Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Sawa dada umeyatoa ya moyoni na watu tumekusikia!

Hata hivyo kuna jambo moja bado hujaliweka sawa!

Tunataka kujua yale majina 19 ya MP's wa viti maalum yaliandaliwa na nani?

Yaliidhinishwa na kikao kipi cha chama?

Je, ni kweli Mnika ndiye aliyeyapeleka NEC kama jinsi mhalifu Mahela anavyosema?

Umeseusema ukweli kuwa CGADEMA ni taasis kubwa na inafanya kazi kitaasis sasa ni kwanini hata kama uliitwa na spika Dodoma usifanye mawasilianlo na viongozi wenzako japo Mwenyekiti Mbowe au Mnyika ambaye ndiye incharge wa suala hilo?

Mkubali kwamba mmekikosea chama na ombeni radhi kwa unyenyekevu kwani hakuna mkubwa kuliko chama!
 
Sawa dada umeyatoa ya moyoni na watu tumekusikia!
Hata hivyo kuna jambo moja bado hujaliweka sawa!
Tunataka kujua yale majina 19 ya MP's wa viti maalum yaliandaliwa na nani?
Haya ndio masuali ambayo watu wengi wanasubiria majibu yake.
 
Halima kajaziwa vyombo vya habari kama wakati ule wa Dokta MIHOGO alipounga juhudi.

MaCCM yanakoment kwa nguvu zote, kama wakati ule wa Lipumba na CUF.

Halima kanunuliwa kama kuku kishingo sokoni, kazi moja aliopewa, ahakikishe anavuruga CHADEMA na anachukua nafasi ya Mbowe.
 
Halima Mdee na wenzake wanaongea maneno mengi ambayo hayana maana... Watu wanachotaka kujua ni mchakato gani ulitumika na nani aliwapitisha kuwa wabunge wa viti maalum kupitia CHADEMA... Simple question tu. Maelezo mengi ya nini?
 
Watanzania ni kama tunachanganywa.

Spika Ndugai amesema wabunge 19 wanawake wa Chadema wananyanyasika kwa sababu chama hicho kina mfumo dume tena ni kampuni inayoongozwa na mtu mmoja...
Halima kamstukia spika kuwa ni mkaanga mbuyu tu. Hana lolote!

Kasema yu tayari kuyajenga.

Itapendeza kwa mustakabala mwema wa taifa akiumbuka mtu hapa!

Walisema waungwana: "Bibi na bwana wakigombana nyumbani, waache wataelewana wenyewe. Ukiingilia itabaki na aibu."

Yetu macho.
 
Halima Mdee na wenzake wanaongea maneno mengi ambayo hayana maana... Watu wanachotaka kujua ni mchakato gani ulitumika na nani aliwapitisha kuwa wabunge wa viti maalum kupitia CHADEMA... Simple question tu. Maelezo mengi ya nini?
Nilitarajia waandishi wa habari waulize Hilo swali lakini kimyaaaa

Tanzania ni nchi ya wendawazimu kabisa
 
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Naibu Katibu Mkuu kuna kitu wanakijua kuhusu sakata hili ambacho Mnyika hakijui

Wanakwenda kuyajenga. Hapo ndipo wasipohusika mnapotakiwa kuweza kujitambua nafasi zenu zilipo!
 
Sawa dada umeyatoa ya moyoni na watu tumekusikia!

Hata hivyo kuna jambo moja bado hujaliweka sawa!...
Kwa kuongezea siku anaapishwa Halima Mdee a.k.a Delilah wa Tanzania na genge lake alidai ana baraka zote za mwenyekiti , mbona hajazionyesha baraka hizo?

Maana chama kinaendeshwa kwa vikao, kikao kipi kikiwateuwa , maandishi yapi ya baraka za mwenyekiti walipewa ? Mbona hajaonyesha . Halima Mdee a .k.a Delilah wa Tanzania na genge lako mtakuwa wajinga sana kufikiri mkia unatikisa ng"ombe badala ya ng'ombe kuutikisa mkia .
 
Halima Mdee na wenzake wanaongea maneno mengi ambayo hayana maana... Watu wanachotaka kujua ni mchakato gani ulitumika na nani aliwapitisha kuwa wabunge wa viti maalum kupitia CHADEMA... Simple question tu. Maelezo mengi ya nini?

Hilo swali limeulizwa bi dada amekataa kulijibu kwa maelezo kuwa ni msingi wa mgogoro, adhabu na hivyo rufaa yao.

Kiufupi bila shaka jibu ni kuwa ndipo msingi wa kuyajenga ulipo!
 
Basi sawa ila CHADEMA kama CHADEMA haina mbunge hata mmoja, uchaguzi haukuwa huru tumegomea matokeo kutokana na uchafuzi uliofanywa na CCM.

Mnachotakanyie ni hela za mababeberu hazitatolewa kamwe, mark my words.
 
Nashauri nafasi zao zijazwe ili kupata viongozi wapya, lakini pia wanasheria wetu waende mahakamani Kuwafungulia mashitaka ya kughushi, na wawekee zuio la kimahakama kutumia alama za chadema kwa kuwa siyo wanachama tena hadi hapo watakaporudishiwa uanachama wao.

Nilitegemea kumsikia huyu Dada niliyemuamini, aliyepigwa na polisi, magereza nikaumia, aliyefukuzwa na kufungiwa vikao vya Bunge na ndugai nikaumia Mdee akieleza utaratibu wa kamati kuu au halamashauri kuu ulivyofanyika wakateuliwa na majina yao kupelekwa tume. Badala yake amaekuja na ngonjera za kijinga kabisa.

Halima ulipaswa kuwaeleza wandishi wa habari ni wakati gani vikao vya uteuzi vilikaa vikawateua, nani alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho. Vingenevyo rudi omba msamaha tena omba sana. Mdee tumekuchangia faini kubwa sana ulipohukumiwa na Mahakama za ccm, tulichanga pesa za matibabu yako, kifupi tulilia pamoja na wewe, tulihuzunika pamoja na wewe Lakini leo umetugeuka! Rudi Dada au kaa Kimy. Nakuhakikishia Mungu atatulipa haushi mwaka huu tutakusikia
 
Nilitarajia waandishi wa habari waulize Hilo swali lakini kimyaaaa

Tanzania ni nchi ya wendawazimu kabisa
Swali hilo limeulizwa jombi. Ni moja ya aliyokataa bi dada kujibu hadharani.

Ndipo msingi wa kuyajenga ulipo.
 
Nashauri nafasi zao zijazwe ili kupata viongozi wapya, lakini pia wanasheria wetu waende mahakamani Kuwafungulia mashitaka ya kughushi, na wawekee zuio la kimahakama kutumia alama za chadema kwa kuwa siyo wanachama tena hadi hapo watakaporudishiwa uanachama wao...
Halima hawezi kurudi CHADEMA, ameshakula hela ya kuivuruga CHADEMAna anacho fanya sasa sio kwa bahati mbaya, ni sehemu ya kazi aliotumwa alikounga juhudi. Muhimu ni kumdhibiti asituletee mambo ya CUF.

Halima katugeuka katikati ya vita, sio mwenzetu tena huyo.
 
Kwa hiyo alichokizungumza Mbowe na KK pale Kunduchi zilikuwa porojo tu
 
Kimsingi mkutano wa Mdee ni wa kuuza sura, kwasababu vitu vya msingi vyote tulivyotaka kusikia hujajibu hata moja
 
Back
Top Bottom