Ni lini Diamond atapewa maua yake?

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Mtampa lini Diamond Platnumz heshima yake kwa kile alichokifanya kuwainua Harmonize na Rayvanny wakati wao wameshindwa kabisa kuwainua wengine kwenye lebo zao.

WCB ndio lebo pekee iliyofanikiwa kupelekea wasanii International na kujulikana... Leo hii ukimzungumzia Zuchu, ni msanii international. Ukimzungumzia Mbosso Khan na wengineo ni wanasumbua vichwa vya mjini. Dogo D-Voice katoka juzi tu lakini sasa hivi ana hit songs za kutosha.

Nyie mashabiki wa konde gang for everybody msingemjua Konde Boy bila Chibu Dii Chibu Dee Simba (Wee Zombie Haujui). Harmonize anatutumua kifua lakini Godfather wake ni Chibu. Same applied to Rayvanny V-vanny boy Chui, leo hii kafanikiwa kuchukua tuzo ya BET kwa sababu alipewa platform na chibu Dii Chibu Dee.

Ni wazi kabisa PLATNUMZ inabidi apewe maua yake kwa kufanya soko la mziki kuchangamka na kuwa kibiashara. Diamond Platnumz akifa leo uenda yakatokea kama ya Kanumba na Bongo Movie. Tutakuwa kama wakenya na mziki wao, tunaimba wee ila hatutoboi. Mziki wa East Africa umeshikwa na WCB.
 
Wamekulipa kiasi gani kuleta adv ya Naseeb hapa JF.Pale nitakapo ona msanii anajenga Hospitali kwa ajili ya kuwatibu wanyonge au kujenga Shule kwa ajili ya wanyonge kupatiwa elimu mzuri hapo nitampa maua na vilua na asmini more then that ni ujinga tu .
Yeye kafanya kuinua vijana wengine kina Harmonize na wengineo ambao nao wanakundi la watu wengi wanaowategemea....

Wewe pia vingine unaweza kufanya wewe, sio kila kitu afanye mtu mmoja. Wewe mpaka hapo umeinua vijana wangapi?
 
hayo ni mambo madogo sana ukilinganisha na madhara ya yeye kuharibu maadili ya jamii anayofanya.
Yeye hana wajibu wa kuharibu jamii, mwenye wajibu wa kulea watoto katika maadili kwa asilimia kubwa ni wewe mzazi.... Vitu vinavyoharibu maadili ni vingi na sio mziki tu. Labda uje na hoja nyingine.
 
Hajawainua usimpe sifa asizo stahil.
Alichofanya ni kuwapa mafas ya kuonyesha uwezo (wao) kama yeye alivyopewa nafas na Bob Junior.

Mwisho wa siku akautumia uwezo wa hao vijana kujinufaisha. So kwakifupi madogo walipewa platform ila wakawa wao ndio wanapambana kuingiza pesa ya kumlipa Diamond na kujilipa wenyewe
 
Kwani kuwainua maana yake nini... Kuwapa nafasi ndiko kuwainua, kumtoa mtu chini na kumpa platform ya kujulikana ni kumuinua... Tukizungumzia mziki wa biashara umeanzia kwa Diamond
 
Hakuna msanii international Tanzania.

Nimemaliza.
diamond platinumz ni msanii international.

Kutambulika katika scale ya global ni mosi,
Kuingia katika contest nafasi za kimataifa ni pili.
Kuwa na stream nyingi katika mitandao mikubwa kama itunes, spotfy n.k ni kigezo no tatu.
Kuwa msanii mwenye hit ndan na nje ya nchi yako nyingi ni kigezo.

Wacheni ujinga diamond kaaminisha vijana weng mziki sio uhun na mziki wa biashara kwa kiasi kikubwa kaja kuuweka kwenye ramani
 
hayo ni mambo madogo sana ukilinganisha na madhara ya yeye kuharibu maadili ya jamii anayofanya.

Na kuimba ujinga
unachopaswa kutambua kila kizazi kina staili yake.
Diamond ndio kaharibu jamii au ni kizazi tu kinavyokua pamoja na teknolojia iliyokuja ambayo hatukuwa nayo tayari?
 
diamond platinumz ni msanii international.

Kutambulika katika scale ya global ni mosi,
Kuingia katika contest nafasi za kimataifa ni pili.
Kuwa na stream nyingi katika mitandao mikubwa kama itunes, spotfy n.k ni kigezo no tatu.
Kuwa msanii mwenye hit ndan na nje ya nchi yako nyingi ni kigezo.

Wacheni ujinga diamond kaaminisha vijana weng mziki sio uhun na mziki wa biashara kwa kiasi kikubwa kaja kuuweka kwenye ramani
diamond platnumz sio msanii international kwasababu;

mashabiki wake wengi hawatoki kwenye the biggest music consumers(US, UK, GE) yupo international hapa africa tu

na ndio maana akishindanishwa na wasanii international(kina burna, ckay, arya) hatoboi

kuhusu kuinua wasanii wadogo, karibia kila msanii kaanza kwa kujiegesha kwa mwingine
 
niambie katika watu 500 wanaotoka congo, Tz, malawi, kenya, ethiopia ni wangapi wanamfatilia meghan thee stalion au drake au lil baby?
Bado una matatizo ya kuamini wazungu ndio wasikilizaji na ndio wanaamua nani awe msanii international?

BTS wa korea ni wasanii wanaofuatiliwa na wana followers wengi, kuwa kimataifa unapewa na fanbase yako iliyotapakaa duniani kote na si watu wa race fulani.
Hakuna mtu asiyemfafilia msanii diamond kuanzia marekani, uingereza na nchi zote hizo duniani.
 
Bado una matatizo ya kuamini wazungu ndio wasikilizaji na ndio wanaamua nani awe msanii international?
Ndo ukweli, unadhani hizo academy awards kina burna boy wanachukua bure?

Mashabiki wa marekani na ulaya ndo wana uwezekano mkubwa wa kustream, kusafiri kuona shows, kupigia kura nominations

Wasanii wengi wa nigeria ndo wapo global, hata wakifanya show huku africa kuna wazungu wanakuja kuona

Angalia mashabiki wake wengi wanapotoka, hata nyumbani mnamkataa
{A4872EDF-F9D6-4640-8451-E39EF8BE4086}.png.jpg

Anaposikilizwa sana maredioni
{3D14FAC4-EBEE-41CD-9F1B-2BB682082CCB}.png.jpg
 
Ndo ukweli, unadhani hizo academy awards kina burna boy wanachukua bure?

Mashabiki wa marekani na ulaya ndo wana uwezekano mkubwa wa kustream, kusafiri kuona shows, kupigia kura nominations

Wasanii wengi wa nigeria ndo wapo global, hata wakifanya show huku africa kuna wazungu wanakuja kuona

Angalia mashabiki wake wengi wanapotoka, hata nyumbani mnamkataa
View attachment 2921209

Anaposikilizwa sana maredioni
View attachment 2921210
haya tumlinganishe na Tyla, chipukizi, lakini amekamata support ilipo

Anaposikilizwa sana
{42D7E1EC-A4B5-49CD-9F81-5F88FD600CAE}.png.jpg

Anaposumbua sana maredioni
{9CE07E42-4F5E-45A6-B3AC-BA863C65EE36}.png.jpg

halafu mnashangaa tyla kuchukua academy award mapema
 
Back
Top Bottom