Hata Tundu Lissu hawezi shinda kesi ya Bil 260 ICSID. Wanaohusika na kuingia mikataba mibovu wanyongwe

Issue sio kushindwa,jinsi unavyoshindwa pamoja na kuwa kote ni kushindwa
 
Mbona pale kesi ni rahisi nyie kushindwa.

Kwanini mliwatoa RL wakati mngewaachia ilikuwa inaisha mwaka huu kama walikuwa hawajaanza uzalishaji?
Mbunge Matayo David Phd, mkurugenzi wa Ramani investment alikuwa anazivizia hizo Retention Licence ili apewe bure au azinunue kwa bei ya kutupwa then aite watu wale wale kuja kuziwekeza.

Pia hizo RL zilitolewa kwenye tender kuwa zinauzwa ni nani alizinunua haijulikani? Je zilinunuliwa haijulikani?

Kesi inaendeshwa Doto waziri wa madini yeye yuko kimyaaa kumbe kashaxiuza RL huku kuna mafaini ya mabilioni?
CCM ni shida .

Soma Hapa:-👇

Dodoma. Serikali imefuta leseni zote za kuhodhi maeneo ya madini na wamiliki wake wametakiwa kuomba upya wakizingatia Sheria ya Madini na kanuni zake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Mei 11, 2018 Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini, Profesa Idris Kikula amesema tangazo la Serikali namba moja la mwaka 2018 limesema maeneo yote yaliyopewa leseni yanarejeshwa serikalini bila hakikisho la kupewa tena.

Amesema uamuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ikisomwa na marekebisho yake ya mwaka 2017 na kanuni ya 21 ya kanuni za Madini (Haki Madini za mwaka huu).

Amesema leseni zilizofutwa na wamiliki wake wanatakiwa kuomba tena zinazihusu kampuni 11, kwamba leseni hizo zinajumuisha migodi ya kati na mikubwa.

Migodi hiyo ni pamoja na Kabanga Nickel Company Limited, National Mineral Development Corporation Limited, Bafex Tanzania Limited ambayo inamiliki leseni za maeneo matatu.

Nyingine ni Mabangu Mining Limited, Resolute (Tanzania) Limited, Wigu Hill Mining Company Limited, Nachingwea Nickel Limited na Precious Metals Refinery Company Limited.

Chanzo: Mwananchi ( May 11,2018)

Soma Hapa:-👇👇👇
Tume ya Madiniimetangaza zabuni kwa ajili ya ununuzi wa maeneo10 yenye leseni hodhi za madinina yenye ukubwa wa kilomita za mraba 381.89 yaliyopo katika maeneo ya Ngara – Kagera, Kahama- Shinyanga, Chunya- Mbeya, Bariadi na Busega – Simiyu, Morogoro, Nachingwea – Lindi ambayo awali leseni hodhi zake zilikuwa zimerudishwa Serikalini.

Uamuzi huo umetangazwa leo tarehe 19 Desemba, 2019 na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula kupitia mkutano wake na waandishi wa habariuliofanyikajijini Dodoma na kuhudhuriwa na Kamishna wa Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya pamoja na watendaji wengine wa Tume ya Madini.

Profesa Kilula alifafanua kuwa, awali mwaka 2017 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha marekebisho ya Sheria ya Madini Sura Namba 123 na kanuni zake ambapopamoja na mambo mengine, zilizokuwa lesenihodhi za madini ( retention licence) zilirudishwaSerikalini

Alisema baada ya marekebisho hayo maeneo yote 10 yenye ukubwa wa kilomita za mraba 381.89 yalirudishwa Serikalini na kuongeza kuwa, wachimbaji wa madini wengi wamekuwa wakiulizia maeneo hayo mara kwa mara lengo likiwa ni kuomba leseni za uchimbaji madini.

Aliendelea kusema kuwa, baada ya uchambuzi wa kina kufanyika, Serikali kupitiaTume ya Madini, maeneo yote 10 yaliyokuwa na leseni hodhi yatatolewa kwa zabuni na kukaribisha kampuni za uchimbaji wa madini na watu binafsiwenye uwezo wa fedha na utaalam katika miradi ya uchimbaji wa madinina wenye nia ya kuendeleza miradi ya madini ya nickel, dhahabu na rare earth elements kuomba zabuni hizo.

Aliongeza kuwa, mwekezaji atakayeonesha nia ya kuwekeza katika maeneo hayo atakuwa na jukumu la kufanya kazi na kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini.

