Hataki kuchukua mahari yake nifanyeje??

Hataki kuchukua mahari yake nifanyeje??

Status
Not open for further replies.
Mmevalishan mbele ya wazazi ndugu..mkazaa sa hv mnatengana kwa sababu ambazo naona dah...ila jamaa hana cha kupoteza itakuwa ashahesabu mtoto anaye anahudumi....kuzaa kwemye uchumba nayo ni challenge sana..au bila ndoa
Hivi watu wa Iringa Njombe unawajua vizuri...
Yani huo mkakati wa kurejesha mahari umejadiliwa na ukoo.. Kifupi hapo Mangi akikubali kupokea mahari ndo mtoto haji kumuona maisha.. Na anaitwa jina la huko kwao mwanamke.
 
Kwa hiyo ulirudi nyumbani ili afuate utaratibu wa kufunga nawe ndoa?
Ilikuwa moja ya sababu kwani April hii ilibidi tubariki lakini sababu kubwa ni changamoto nilizopata baada ya kujifungua na kukosa uangalizi wa karibu hasa na zile homa baada ya uzazi huku nashinda njaa sina wa kunipikia
 
Kwa hiyo unataka kusema ulipoenda kwa mamamkwe hawakuweza kukuangalia vizuri kihuduma? Ukaamua urudi kwenu?

Jamaa anakipato? Alikuwa hatumi pesa na kuja kukuangalia?
 
Alinikubalia nirudi nyumbani lakini mama yake aliposikia akamlazimisha niende kwao Moshi na yeye wakati procedure za kwenda nyumbani zimekamilika. Nikamwomba tusogeze mbele kwenda Moshi kwakuwa ametaka ghafla ndipo mama yake alipokasirika. Na yeye akabadilika akawa hataki niondoke na akasema nikiondoka niende moja kwa moja
Inshort kuna mambo yaliyonilazimisha kwa kipindi kile nirudi nyumbani na mwenza wangu anamsikiliza sana mama yake hata kitu mkikubaliana wawili anamshirikisha mama akikataa basi na yeye anakubali tuu hadi mambo personal.
Mfano mzuri tulitaka kubadilisha dada wa kwazi sababu alikuwa ana mambo ya wanaume sana asingeweza kulea mtoto tukakubaliana na mwenzangu nikamwomba mama yangu atutafutie akampata kabisa ikabaki kumwagiza aje tunapokaa.Mwenzangu alipomshirikisha mama yake akakataa tusibadilishe nae akakubali kumbuka alishafatutwa mpya.
Je hakufukiria mtoto wake ataishije na dada anayeshinda kwa wanaume pale sisi tutakapoenda kazini? Hajui madhara yake?
Hii ndio sababu iliyo sababisha mtengane.Ili mahusiano ya dumu lazima mkubali mmoja kujishusha pale inapotokea mgogoro hakuna mkamilifu utaacha wangapi dada?
 
Kwa hiyo unataka kusema ulipoenda kwa mamamkwe hawakuweza kukuangalia vizuri kihuduma? Ukaamua urudi kwenu?

Jamaa anakipato? Alikuwa hatumi pesa na kuja kukuangalia?
Mama mkwe alikuja tunapoishi sisi ingawa na yeye anaishi hapo hapo mara moja moja. Lakini aliondoka wiki ya 2 tu nilivyojifungua nikabaki na dada wa kazi na mwenza wangu ambae anaondoka asubuhi anarudi usiku sababu ya kazi zake.
 
Ilikuwa moja ya sababu kwani April hii ilibidi tubariki lakini sababu kubwa ni changamoto nilizopata baada ya kujifungua na kukosa uangalizi wa karibu hasa na zile homa baada ya uzazi huku nashinda njaa sina wa kunipikia
Ulijifungua kwa njia ya kawaida au operashen
 
Nimejishusha sana kwa miezi 2 mfululizo lakini yeye alishaamua influence pia zinamcost haangalii familia yake
Hii ndio sababu iliyo sababisha mtengane.Ili mahusiano ya dumu lazima mkubali mmoja kujishusha pale inapotokea mgogoro hakuna mkamilifu utaacha wangapi dada?
 
Mama mkwe alikuja tunapoishi sisi ingawa na yeye anaishi hapo hapo mara moja moja. Lakini aliondoka wiki ya 2 tu nilivyojifungua nikabaki na dada wa kazi na mwenza wangu ambae anaondoka asubuhi anarudi usiku sababu ya kazi zake.
Sawa sawa... alitakiwa hata akae week 5 hapo ni kosa.

Haujanijibu kuhusu matumizi. Umesema ulishinda njaa. Alishindwa kukuhudumia?
 
Nimejishusha sana kwa miezi 2 mfululizo lakini yeye alishaamua influence pia zinamcost haangalii familia yake
Haangalii familia yake una maanisha haudumii mahitaji hapo nyumbani? Je mama yako mkwe alipo ondoka hapo nyumbani ulibaki na nani?
 
Mrudishie mshenga wake au wazazi wake full stop...
 
