Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

All in all Halima Mdee umeteleza mno. Uwezo wako tunaujua ila kwa hili umeteleza mno. Wewe ni mjumbe wa baraza kuu taifa kwanini usingeenda ili haya ukayajibie huko maana mwenyekiti amesema hakuna barua aliyotoa na wewe unasema mwenyekiti alitoa barua sasa nani muongo kati yako na Mbowe.

Tunajua yote huisha vikaoni na chadema haiangalii umefanya nini bali inaangalia future ya chama.
 
Maswali mengi mliomuuliza H.Mdee yalikuwa yakimkakati sana na kwa namna moja yamemuyumbisha Halima kwa kipekee kabsaa na mengi amrshindwa kabsaa kuyajibu na Hilo ni ushindi wa kazi yenu. Ujibu wa maswali kisiasa hatukatai hasa ukiwa unajua ukweli wa jambo liliko Mezani. Kundi lile leo ukiangalia sura zao limeonyeha kukosa Amani kabsaa.

Kundi lile natabili kutoa siri ya sarakasi zote siku za mbeleni!! Hongera waandishi na sasa Hamisheni maswali kwa Tume ya Uchaguzi. Mtafuteni Mahera na Kaijage mukapge maswali ya kufungia mjadala mana in Mathematics there's always Chek and Balance!
 
Anazunguka mbuyu Kwa sababu hataki kuwa mbuzi wa kafara Kwa mbowe , amempa chance mwenyekiti wake kabla ya kumwaga ugali. Mbowe na Mdee ni top brand kwenye chama maswala ya kudhalilishana Kwa shinikizo toka Kwa watoto akina mnyika sio pouw , inshort mbowe anajua what is going on. Akishindwa kunetralize mambo, wataenda kuvuana mahakamani.
Acha prediction zako, Mbowe aliongea kwa uwazi na fasaha wazi wazi kwamba wao hawajahi kukaa kuandaa list ya majina na kupelekwa bungeni kama ilivyo katiba yao, na alirudia mara kadhaa hawa madada wamevuliwa uwanachama na nyadhifa zao zote ndani ya chama.

Ninachokiona kwa Halima Mdee anatafuta namna ya kuwa huru mtaani bila kunyooshewa vidole kila mahali apitapo jambo ambalo sasa haliwezekani tena, ukisaliti mara 1 heshima yako inapotea milele. Kujidai kwamba bado anaipenda Chadema ni unafiki wa kiwango cha juu zaidi kutaka jamii imuone kama hana makosa vile.

Njia ipo moja tu ili heshima yake/yao irudi na chama kifikirie kumpokea: Aache mara moja ubunge wa bandia na kuhudhuria vikao vya bunge akubali kwamba ubunge wake umepotea baada ya kufutwa uanachama lakini aombe radhi hadharani. Othewise ni wasaliti (Covid-19)
 
Maswali mengi mliomuuliza H.Mdee yalikuwa yakimkakati sana na kwa namna moja yamemuyumbisha Halima kwa kipekee kabsaa na mengi amrshindwa kabsaa kuyajibu na Hilo ni ushindi wa kazi yenu...
Hata wakati wanapiga picha na Ndungai walikua na huzuni kama vile wapo mahakamani na hakimu amewapa hukumu ya kwenda jela COVD-,19 wote miaka 30 pamoja na Kazi ngumu.

Usaliti ni laana inayowachoma wasaliti daima dawamu
 
Katika chaguzi zote tangu vyama vingi vimeanza kuanzia 2010, 2015 na 2020 hakuna uchaguzi ambao tuliuukubali

=>Lakini Wabunge si walienda? Kwanini 2020 wasiende mpaka sasa Madiwani wanaapa na Mbunge aliyechaguliwa ameapa
Usishangae sisi au wengine wakienda
 
Mpka sasa hivi hawajajibu maswali yenye tija, kwa mfano: Nani aliwasainia fomu na kugonga mihuri? Nusrat Hanje amefika fikaje bungeni? Imekuaje process zote zile zienda discreet kiasi kile mpka wameapishwa hakuna mtu aliyekuwa anajua? Na pia Leo asipoikana hyo nafasi yake ya ubunge wa kupewa apite hivi asijilazimishe kuwa mwana Chadema. Aamie hata ccm maana nacho ni Chama 😂
Mbona amejibu vizuri sana? Alichosema ni kuwa hayuko tayari kuendelea na malumbano in public ambayo yatawafaidisha wasio na nia njema. Haya maswali yote watayajibu katika rufaa yao mbele ya Baraza Kuu la Chadema.

Kwenye hili hawawajibiki kwetu bali kwa Chadema. Hakupinga kuwa Chadema walikuwa na haki ya kuchukua hatua waliyochukua. Kwa maoni yangu ameonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kutaa kuingia katika mtego wa kuanza kujibishana na chama chake hadharani.

Inabidi kujiuliza kwa nini CCM wanaonyesha "mapenzi" yao hadharani kwa hawa wanawake? Kulikuwa na haja gani kwenda kuwapongeza kwenye twitter?Kwa nini kila kukicha yanatoka matamko ya kuibeza Chadema kwa hatua waliyochukua na kujifanya leo hii ndio wanatambua mateso makubwa ambayo waliyopata hawa wanawake kwa ajili ya chama chao. Nia ni kuwafanya Chadema wawafukuze kwa hasira ili wabaki Bungeni kwa fadhila yao. Wakifika hapo watawatumia wanavyotaka. Chadema ikiwasamehe na kuwaambia wajiuzuru ubunge ili taratibu za uteuzi zianze upya, itakuwa imekula kwa CCM.

Amandla...
 
Chadema walifanya makosa makubwa Sana kuwafukuza wabunge wao bila ya kubaini ukweli wa Jambo lenyewe
Hivi kuitwa kwenye kamati na kugoma kwenda, bado unataka chama kiendelee kuwavumilia. Wabaki na hao waliojitangaza kuwalinda. Hakuna anayezungumzia huo ubunge wao, waendelee nao wakiwa chini ya ulinzi wa Ndugai.
 
Ni vyema Chadema mkae mezani na hawa mwanachama 19 ni muhimu mno. Mkiwapoteza itakula kwenu. Hawa wanawindwa kuliko wale waliounga juhudi. Mbunge mmoja kati yao ni sawa na wabunge 200 nWahakikishia muhimu mkutane mjue ukweli then baadaye watajiondoa bungeni kwa kuwa waliteuliwa kibatili na mteuzi asiyejulikana.
Imeisha hiyo Mkuu. Hawawezi kuwa maarufu kuliko Chama kilichowajenga kisiasa. Walisahau kuwa kilichowavutia Wanachama na Wafuasi wengi wa Chadema kuchanga fedha na kuwanusuru na kifungo siyo kwa sababu ya umaarufu/umuhimu wao bali ni Chadema.

Hivyo hakuna atajaekuwa na umaarufu kuliko Chama. Kwa muda huu mfupi tu hata wiki moja bado umaarufu wao umeanza kupukutika.
 
Mimi kama Mimi nadhani hawa majembe 19 wapewe nafasi, si vizuri kuwapoteza.
Ni hayo tu kwa sasa

Ngongo safarini Zanzibar Mfereji maringo.
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom