Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,086
- 7,097
Katika hali isiyo ya kawaida, sintofahamu iliibuka Septemba 10, 2025 wakati wa siku ya kwanza ya kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Tabora zilizofanyika Wilayani Nzega, baada ya mabango yaliyokuwa yakimnadi mgombea huyo kuondolewa ghafla kabla ya ujio wake.
Mabango hayo yametaja kuandaliwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla, yakionesha miradi na kazi zilizotekelezwa na CCM chini ya uongozi wa Dkt. Samia katika jimbo hilo na wilaya nzima. Hata hivyo, inadaiwa kuwa viongozi wa chama katika Wilaya ya Nzega walimpigia simu Kigwangalla na kumtaka kuyaondoa kwa madai kuwa yeye si mgombea, hivyo hapaswi kutengeneza mabango ya kumnadi mgombea wa Urais.
Kwa mujibu wa mashuhuda na waandishi waliokuwepo Tabora, mabango hayo yalikuwa yanaonekana dhahiri mapema asubuhi ya tarehe 10 Septemba, lakini yaliondolewa kufikia mchana.
Taarifa ambazo Jambo TV imezipata zinaeleza kuwa Kigwangalla alitetea hatua yake akisema yeye kama mwana CCM ana haki na wajibu wa kumuombea kura mgombea wa urais kupitia chama chake. Hata hivyo, viongozi wa chama wilayani humo walimtaka abadilishe mabango hayo na kuweka pia picha za mgombea ubunge aliyeidhinishwa kwa jimbo hilo, jambo alilokataa. Baada ya mvutano huo, maofisa usalama wa Wilaya wakaamuru mabango hayo yaondolewe mara moja.
Jambo TV imemtafuta pia kwa njia ya simu Katibu wa CCM Wilaya ya Nzega, Adia Rashid ambaye ameeleza kuwa hatua ya kuondolewa kwa mabango hayo ilihusiana moja kwa moja na kutokufuata utaratibu wa chama.
Naye Dkt. Kigwangalla alipopigiwa simu amesema mabango hayo aliyatengeneza kwa ridhaa ya chama Makao Makuu, na kwamba picha alizoweka ni zile alizopewa na chama. Aidha, mratibu wa kampeni za CCM Kanda ya Kati, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa aliridhia yawekwe na alielekeza kwamba ‘logo’ ya HK ifunikwe na stika- maelekezo aliyoyatii. Pamoja na kutii maelekezo hayo ameshangazwa kuona mabango yake yote yakitolewa