Sababu za kutengana niliwahi kuweka uzi hapa...ni kwamba alitoa mahari wakati nina ujauzito wakasema inabidi nikajifungue chini ya mama mkwe. Baada ya kujifungua mtoto akafika miezi 4 ikabidi nirudi nyumbani mwanzoni alinikubalia nikakata hadi tiketi kabisa. Mama yake akamkatalia nisiondoke ndio akaniambia nikiondoka kwenda kwetu niondoke moja kwa moja. hiyo ndio sababu ya kutengana nilirudi nyumbani
ni kwamba mama mkwe ulikuwa hupatani nae au ni nini hasa?!!...haingii akilini utake kurudi tena kwenu bado kuna kitu hujakiweka sawa.

kwa ufahamu wng wa haraka haraka kuna uwezekano mlitofautiana kimtazamamo na mama mkwe na huenda mume wako alishinikizwa na wazazi wake akuache kwa kosa la wewe kuondoka kwa mama mkwe ...ni kama hukuwa na utii kwao kwa kile walichokuonya

pili .....nahisi jamaa bado anatathmini sana juu ya maamuzi aliyoyaamua maana kama kweli aliamua kukuacha haiwezekani iwe ngumu kuchukua mahari yake

tatu...acha kumjibu kwa kiburi na jeuri kama bado mnaongea nae maana nahisi na wewe unataka kumkomoa kutokana kuachwa kwako hii ni kwa mujibu ya baadhi ya maelezo yako sina haja ya kuyaquote
 
Sawa sawa... alitakiwa hata akae week 5 hapo ni kosa.

Haujanijibu kuhusu matumizi. Umesema ulishinda njaa. Alishindwa kukuhudumia?
Mbona nimesema mkuu kwamba nilibaki na dada wa kazi ambae alikuwa mambo mengi hashindi nyumbani kwahyo sina mtu wa kuagiza hata aninunulie vya kupika nikapika mwenyewe au akipika anapika kibichi. Matumizi alikuwa anatoa lakini siwezi kwenda sokoni wiki ya pili tuu. Kwahyo unakaa njaa umsubiri amalize mambo yake akirudi ndio akakukelee vitu vya kupika
 
Hata mimi pia sijapoteza kitu mkuu sababu mtoto wangu ni zawadi nzuri sana na sijutii kumzaa ananipa furaha sana. Mengine Mungu anapanga mwenyewe.
Sio mtoto wangu ni mtoto wenu acha ubinafsi bidada
 
Haangalii familia yake una maanisha haudumii mahitaji hapo nyumbani? Je mama yako mkwe alipo ondoka hapo nyumbani ulibaki na nani?
Kusema haangalii familia yake namaanisha future ya mtoto wake . Alipoondoka nilibaki na dada wa kazi na yeye baba mtoto
 
Hapana sikuwahi kutofautiana nae mama mkwe wala kugombana nae. Labda kama kibinadamu unamkosea bila kujua
Mkuu Kuna swali nimemuuliza kuhusu mama yake mkwe haja nijibu.
 
Mbona nimesema mkuu kwamba nilibaki na dada wa kazi ambae alikuwa mambo mengi hashindi nyumbani kwahyo sina mtu wa kuagiza hata aninunulie vya kupika nikapika mwenyewe au akipika anapika kibichi. Matumizi alikuwa anatoa lakini siwezi kwenda sokoni wiki ya pili tuu. Kwahyo unakaa njaa umsubiri amalize mambo yake akirudi ndio akakukelee vitu vya kupika
Hukuyasema ndiyo umeyasema sasa. Unaonekana umechoka pole, bila shaka hawa wanaJF wamekuchosha usiku kucha.

Ok kwa hiyo vikubwa vilivyokupeleka nyumbani ni.

1. Huduma mbovu na kutojaliwa ukweni.
2. Unataka utaratibu mpya wa ndoa.

Lakini, ulishayazungumza na mwenza wako kuhusu haya mambo kwa undani? Naposema kuzungumza sio kule kulalamika.

Hapana ni kutafuta sehemu tulivu ukamtajia moja baada ya jingine kisha mkaja kwenye suluhu. Hili ulipaswa ulifanye kabla ya kurudi kwenu lakini unaweza kulifanya pia.

Usiniambie ulishajibu hili kule juu, nijibu.

Yeye anasemaje kuhusu situation nzima? Msimamo wake.
 
Kusema haangalii familia yake namaanisha future ya mtoto wake . Alipoondoka nilibaki na dada wa kazi na yeye baba mtoto
Ushauri wangu kwako kwa Sasa tulia usichukue maamuzi ya kuludisha mahari, pole kwa yaliyo kutokea.
 
Sio mtoto wangu ni mtoto wenu acha ubinafsi bidada
Ohoo...
Nishasema jeuri huyu... Na mchaga jeuri za kifamba ka hizi hawezi vumilia.

Hawa watu wa Njombe huwa wanaona wao kwa wao tu... Wana mambo yao flani hivi kama si kabila lao huezi waelewa.

Mchaga na Mbena its the hellest combination I have ever seen. Basi tu kwa vile wana mtoto ila ingekuwa bora waachane tu.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom