Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Kaongeza misamiati siku hizi kuna matusi , huu ndio wimbo wake wa kwanza kwenye album katoa video juzi juzi, haueleweki anaimba nini, hapo kwenye sleep sleep nafikiri alimaanisha halali lali, hiyo outside sijui ndio ametoka😆

"Yeah hustle everyday I never sleep sleep coz am outside
When am falling love I go deep deep coz am outsidee
Time for the money two for the show enzi za kuuza maji na wanangu wa kariakoo
That was before long time ago I wish you know I wish you know yeaah
"

Chorus:
"We are outside outside outside outside
B*tch am outside outside outside outside
Am outside outside outside (Eeeh)
Kondegang we are outside outside outside (Yah yah yah)
"
I never sleep sleep😂😂😂😂
Kwan ilitakiwa aseme vp
 
Summer Walker ni msanii mkubwa tu Marekani kwa sasa kwenye mkataba wake kapewa advance ya $110,000, kwenye mauzo ya album kwa kila $1 atakayotengeneza yeye atapewa 16 cents baada ya kuirudisha advance aliyopewa. Record labels hazina huruma, ndio soko la kibepari hapo penyewe bongo bado mziki unapelekwa kishikaji na kibinadamu sana.
Wabongo tushazoea Mambo ya huruma hata panapobiashara
 
Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na ccm kuwapotosha wananchi , na hasa hawa wanaoitwa Wanamuziki wa kizazi kipya , ambao pia wanatuhumiwa kusafirisha na kusambaza madawa ya kulevya hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa .

Bali nimesononeshwa sana na yaliyojitokeza kwenye mgogoro wa Harmonize na Diamond , pale huyo Harmonize alipokuwa anaomba kujitoa kwenye lebo ya WASAFI , mengi sana ameongea mwenyewe kila mtu kayasikia wala sina haja ya kuyarudia , bali nitagusia kidogo maeneo mawili tu .

Kwamba Diamond alimwambia Harmonize kwamba anaweza asimkamilishie kile anachotaka na wala hatomfanya chochote na kokote atakakoenda hatofanikiwa , kwa vile HAMUWEZI KISERIKALI , KIFEDHA NA KIUCHAWI , hii ni kauli ya kijinga sana kutolewa na anayeitwa msanii mkubwa , ni kauli ya kishamba sana iliyojaa Utanzania mtupu ! Jambo lingine linalotia aibu ni kitendo cha Harmonize Kuomba msaada kwa Magufuli moja kwa moja baada ya ngazi za chini ikiwemo wizara kumgwaya Diamond , Yaani Rais wa nchi ampigie simu Msela Diamond na kumbembeleza ili akubali kuterminate mkataba wa Harmonize na Wasafi ! hili ni jambo la kutia aibu sana , Yaani inawezekanaje Wizara na BASATA kutiwa mfukoni na msanii mmoja ?

Haya mambo yakiachwa iko siku yatakuja kufedhesha mamlaka ya Rais , na sisi kama wananchi hatutakubali .
Waingilie kati ili iweje tuna mambo mengi sana na ingekuwa vizuri kama akianzisha system ya wasanii kulipwa kazi zao zikitumika mahala popote na kusimamia kazi zote za wasanii.

Mimi hapo sioni tatizo lolote zaidi ya kelele tu, watagomba wakidrop watapatana.
 
Fikiria hata kama ungekua ni wewe
umerudi kutoka Marekani na msweta wako unakutana na joto nyuzi 999... gogo lilikubana kwenye ndege unafika airport maji yamekata...
Albamu imebuma
umeme nao umekatika unarudi country wiz ameuza genereta la studio...lazma umuwaze simba
Weee Jamaaa
 
Yaani waingilie kati hawa wavuta ngada na ndumu, aloo tumia akili kidogo tu wacha wamalizane hukohuko.
Wizara iko busy na vigodoro na michiriku huku hamna mda wa kupoteza msiichukulie poa na hao wamarekani wenu "beibi"
 
Yatakuja au tayari yamelifedhehesha taifa! Yaani Rais wa nchi awabembelezee wasanii! Sishangai kwani Rais alimvika kofia msanii! Nikamkumbuka yule mama aliyemfunga kamba za viatu mwanae ikulu mbele ya Rais.
Na yule DC wa Iringa aliyempigia salute dai. Akasema wewe nasib ndio kila kitu
 
Unaambiwa harmonize alimpigia simu mpaka mwakyembe ambaye kwa wakati huo ndio waziri wa sanaa, lakini yule mnyakyusa naye alikuwa chawa hakutaka kumsikiliza harmonize
Alimjibu bana eeh hebu subir nkaongee kwanza na nasib
 
Diamond anatakiwa ayatolee ufafanuz haya malalamiko , Harmonize anamtuhumu Diamond kwamba kuna watu anawatuma wamchafue notable Baba levo na Juma lokole , ili kumharibu kiidie azma yake ya kuvunja mkataba , kwani by that time kwake ilikuwa ni ngumu hata kumfikia Diamond Kwa jinsi mambo yalivyokuwa yana-turn around...

Aliwafikia watu kama kusaga ( sababu ya status yake na ushkaji na mond ), alimfikia mama dangote (nguvu ya mama) alimfikia mwenyekiti sjui ndo katibu wa Basata, na alimfikia
J3 dai anafanya press na aljazira
 
Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na ccm kuwapotosha wananchi , na hasa hawa wanaoitwa Wanamuziki wa kizazi kipya , ambao pia wanatuhumiwa kusafirisha na kusambaza madawa ya kulevya hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa .
Tunaweka rekodi sawa, Konde Kasema Raisi JPM alimpigia simu waziri wa sanaa wa wakti huo Hon. Dr. Mwakyembe. Mwakyembe ndio akawapigia airport kwamba wamzuie msaanii wa WCB asitoke nje ya nchi mpaka awe kasaini termination contract.

Kumbuka Mwakyembe alikuwa waziri wa miundombinu mwenye dhamana na airport wakati fulani kabla hajapelekwa wizara ya sanaa na utamaduni, hivyo I presume alikuwa na contacts za airport
 
Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi
Tunaweka rekodi sawa, Konde Kasema Raisi JPM alimpigia simu waziri wa sanaa wa wakti huo Hon. Dr. Mwakyembe. Mwakyembe ndio akawapigia airport kwamba wamzuie msaanii wa WCB asitoke nje ya nchi mpaka awe kasaini termination contract.

Kumbuka Mwakyembe alikuwa waziri wa miundombinu mwenye dhamana na airport wakati fulani kabla hajapelekwa wizara ya sanaa na utamaduni, hivyo I presume alikuwa na contacts za airport
 
Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na ccm kuwapotosha wananchi , na hasa hawa wanaoitwa Wanamuziki wa kizazi kipya , ambao pia wanatuhumiwa
Diamond asidanganye lolote kuhusu serikali hawez kuiweka mfukoni. Serikali ya tanzania as idharirishe kiwango hk. kifedha pia Hana hela za kutisha, kiuchawi labda huo wa kumlala mama yake.... Ndio maana Zai akaona tusitoane roho na mama mkwe kisa........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom