Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Ni jambo rahisi tu la kusema mchakato wa kuwapata hao wabunge 19 ndani ya chama ulifanyikaje na majina yao pale NEC yalipelekwa na nani.

Hakuna siri ya kusubiri rufaa ndio ueleze ikiwa mchakato wote ulifuata katiba ya Chadema.

Hadi sasa picha waliyonayo wananchi ni kwamba wabunge wa viti maalumu Chadema hupatikana kwa njia za panya yaani kwa utaratibu usio rasmi.

Maendeleo hayana vyama!
Ni jambo jema, kweli itatuweka huru.
 
Wafanye haya kwanza.
1. Watangaze kukubaliana na maamuzi ya kamati kuu yaliyowavua uanachama.
2. Watangaze kuachana na ubunge wa viti maalum waliojivika kihuni huni.
3. Waseme nani alikuwa anawatumia.
4. Waombe radhi watanzania wote.
5. Wakae kimya kabisa.

Wakifanya hayo yote, mimi nitakuwa miongoni mwa watu watakaotafakari namna gani wasamehewe.

Nina uhakika kwa 99% hawawezi kufanya lolote katika hayo, maana hicho walichokifanya leo kwenye Press kulikuwa staged na CCM Lumumba toka jumapili. Kama huamini subiri kitakachofuata.
Mbowe hana shida na viti maalum wewe. Ndugai na Jiwe ndiyo wanahitaji kutick boxes za kuonyesha wanajali demokrasia.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Huu muamala hatari sana, kuukunjua unaweza kutikisa nchi.

Lakini kauli yangu inabaki pale pale, bora kahaba kuliko mwanasiasa. Usimwamini mwanasiasa yeyote yule.
 
Mambo hayaendi kirahisi namna hiyo.

Hao traitors siyo muda sahihi wa kusamehewa, wamelitafuta na sasa wanalipata. Nafasi zao zitajazwa na wengine.!
They're matured politicians, wanatambua walichofanya, wanachofanya na watakachokifanya baada ya hiyo press.
 
Mzee Mdee alipoulizwa ilikuwaje Nusrat Hanje jina lake kuwepo kwenye orodha yake ya viti maalum vya CHADEMA wakati alikuwa Jela na siku moja kabla ya kuapishwa alitolewa jela, Mzee Mdee alisema hilo suala akaulizwe DPP, maana hata yeye hajui!
 
We are on the same page Mkuu wakifanya hayo mimi binafsi nitaomba wasamehewe na kupokelewa kwa mikono miwili, hiyo namba tatu kwangu mimi si muhimu sana kwani aliyekuwa anawatumia ni huyo anayejiita mwendawazimu na makamongo yake baada ya kugundua wizi alioufanya umesababisha Bungeni kutokuwepo wapinzani na hivyo kutasababisha Nchi kukosa 2 trillions kutoka UN ndiyo sababu wakaanza kutapatapa.
Wafanye haya kwanza.
1. Watangaze kukubaliana na maamuzi ya kamati kuu yaliyowavua uanachama.
2. Watangaze kuachana na ubunge wa viti maalum waliojivika kihuni huni.
3. Waseme nani alikuwa anawatumia.
4. Waombe radhi watanzania wote.
5. Wakae kimya kabisa.

Wakifanya hayo yote, mimi nitakuwa miongoni mwa watu watakaotafakari namna gani wasamehewe.

Nina uhakika kwa 99% hawawezi kufanya lolote katika hayo, maana hicho walichokifanya leo kwenye Press kulikuwa staged na CCM Lumumba toka jumapili. Kama huamini subiri kitakachofuata.
 
Halima na wenzake licha ya kukosa majibu ya msingi mfano ilikuwaje wajipeleke kuapishwa ikiwa chama hakikuwa kimefanya uteuzi wa wabunge; saini ya katibu mkuu wa chama waliipate wakati KM mwenyewe alisema wazi hajapeleka majina; kwa nini walikiuka utaratibu wa chama n.k lakini pia wamejaribu kuleta hoja ya kwamba mwaka 2010 na 2015 chama kiligomea matokeo lakini bado walienda bungeni.

Ni hoja dhaifu tu. Kwa sababu mwaka 2010 na 2015 chama kiligomea na kutotambua matokeo ya Urais pekee. Ndio sababu walitoka nje alipoalikwa kuhutubia bunge. Walitoka sababu hawakuwa wanatambua matokeo yaliyompa ushindi. Safari hii, 2020 chama kimegomea matokeo yote ya uchaguzi mkuu.

Hakiyatambui na msimamo wa chama ni uchaguzi kurudiwa upya chini ya tume huru ya uchaguzi (kama ilivyotokea Malawi). Hivyo chama hakitambui chochote kilichotokana na uchaguzi (ikiwamo hizo asilimia za ubunge wa viti maalum) kwa sababu walikamata kura fake za udiwani, ubunge na urais, mawakala waliondoshwa kabla/wakati wa kupiga kura na/au kuhesabu kura n.k. Hivyo, msimamo wa chama ni kutotambua matokeo yote ya uchaguzi na kutaka urudiwe.

