Harambee ya CHADEMA - Naura Spring, Arusha

watanzania wanafiki sana,mzee anachangia pesa zote hizo wakati vibarua wake wa kampuni yake ya utalii wanateseka pale katika hoteli yake ya keys hotel kusubiri ujira ambao kwanza wanapunjwa sana,wanacheleweshewa sana,wafanyakazi wa redio yake wanalia njaa! Mi nafikiri badala ya kujionyesha kwenye itv, angewasaidia kwanza vibarua wake otherwise huo unakuwa ni unafiki tuu ambao hauna maana
hao vibarua wakamshtaki. Kwani hawajui mahakama ya kazi ilipo?
 
Dialo anajua tofauti kati ya yeye kama mtu na ufuasi wake wa kisiasa CCM ni vitu viwili tofauti ukilinganisha na makusudio ya biashara ambazo anazimiliki yeye hivyo haimsumbui kitu hata kidogo kutenganisha itikadi na siasa.

Usione hata Mzee Mengi ni kwamba tu kashikwa pabaya na CCM kuhusu mambo fulani hivi ndio maana analazimika kufunika miiko ya kitaaluma kuchukuliwa nafasi na ushabiki kwa CCM hivi sasa.

Si kipindi kirefu sana vyombo vingi sana nchini navyo vitaanza kufunguka taratibu nje ya mabano ya CCM ya hivi sasa.

Dialo ccm washamwaga naye kaamua kulipa kisasi na ndicho kinauchotokea. 2010 alishindwa kuiruhusu coz naye alikuwa mgombea ila sasa ni mwanachama huru kabisa. Viva Dialo kwa maamuzi magumu
 
Mkuu, hizi tuhuma ulizozitoa kwa nini usizipeleke kweye vyombo husika?

Mkuu vyombo husika nchii ni vipi hivyo? Kwa manumba au saba sita? Mkuu wa Kaya aliileta Richmond then akairuka eti haijui.
Mwakyembe akaichunguza juu juu akapewa unga. manumba, nahodha, mponda wote hawajui jamaa anaumwa nini.
Zombe kaua watu na kupora ila yuko mtaani sasa.
Vyombo husika ni M4C tu.
 
Serikali ya CCM isiendelee kuikwaza jamii ya Tanzania kwa kutumia kituo cha vyombo vya habari kinachoendeshwa na kodi za watu wenye itikadi mbalimbali kisiasa nchini na kugeuza hizo rasilmali kuwa ni haki, miliki na stahili ya kipekee kupengelea kungi moja tu ndani ya mipaka yetu.

Hili tukalitazame kiundani zaidi kabla hakujachelewa sana.
 
Back
Top Bottom