Yaliyoko nyuma ya pazia kuhusu clip ya Haji Manara inayotembea mitandaoni.
Nimepata bahati ya kuyapata yaliyoko nyuma ya pazia kuhusu clip ya Haji. Habari iko hivi:-
Kwa mwaka mzima sasa, viongozi wa Simba wamekuwa na wasiwasi kuhusu ukaribu wa Haji na GSM ambao ni wadhamini wa wapinzani wetu. Hata hivyo, wamekuwa wanamvumilia kwasababu haikatazwi kuwa na marafiki wa upande wa pili. Hata hivyo, katika miezi miwili iliyopita kumekuwa na taarifa za kuvuja kwa taarifa za Simba kwa wapinzani wetu. CEO na viongozi wa Simba wakapanga mikakati ya kudhibiti hujuma dhidi ya Simba. Hivyo, siku ya tarehe 20/07/2021, CEO alimpigia Haji kumsihi kwamba, licha ya urafiki alionao na GSM, na licha ya kwamba ndio wadhamini ya YouTube TV yake, lakini katika kipindi ambacho tunaelekea kwenye mchezo muhimu na wapinzani wetu, ajitahidi kukaa mbali na wadhamini wao kwani inaweza kuleta tafsiri mbaya. Haji aliupokea ushauri huo na kuahidi kuuzingatia.
Hata hivyo, mnamo majira ya tano usiku ilitolewa taarifa kwamba Haji ameonekana maeneo ya Kigamboni, ambapo ndipo ilipo kambi ya Yanga lakini pia ndipo yalipo makazi ya mdhamini wa GSM. Baada ya taarifa hiyo, uongozi wa Simba haukutaka kukurupuka bali ulitafuta ushahidi ili kuthibitisha hilo. Kisha, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba Mo Dewji alimuita Haji na kumuuliza kuhusu suala hilo. Haji alikataa kwamba hakwenda Kigamboni. Alipoonyeshwa ushahidi wa dhahiri wa yeye kuwepo Kigamboni akalipuka na kutoa povu kali na kumtukana na kumdhalilisha Dewji, ingawa Dewji ndiye siku zote amekuwa anamtetea hata pale Bodi ilipotaka kumfukuza kazi miaka miwili iliyopita.
Ili kuwawahi viongozi wa Simba na kujisafisha, ndipo akatoa ile clip kuonyesha anaonewa. Haji ametoa mchango kwenye hamasa kwa Simba na amepata umaarufu mkubwa kupitia Klabu ya Simba. Sisi washabiki wa Simba tunajua kwamba Haji kanufaika sana kwa mgongo wa Simba. Sasa hivi anaamini ni mkubwa kuliko Simba na ana uwezo wa kuwatukana na kuwatisha viongozi wake.
Uamuzi wake wa kusambaza clip yake ili kujenga taswira ya mgogoro katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye mechi kubwa ni hujuma kwa Simba.