Malyenge
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 6,658
- 3,646
Wacha uwongo wewe hata kama wewe ni mmja wa beneficiaries hao.
Waheshimiwa hao walipewa hela hizo kama mkopo usio na interest kwa ajili ya kununulia magari makubwa ya kuwahikishia usafiri salama. Sheria iliyotumika kuwapa mkopo huo inabainisha wazi kuwa zitatumika kununulia magari kwa ajili ya usafiri wa wabunge katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku; na kila siku wanalipiwa mafuta kwa ajilia ya usafiri huo huo. Majukumu ya wabunge siyo tu kuzunguka jimboni kwake bali ni pamoja na kuzunguka sehemu nyingine nchini kulingana na atakavyotumwa na bunge. Ndiyo maana hata wabunge wa kuteuliwa wasiokuwa na majimbo walipewa hela hizo, na pia wanapewa hela za mafuta.
Ni kweli sina uhakika sawasawa kuwa walipewa kiasi gani kwa vile namba kamili huwa inafichwa, hata hivyo miaka kadhaa iliyopita tuliambiwa ni milioni themanini. Iwapo walipewa zaidi ya hapo, basi ni kwa nini watembelee na bodaboda; je wakianguka juu ya mabodaboda hayo sakaumia bado bunge letu litawahudumia matibabu yao?
Kumbe unakubaliana na mimi kwamba walikopeshwa na SI KWAMBA WALIPEWA. Au bado umeshikilia kwamba walipewa? Na pia unakubali kwamba wabunge hawana limit ya mahala pa kwenda ilimuradi ni Tanzania na kwa ajili ya ya wananchi! Halafu unaposema wanapewa pesa za mafuta sikuelewi! Maana allowance ya mafuta ni mojawapo ya malipo yaliyomo kwenye payroll. Yaani ni sawa na marupurupu unayolipwa wewe hapo TPDC! Kwa hiyo si ajabu kumwona mbunge ana gari lake Singida wakati yeye ni mbunge wa Songea. Suala la wabunge kupanda bodaboda si issue maana kama anaweza kuzunguka Tanzania kwa bodaboda mimi sina la kusema, isipokuwabaadaye wakianza kutembelea bajaji au bodaboda msije kusema wamevunja sheria.....