HKigwangalla
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 717
- 971
-Kuwa karibu na wananchi kivipi?Yeye ni mwakilishi wa wananchi lakini inaonekana anawakilisha wavunja sheria za barabarani na wahalifu.Hapa anastahili kuchukuliwa hatua za kisheria mara moja
-Pia hoja ya kuwa karibu na wananchi kutafuta ATM kwa kupanda Bodaboda mjini ni kutafuta cheap popularity na ku-expose fikra zilizochusha na kwa kuwa huyu ni msomi mwenye MBA anajua umuhimu wa huduma ya kibenki vijijini.Sasa kule Nzega ameshapigana kwa kiasi gani kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi vijijini?
-Nilidhani hiyo ndiyo inge-reflect ukaribu wake kwa wananchi kuliko jitihada hizi anazofanya mjini za kuvunja sheria za usalama barabarani na kuwadhalilisha wananchi waliomchagua kwa jaribio hili la kuonyesha yeye ni mwakilishi asiyezingatia sheria na anayerudisha nyuma harakati za kukabiliana na ajali za barabarani
Nd. Ben,
You have put forward some good points here that I feel obliged to address.
1. Kuwa karibu na wananchi - nimeeleza kwa urefu dhana hii kwenye mchango wangu mwingine hapa so soma kule.
2. Kuhatarisha maisha yangu - I totally agree with you kwamba kwa kiasi fulani nimehatarisha maisha yangu kwa kutokuvaa protective gears, lakini sina hakika kama kuna sheria nimevunja kwa kuwa sikuwa mwendeshaji na ndiyo maana kwenye mchango wangu kule FB (kuna mtu ameuleta hapa) nimeeleza kwamba pengine kuna haja ya kutunga sheria itakayolazimisha wapanda pikipiki wote (uwe mwendeshaji ama abiria) ni lazima wavae protective gears, na hii kazi nitaifanya. Naomba radhi kwa kutokuwa mfano mzuri kwa kuvaa protective gears ukizingatia kuwa mimi ni Daktari Bingwa niliyebobea kwenye fani ya Injury Prevention and Safety Promotion na zaidi kwa kuwa mimi ni Mbunge na kiongozi katika jamii - mara nyingi nikiwa Nzega huwa natumia protective gears na majuzi tu nimewagawia reflective tops waendesha bodaboda wote jimboni.
3. Huduma za kibenki - pale kwetu Nzega mjini kwa sasa tuna matawi ya benki za NBC na NMB, na tumefanya mazungumzo na uongozi wa benki ya CRDB watuletee tawi lao pale na wameishakubali - tayari tumewapa kiwanja. Benki vijijini - tunaelekea kuanza mchakato wa kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Jamii Nzega (Nzega Community Development Bank) ambayo itafungua matawi kwenye tarafa zote nne za wilaya ya Nzega, kwa kuanzia; na itaanza kwa kufanya kazi na SACCOS za kila kata ambazo tumezianzisha. Mtaji tumeupata kutokana na ushuru wa huduma (service levy) tuliyoidai kwa mbinde kutoka kwa wawekezaji wa kampuni ya Resolute (mgodi) ambayo haikuwahi kulipwa kwa zaidi ya miaka 14.
Wakatabahu,
HK.