Wakati huo huo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akielezea hatua zinazochukuliwa kwa wamiliki wa leseniwasioendeleza maeneo yao, aliwataka wamilikina waombaji wote wa leseniza utafutaji na uchimbaji wa madiniwenye mapungufu kurekebisha mapungufuhayo ndani ya siku 30 kuanzia sasa..

Alifafanua mapungufu hayo kuwa ni pamoja na leseni ambazo hazifanyiwi kazi, leseni ambazo hazijalipiwa ada ya pango la mwaka, maombi ambayo hayajalipiwa ada ya maombi na maombi yaliyokosa viambatisho muhimu kwa mujibu wa sheria.

Profesa Manya alitaja mapungufu mengine kuwa ni pamoja na waombaji waliokidhi vigezo vya kupewa leseni lakini hawajalipa ada ya maandalizi na wamiliki ambao leseni zao zimeshatolewa lakini hazijachukuliwa.

Alifafanua kuwa mpaka sasa leseni zaidi ya 134 za utafutaji na uchimbaji wa kati wa madini hazijachukuliwa na zaidi ya maombi 450 ya leseni za utafutaji yana mapungufu.

Akielezea hatua zitakazochukuliwa kwa kampuni au watu binafsi walioaminiwa na Serikali na kupewa leseni lakini wameshindwa kutekeleza masharti ya leseni kwa mujibu wa Sheria ya Madini, alisema leseni ambazo hazijalipiwa ada ya pango kwa mwaka, leseni ambazo hazifanyiwi kazi na leseni ambazo zimekwishatolewa lakini hazijachukuliwa zitaandikiwa hati ya makosa na yasiporekebishwa zitafutwa kwa mujibu wa sheria.

Aidha alisema kuwa, maombi yote ya leseni za utafutaji na uchimbaji wa kati yenye mapungufu yataondolewa kwenye mfumo wa utoaji wa leseni ili waombaji wengine wenye sifa pamoja na wachimbaji wadogo waweze kuomba maeneo hayo.

Aliendelea kusema kuwa, maombi ambayo yamekidhi vigezo vya kupewa leseni lakini hayajalipiwa ada ya kuandalia leseni yataondolewa kwenye mfumo ili waombaji wengine wenye sifa waweze kuomba maeneo hayo.

Alisisitiza kuwa tangazo la zabuni husika linapatikana katika tovuti ya Wizara ya Madini ambayo ni (www.madini.go.tz)Tume ya Madini (www.tumemadini.go.tz) magazeti ya Habari Leo na Daily News ya tarehe 20 Desemba, 2019 pamoja na blogs na mitandao ya kijamii.
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Hivi ni nani akipewa Bil 2 kati ya hizo bil 260 atasimama imara kutetea taifa letu? Hata Tundu Lissu pamoja na Uzalendo wake hawezi shinda.

Tumeshuhudia mlolongo wa kesi nyingi serikali ikishindwa hata mahakama za hapa kwetu.

Mtu anaelipwa chini ya 5M akasimamie kesi ya billions unategemea nini?

Suluhisho la haya mambo ni tushughulike huku kwetu hasa tunapoingia mikataba na tenda mtu akiingi mkataba mbovu ni anyongwe tu awe mfano maana hizo pesa zinazopotea zingeweza okoa maisha ya Watanzania wengi.

Na Watanzania tufunguke mtu kaingia mkataba mbovu 2013 /2014 unakuja unavunjwa 2017 analaumiwa alievunja alie ingia katulia anaejoy life, tuko serious kweli?

Tuanze na KIKWETE Kumnyonga
 
Hakuna njia yoyote hao jamaa watashinda kesi hito ya mchongo.Hiyo kampuni haijasajiliwa wala kufanya investment yiyote Tanzania.siyo kampuni ambayo iliingia mikataba na nchi yetu.Wahusika wala sio raia wa Canada....wanachokifanya kwa kushirikiana na watz wasio waaminfu kutengeneza kesi kwa kutumia makampuni yaliyowahi kuja kuwekeza hapa nchini. Muhimu pia kuweka clip ya respondent mkajua serikali imejibu kitu gani katika hii kesi ya kubumba.
 
Kuna mambo yanatia hasira sana
Kwa sababu tunampa mtu yeyote uongozi bila kujali elimu, uwezo, uaminifu, uwezo na uzoefu.

Akiwa bibi mpe !!!! Tutaenda naye akiuza Tanapa tunapiga kimyaaa akkmaliza kipindi chake ametulia kwake tunaanzisha sasa keleleeeee .

Kwa ujumla hata shetani ana unafuu kuliko sisi.

Mtu hata dini yake haimruhusu kuongoza sisi tunasema tunaenda naye , tunaenda naye wapi? Atatufikisha wapi?
 
