CHADEMA
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 488
- 2,468
Tumepokea hukumu iliyotolewa leo Alhamisi tarehe 14 Desemba, 2023, uamuzi wa Mheshimiwa Jaji Cyprian Phocas Mkeha;
1. Kwamba uamuzi wa kuwafukuza uanachama waliokuwa wanachama wetu 19 uliofanywa na Kamati Kuu ya Chama, umeendelea kusimama (Upo pale pale) na Mahakama imekubaliana kuwa taratibu zote za Katiba ya Chadema na Sheria za nchi zilifuatwa kikamilifu na Kamati Kuu katika kuchukua uamuzi huo.
2. Kwamba, maamuzi ya Baraza Kuu kuhusu Rufaa yamefutwa na hivyo Baraza Kuu linapaswa kukaa upya kusikiliza Rufaa; lakini Kamati Kuu ilishawafukuza Uanachama na uamuzi wake Judge kasema wazi upo sahihi.
Hivyo basi, kwa hatua ya sasa Chama kitawasiliana na Mawakili wake ili kutafakari hatua za kuchukua ikiwa ni pamoja na kumkumbusha Spika wa Bunge kuhusu utekelezaji wa uamuzi wa Kamati kuu ya Chama wa tarehe 27 Novemba, 2020 kwani Mahakama imethibitisha kuwa walishafukuzwa uanachama kihalali na taratibu zote zilifuatwa .
Tunawataka wanachama wetu watulie wakati huu chama kinapotafakari hatua za ziada.
Imetolewa leo Alhamisi tarehe 14 Desemba, 2023.
John Mrema
Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya nje.
Pia soma > Halima Mdee na wenzake Washinda kesi dhidi ya CHADEMA. Waendelea kuwa wanachama wa CHADEMA. Kuendelea na Ubunge wao