Halima na wenzake wamekamatwa pabaya. Wamefutwa uanachama sharti waamue mambo mawili tu: Kukiri, Kujutia, na kuomba msamaha CHADEMA na kuukana ubunge wao, au kuhamia ccm moja kwa moja na kuendelea na mambo mengine.
Kwa upande wa CHADEMA, wao wameongeza credibility yao kwa wananchi kwa kuonesha kivitendo kwamba kipaumbele si fedha za ruzuku ama ubunge bali uhuru, haki, na maendeleo ya watu kama kauli mbiu yao ya uchaguzi ilivyoainisha. Hivyo katika mchezo huu CHADEMA ameshinda points, sirikali hasa kwa ile movie ya Nusrat IMEPOTEZA BIG TIME, Halima & co. wamepoteza in the long term.
 
Ni jambo rahisi tu la kusema mchakato wa kuwapata hao wabunge 19 ndani ya chama ulifanyikaje na majina yao pale NEC yalipelekwa na nani.

Hakuna siri ya kusubiri rufaa ndio ueleze ikiwa mchakato wote ulifuata katiba ya Chadema.

Hadi sasa picha waliyonayo wananchi ni kwamba wabunge wa viti maalumu Chadema hupatikana kwa njia za panya yaani kwa utaratibu usio rasmi.

Maendeleo hayana vyama!
Naunga hoja Yohane
 
Wendawazimu sio lazima uvue nguo, hivi ufukuzwe uanachama na chombo halali cha chama halafu uende kwenye press umevaa nguo za chama ulichofukuzwa? Ni akili matope. Hata kama utakata rufaa, hivi hiki sio kichaa. Kwanini usisubiri rufaa? Mwanachama kindakindaki unakata rufaa unajuaje kama utashinda rufaa? Mbinu ya kuleta mgogoro kwenye chama ya kishamba sana.
 
Pengine katika mambo ambayo aliyekuwa Mbunge wa Kawe Ndg. Halima Mdee hatokaa ayasahau maisha yake yoote na kujutia Zaidi, ni maamuzi ya kufanya "Press conference" leo bila kutafakari nini ingekuwa mrejesho wa "Press" ya Leo kutoka kwa Watanzania walio wengi.

Nadhani Jambo lilomponza Halima ni kusahau kuwa aliwakosea saana wananchi na alitakiwa kulitambua hilo kabla ya Press ya leo. Badala yake akaja kama mtu aliyekwisha andaliwa kujibu tuhuma fulani jambo ambalo limekuja kumtokea puani (hii ni kutokana na mrejesho kutoka kwa wananchi kupitia mitandao mbali mbali ya kijamii waliotoa maoni yao baada ya Press ya leo)

Swali la pili alilotakiwa kujiuliza kabla ya Press ya leo ni juu ya kwanini CCM wapo nyuma yake saana katika kuunga mkono usaliti alioufanyayeye na wenzake na mwisho kabisa angejiuliza hivi ni lini CCM waliwahi kuandaa "movie" ikapokelewa chanya na wananchi. Siku zoote sinema za CCM huonekana ni za kihindi mbele ya wananchi....

Ili kupata mrejesho wa Press ya leo tembelea mitandao mbali mbali ya kijamii m.f ya akina Milard Ayo (Facebook n.k) ujionee mwenyewe majibu ya wenye nchi yao..
 
Rule of law should be a cornerstone of our nation! Even the persons that have the power to be above the law by instruments, should observe the existence of such instruments as the law itself!

Wenye mamlaka wasitumie mapungufu ya kisheria yanayotoa mianya ya ubabe kuwa wababe. Huo ni ushamba uliopitiliza.
 
Pengine katika mambo ambayo aliyekuwa Mbunge wa Kawe Ndg. Halima Mdee hatokaa ayasahau maisha yake yote zaidi ni maamuzi ya kufanya "Press conference" leo bila kutafakari nini ingekuwa mrejesho wa "Press" ya Leo. Nadhani Jambo lilomponza Halima ni kusahau kuwa aliwakosea Watanzania walio wengi na alitakiwa kulitambua hilo kabla ya Press ya leo. Badala yake akaja kama mtu aliyekwisha anadaliwa kujibu tuhuma fulani jambo ambalo limekuja kumtokea puani (hii ni kutokana mrejesho kuptoka kwa wananchi
kupitia mitandao mbali mbali waliotoa maoni yao baada ya Press ya leo)
Swali la pili alilotakiwa kujiuliza kabla ya PRESS ya leo ni juu ya kwanini CCM wapo nyuma yake saana katika kuunga mkono usaliti alioufanya na mwisho kabisa angejiuliza hivi ni lini CCM waliwahi kuandaa "movie" ikapokelewa na wananchi. Siki zoote sinema za CCM huonekana ni za kihindi mbela ya wanchi....

ILi mrejesho wa Press ya leo tembelea mitandao mbali mbali ya akina Milard Ayo (Facebook n.k) ujionee mwenyewe majibu ya wenye nchi yao..
Okay, sawa basi.
 
Hao wanaomtukana Mdee waliambiwa waandamane na Lissu hakuna aliyetokeza poa yake
 
Back
Top Bottom