchumba haujavunjwa wala kurudisha mahari?? Anyway yeye ndio aliyevunja uchumba
 
Umeshapata anae kudanganya Yule alie kutolea mahari na pete kukuvalisha una mdharau?
 
Umeshapata anae kudanganya Yule alie kutolea mahari na pete kukuvalisha una mdharau?
aliyenitolea mahari ndie alivunja uhusiano. Nadhani watu wengi huwa hawasomi mada wakelewa wanakimbilia kucoment. Sababu nimeuliza madhara ya kukaa na mahari yake haina shida kwa baadae coment nyingi zinashutumu nakimbilia kuolewa
 
Mmeachana miezi 3 tu unataka kuingia kwenye mahusiano mapya? Haraka ya nini dia? Mbona ni muda mfupi sana....tulia tuloza akili yako kwanza ulee mwanao.
Yawezwkana alichepuka huyu Dada ndio maana wakaachana sio kqa haraka hip ya kutaka kuingia mahusiano mapya
 
Utaratibu unasema hivi kama kakuacha yeye hakirudi kitu ila kama unamwacha wewe kisa umepata new comer rudisha ili mwenzio akatafutie sehemu nyingine
 
Washirikishe watu wa dini kama ni msikitini au kanisani kuhusu kujua hili la kukufanyia fujo baadaye, “Huyu ni mchumba wangu halali nimezaa naye na mahari nimemtolea”

Mtoto alishalipa hela ya uchafuzi maana mahari alitoa kipindi nina ujauzito. Mimi nahitaji kujua je kubaki na mahari yake haitaleta shida?? na vile hataki tuvunje uchumba mbeleni hawezi kuleta shida kwamba huyu ni mchumba wangu halali??
 
Unataka kwenda kuanza ndoa nyinginge wakati na Handcap +1??
 
Yawezwkana alichepuka huyu Dada ndio maana wakaachana sio kqa haraka hip ya kutaka kuingia mahusiano mapya
Matatizo ya watanzania hawasomi wakaelewa kabisa. Wapi nimesema nimeingia au ninaingia kwenye mahusiano mapya?? swali lilikuwa je kubaki na mahari yake haina shida kama kutakuwa na mtu atataka kutoa mahari kwa baadae? Sikuchepuka wala sina hiyo tabia aliniacha kwa sababu hakutaka nirudi kwetu baada ya kujifungua.
 
Utaratibu unasema hivi kama kakuacha yeye hakirudi kitu ila kama unamwacha wewe kisa umepata new comer rudisha ili mwenzio akatafutie sehemu nyingine
Yeye ndie alieniacha. Mimi kinachonipa woga ni pia hataki tushirikishe wazazi kuhusu kuachana kwetu while pete tulivalishana mbele yao je hawezi kuleta shida baadae akidai ni mchumba wake halali??
 
Mama wewe kwanza fikiria kulea mwanao ndiyo kwanza ana miezi saba hayo mambo ya mahari kwa sasa achana nayo utayafikiria walau mwanao akiwa na miaka minne au sita mkuu
Hasira hizo ndo wanakwake wanakimbilia huko! Wanadhani wanamkomoa mwanaume?
Ndo maana anasema akitokea mwanaume mwingine akitoa mahari hakuna shida?

Mwambie ukishapigwa mhuri "kuzalishwa" uwezekano wa kuolewa lazima utumie mbinu za kujeshi
 
Matatizo ya watanzania hawasomi wakaelewa kabisa. Wapi nimesema nimeingia au ninaingia kwenye mahusiano mapya?? swali lilikuwa je kubaki na mahari yake haina shida kama kutakuwa na mtu atataka kutoa mahari kwa baadae? Sikuchepuka wala sina hiyo tabia aliniacha kwa sababu hakutaka nirudi kwetu baada ya kujifungua.
Kama hauko kwenye mahusiano mapya tulia basi haraka ya nini?

Usikute jamaa bado anajifikiria hasa mtoto wake .

Unataka uachane nae saivi halafu baadae uje kuleta vilio vya kisingo maza hapa wakati mambo umeyataka mwenyewe .

We tulia jamaa ubongo uformat upya aanze kukuona malaika .

Ni mtazamo tu
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom