Harambee ya CHADEMA - Naura Spring, Arusha

Harambee ya CHADEMA - Naura Spring, Arusha

Mimi ninachokiangalia si pesa itakayopatikana ila message inayotumwa kwa wananchi. Unapochangia kitu lazima utakiona ni chako kinakuhusu na utakuwa tayari kukitetea ikiwa ni pamoja na kukipigia kura. Chadema wameanzisha strategy nzuri, haijalenga kwa jimbo la Arumeru Mashariki tu bali ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2015. Chama kimeanza kuwaandaa watu kisaikolojia wazidi kukipenda hasa vijana wanaochipukia 14 - 19 years old. Nina uhakika hawa wanaobeza leo mbinu hii watakuja ku realize faida yake baada ya miaka miwili ijayo.
 
Kuna check imepokelewa yenye thamani milioni saba kutoka kwa mtazamaji wa TV kamtuma mtu, hakutaka jina lake litajwe! Imekabidhiwa kwa mhe Mbowe!

Peoples' Power!
 
hahaha watanzania bana CCM imewakuwa ikiwachangisha watu miaka nenda rudi hata kama return yake ni almost zero katika utendaji. Leo chama kingine bilakuomba radhi au kibali kimeamua kuwapa nafasi wanachama na mashabiki wake kukiunga mkono imekuwa nongwa. Hii sasa ni sehemu ya siasa za kawaida tusiogope au kukwazika. CCM ikija na kuomba kuchangiwa wanaoiunga mkono wanayo haki ya kufanya hivyo tena kwa furaha. Waacheni CDM wajichangishie and I hope this is one of the many other fundraising in the future.

Jambo kubwa ni:

a. Lazima kutangaza kinachopatikana
b. Kiasi kinachopatikana NI LAZIMA kigawanywe kati ya taifa na local branch.
 
Du wanachi maskini wa tanzania wanachanga kidogo walichonacho then zitumike kwa ajili ya chopa lol

Kikwete katumia ngapi tangu aingie madarakani kupanda ma Boeing? Na zilikuwa za nani?
Mara nyingine fikirieni kabla ya kuandika lolote maana sio lazima uandike kitu hapa.
Shwaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Kuna jamaa alikuwa anaangalia kipindi hiki akiwa home kwake Arusha....na ameamua kuandika cheki ya millioni 7
na kuituma kwenye kikao hiki kinachoendelea. Mungu ibariki Chadema!
 
Njia hii itumiwayo na Chadema ni mujarabu, kwani inapeleka umiliki wa chama mikononi mwa umma!
 
hahaha watanzania bana CCM imewakuwa ikiwachangisha watu miaka nenda rudi hata kama return yake ni almost zero katika utendaji. Leo chama kingine bilakuomba radhi au kibali kimeamua kuwapa nafasi wanachama na mashabiki wake kukiunga mkono imekuwa nongwa. Hii sasa ni sehemu ya siasa za kawaida tusiogope au kukwazika. CCM ikija na kuomba kuchangiwa wanaoiunga mkono wanayo haki ya kufanya hivyo tena kwa furaha. Waacheni CDM wajichangishie and I hope this is one of the many other fundraising in the future.

Jambo kubwa ni:

a. Lazima kutangaza kinachopatikana
b. Kiasi kinachopatikana NI LAZIMA kigawanywe kati ya taifa na local branch.
Maneno mazito sana haya
 
Mkapa katoa maagizo eti baada ya uchaguzi wa arumeru matokeo yatangazwe kuwa CCM wameshinda tu na baadae CHADEMA waende mahakamani.
Dr. Slaa anasema CCM ndo watakaoenda mahakamani this time

Mkapa ni janga la Taifa, JK asipoangalia atajikuta anasimama ICC kwa ajili ya Mkapa.
Ijulikane kuwa Mkapa anahaha ili kujinusuru kulipia ufisadi aliotufanyia. Mkapa apende asipende mzimu wa ufisadi wake utamfuata tu, hata kama atakuwa amekufa atakutana nao kwa Mungu.
 
Kwa nini Harambee hii inafanyikia Kaskazini tena Usiku?????

Harambee hii inafanyika Kaskazini kwa sababu ni moja kati ya maeneo ambayo raiya wake wamejikomboa kifikra.
Harambee hii inafanyika usiku kwa sababu mchana watu wengi wapo makazini/shuhulini kwao wakitafuta hizi pesa za kuchangia usiku huu.
Samahani, Eti kwako ni magharibi au kusini??
 
Kweli mpesa inagoma nahangaika hapa bila mafanikio.
 
Mkuu watu kama Rejeo,Ritz,Waberoya,Mohamedi shossi,Kimbunga and com'leo hawatapata usingizi kwa chuki waliyonayo
dhidi ya CDM...yaani kama ninawaona walivyokasilika huko waliko. Poleni sana! Mnamuona Mbowe huyo? Mnaona
hayo manoti ya michango hapo mezani? Kubali mkatae Chadema ni namba nyingine!

Unamlinganisha waberoya na rejao?nafikiri waberoya ana misimamo yake binafsi isiyofanana na misimamo njaa ya rejao
 
Back
Top Bottom