Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Well said. Tena aombe radhi maana aliaminiwa sana Halima, Esther B na Esther M. Hao wengine hata hatuwajui. Ila hizo no 3 zitafakari sana. Na zote 3 zilishinda 2020.
 
Ukweli ulikuwa upi zaidi ya kushawishiwa na CCM na kuwarubuni. Hawa wadada wakajisahau namna walivyokuwa wanavurumishwa na hao hao ambao leo wamewakumbatia.
Mtesi wako wa jana hawezi leo kuwa mkombozi wako( Bagonza voice)!
 
Nakupongeza kwa jinsi ulivyojibu hoja mbalimbali na kuonesha unatambua kuwa ni nani wanaokupenda na nani ni maadui lakini wanasema kuwa ndio walinzi wako. Yaani wauaji na watesaji wako leo wanakuwa walinzi na marafiki zako.
Nami niko upande wako kwa hili Halima umetumia staha sana kujibu. Of course katika watu waliofia CHADEMA wewe unaongoza among top three! Upepo ulikupitia na kama umetubu, MBOWE na kamati Kuu, let us open a new chapter! Let by gone be by gone particularaly kwa watu hawa 19.
 
Umeandika vizuri, lakini wenzako ndio walikuwa mstari wa mbele kumtukana hadi kuwaita COVID 19! Sasa swali, wanamuangaliaje leo? Watajibaraguza na kujifanya wanamsifia kama wewe?
 
Hao wakiruhusiwa kurudi wataanza kuleta vurugu ndani na kujijenga zaidi, huwezi kuwa na tamaa hadi unafikia hatua ya kufoji nyaraka ukisaidiwa na CCM halafu useme wewe ni Mwana Chadema, Fukuzia mbali hao.
Zipo adhabu nyingi ikiwemo kuwafanya wanachama wa kawaida.
 
Kwa hotuba ya Halima Mdee and Co. Ltd, I am convinced kuwa wameona wapi waliteleza na kweli wana damu ya CDM! let bygones be bygones forget past offences or causes of conflict and be reconciled.

Msiwape faida Nyang'au CCM.
 
Ndani ya CHADEMA hakuna wabunge wengine zaidi ya kina Halima Mdee na Matiko? Wao washindwe ubunge hao hao wajichague wapeleke majina yao.
 
Tatizo ni vita ya ubunge ndani ya chama, wakisamehewa kuna watu hawataridhika, Mbowe ana majina yake, Mnyika ya kwake, yaani ni full vurugu.
 
Shida ni kuwa ukiaminiwa itunze imani uliyopewa, kwani kujenga imani iliyopotea ina gharama kubwa mno. Hivyo leo mwataka kuaminiwa ilhali imani mliyoijenga miongoni mwa wafuasi wenu mmeivunja?
 
Ni jambo rahisi tu la kusema mchakato wa kuwapata hao wabunge 19 ndani ya chama ulifanyikaje na majina yao pale NEC yalipelekwa na nani.

Hakuna siri ya kusubiri rufaa ndio ueleze ikiwa mchakato wote ulifuata katiba ya Chadema.

Hadi sasa picha waliyonayo wananchi ni kwamba wabunge wa viti maalumu Chadema hupatikana kwa njia za panya yaani kwa utaratibu usio rasmi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wafanye haya kwanza.
1. Watangaze kukubaliana na maamuzi ya kamati kuu yaliyowavua uanachama.
2. Watangaze kuachana na ubunge wa viti maalum waliojivika kihuni huni.
3. Waseme nani alikuwa anawatumia.
4. Waombe radhi watanzania wote.
5. Wakae kimya kabisa.

Wakifanya hayo yote, mimi nitakuwa miongoni mwa watu watakaotafakari namna gani wasamehewe.

Nina uhakika kwa 99% hawawezi kufanya lolote katika hayo, maana hicho walichokifanya leo kwenye Press kulikuwa staged na CCM Lumumba toka Jumapili. Kama huamini subiri kitakachofuata.
 
Sema CCM haitaki maneno, hakuna cha watanzania hapa. Sema Jiwe, Ndugai, Mahela na Mugasha (may be)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…