Hivi ni nani akipewa Bil 2 kati ya hizo bil 260 atasimama imara kutetea taifa letu? Hata Tundu Lissu pamoja na Uzalendo wake hawezi shinda.

Tumeshuhudia mlolongo wa kesi nyingi serikali ikishindwa hata mahakama za hapa kwetu.

Mtu anaelipwa chini ya 5M akasimamie kesi ya billions unategemea nini?

Suluhisho la haya mambo ni tushughulike huku kwetu hasa tunapoingia mikataba na tenda mtu akiingi mkataba mbovu ni anyongwe tu awe mfano maana hizo pesa zinazopotea zingeweza okoa maisha ya Watanzania wengi.

Na Watanzania tufunguke mtu kaingia mkataba mbovu 2013 /2014 unakuja unavunjwa 2017 analaumiwa alievunja alie ingia katulia anaejoy life, tuko serious kweli?

Tuanze na Mbarawa ama ushu..ngi?
 
Anayetakiwa kunyongwa ni kiongozi mkuu sababu yanatokea akiwa wapi
 
Hivi ni nani akipewa Bil 2 kati ya hizo bil 260 atasimama imara kutetea taifa letu? Hata Tundu Lissu pamoja na Uzalendo wake hawezi shinda.
Hivi Mruma na Osoro mliwapa mpaka vyeti vya uzalendo kivipi Sasa wakishindwa kesi mnawaita wamehongwa?
Tumeshuhudia mlolongo wa kesi nyingi serikali ikishindwa hata mahakama za hapa kwetu.
Sababu Wana uwezo mdogo sana, hivi kwa English Ile ya Prof. Osoro na Mruma unaweza tetea hoja zako kweli? Tuna uwezo mdogo ila ujuaji mwingi. Hivi Kuna haja ya kumhonga mtu asiyejua lolote?
Mtu anaelipwa chini ya 5M akasimamie kesi ya billions unategemea nini?
Sio kweli, Hawa wanakula miposho mirefu sana unakuta kesi ipo mwezi wa 10 ila wanapenda mwezi mzima kabla na wanakaw hoteli za nyota Tano. Hivi CCM na ufisadi wote huu wakipata kasafari kadogo unadhani wataambulia million 5?? Lazima waongeze gharama Ili kujustify ufisadi.
Na Watanzania tufunguke mtu kaingia mkataba mbovu 2013 /2014 unakuja unavunjwa 2017 analaumiwa alievunja alie ingia katulia anaejoy life, tuko serious kweli?
Mbona hao kina Osoro na Mruma wamekiri walipitisha hivyo vibali alafu hao hao wakaja futa leseni. Ukishafanya makosa lazima uwe smart kutafuta loophole uwabane wawekezaji. Mfano unaweza waundia zengwe kuwa wanachafua mazingira au ukategeshea kesi ya kikodi basi ukakifunga kiwanda na kufuta leseni. Sasa sisi tunaenda kichwa kichwa kufuta leseni bila kufanya analysis ya madhara yake kisheria.
 
Kwa sababu tunampa mtu yeyote uongozi bila kujali elimu, uwezo, uaminifu, uwezo na uzoefu.

Akiwa bibi mpe !!!! Tutaenda naye akiuza Tanapa tunapiga kimyaaa akkmaliza kipindi chake ametulia kwake tunaanzisha sasa keleleeeee .

Kwa ujumla hata shetani ana unafuu kuliko sisi.

Mtu hata dini yake haimruhusu kuongoza sisi tunasema tunaenda naye , tunaenda naye wapi? Atatufikisha wapi?
Nimependa sana hata hapo kwa elimu.tuna rais hata asiyejua kuwa yeye ni rais
 
Mbona pale kesi ni rahisi nyie kushindwa.

Kwanini mliwatoa RL wakati mngewaachia ilikuwa inaisha mwaka huu kama walikuwa hawajaanza uzalishaji?
Ulikuwa ujinga wa ajabu, kwanza hakukuwa na uzalishaji, pili leseni ilikuwa inaisha ndani ya three years ambayo ulikuwa muda mfupi sana ukilinganisha na hela inayolipwa. Kesi walishindwa toka wakiwa Bagamoyo Mruma ameniaibisha sana... kila kitu cha kufanya washinde kesi walikitia kapuni. Huku bi tozo kabakiza kuwarembulia tu. Inatia hasira. Kule mkuju napo Rostam anaandaa bomu jingine ngoja warusi wakae sawa tutanyooka tu.
 
Back
Top Bottom