Haji Manara amtuhumu Barbara kuwa na chuki dhidi yake. Amuahidi ataondoka Simba kwani amemkuta

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
11,366
2,000
Manara uswahili unamdanganya, Manara hana uwezo wa kumtoa simba Babra wala Mo.. ila Babra na Mo wana uwezo wa kumtoa Simba Manara..

Mwenye pesa sio mwenzako.. hao kina chama na konde boy unawaona sababu ya kina babra na Mo hapo.. hizo robo fainali za klabu bingwa unaziona sababu ya kina Barbara na Mo.

Je Manara ana uwezo wa kulipa mshahara hata wa Zimbwe tu?
Yeye mwenyewe analipwa jiwe saba bila mkataba ndio ataweza kumlipa mtu kweli?
 

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,882
2,000
6324C7F7-BD11-418E-BFD1-8E5618686176.jpeg

Oscar Oscar kama angekuwa ni Simba. Angekuwa anasubiri simu sasa hivi?
 

Franklin1902

JF-Expert Member
Aug 1, 2018
297
500
Una hoja kubwa sana... timu ambazo zinashindana na simba CAF hazina nafasi wala roles za watu kama manara katika staffs wao... ukitizama documentary ya Enyimba wakati wanabadilika mwaka 2000 walitoa tenda kwa PWC proffessional consultancy firm na hao pwc kuna vyeo vingi sana walivifuta pale enyimba ili timu iwe ya kisasa. Na vikaleta mgogoro kwa wanaotolewa kazini.. ila miaka miwili mbele wakaenda twaa ubingwa wa CAF champions league..

Kuna wakati ili usonge mbele unahitaji ubadili viatu vizito na uvae raba ili utembee haraka
Uko sahihi kbs mkuu..ujanja ujanja na porojo za kahawa hauna nafasi kwenye soka la kisasa.
 

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
654
1,000
Yaliyoko nyuma ya pazia kuhusu clip ya Haji Manara inayotembea mitandaoni.

Nimepata bahati ya kuyapata yaliyoko nyuma ya pazia kuhusu clip ya Haji. Habari iko hivi:-

Kwa mwaka mzima sasa, viongozi wa Simba wamekuwa na wasiwasi kuhusu ukaribu wa Haji na GSM ambao ni wadhamini wa wapinzani wetu. Hata hivyo, wamekuwa wanamvumilia kwasababu haikatazwi kuwa na marafiki wa upande wa pili. Hata hivyo, katika miezi miwili iliyopita kumekuwa na taarifa za kuvuja kwa taarifa za Simba kwa wapinzani wetu. CEO na viongozi wa Simba wakapanga mikakati ya kudhibiti hujuma dhidi ya Simba. Hivyo, siku ya tarehe 20/07/2021, CEO alimpigia Haji kumsihi kwamba, licha ya urafiki alionao na GSM, na licha ya kwamba ndio wadhamini ya YouTube TV yake, lakini katika kipindi ambacho tunaelekea kwenye mchezo muhimu na wapinzani wetu, ajitahidi kukaa mbali na wadhamini wao kwani inaweza kuleta tafsiri mbaya. Haji aliupokea ushauri huo na kuahidi kuuzingatia.

Hata hivyo, mnamo majira ya tano usiku ilitolewa taarifa kwamba Haji ameonekana maeneo ya Kigamboni, ambapo ndipo ilipo kambi ya Yanga lakini pia ndipo yalipo makazi ya mdhamini wa GSM. Baada ya taarifa hiyo, uongozi wa Simba haukutaka kukurupuka bali ulitafuta ushahidi ili kuthibitisha hilo. Kisha, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba Mo Dewji alimuita Haji na kumuuliza kuhusu suala hilo. Haji alikataa kwamba hakwenda Kigamboni. Alipoonyeshwa ushahidi wa dhahiri wa yeye kuwepo Kigamboni akalipuka na kutoa povu kali na kumtukana na kumdhalilisha Dewji, ingawa Dewji ndiye siku zote amekuwa anamtetea hata pale Bodi ilipotaka kumfukuza kazi miaka miwili iliyopita.

Ili kuwawahi viongozi wa Simba na kujisafisha, ndipo akatoa ile clip kuonyesha anaonewa. Haji ametoa mchango kwenye hamasa kwa Simba na amepata umaarufu mkubwa kupitia Klabu ya Simba. Sisi washabiki wa Simba tunajua kwamba Haji kanufaika sana kwa mgongo wa Simba. Sasa hivi anaamini ni mkubwa kuliko Simba na ana uwezo wa kuwatukana na kuwatisha viongozi wake.

Uamuzi wake wa kusambaza clip yake ili kujenga taswira ya mgogoro katika kipindi hiki tunapoelekea kwenye mechi kubwa ni hujuma kwa Simba.
 

Insigne

JF-Expert Member
Jul 3, 2021
564
1,000
ila simba nao wajinga sana, tangu lini afisa habari wa Coca cola akawa ambasador wa Pepsi?

yani haji ni afisa habari wa simba, ambayo ina dhaminiwa na bidhaa za Metl, hapo hapo ni balozi wa bidhaa za Asasi na GSM washindani wa Metl...
Yaah hapo ndo Haji alipokosea, anafanya kazi katika Taasisi ambayo ina udhamini mkubwa halafu anatoka hapo anaenda kuchukua ubalozi wa washindani wa mdhamini kibiashara. Hii haijakaa sawa kabisa.
 

code4494

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
486
1,000
Hizo ni mind games kuelekea Kigoma lake Tanganyika ili kuwatoa kidogo wakina mzee Mpili kwenye reli kamati zimeanza kazi
Mind game inahusiana vp na mchezo wa weekend hii!!? Au hayo mabishano ya Barbara na manara yanawadhoofisha vp wapinzani?au yanawapa nguvu gani wachezaji wa simba?

Au labda utufafanulie "mind game" ipi? Au umetamka tu kufuata mkumbo
Au ndo fashion siku hz kila kitu "mind game"
 

KANYIMBI

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
1,110
2,000
Ila simba nao wajinga sana, tangu lini afisa habari wa Coca cola akawa ambasador wa Pepsi....
Hii inshu ya Asas na GSM ndio chanzo cha tatizo.

Pia Haji kapewa mkataba wa kufanya kazi pale Simba na huo mkataba hauruhusu mtu wa Simba kuwa balozi wa bidhaa nyingine nje ya zile zinazoifadhili timu ya Simba ndio maana anazunguka nao tu hataki kuusaini.

Namshauri Haji aende tu akafanye kazi Azam ndio atajua umaarufu wake umetokana na nini
 

Joo Wane

JF-Expert Member
Mar 14, 2007
727
1,000
Ila simba nao wajinga sana, tangu lini afisa habari wa Coca cola akawa ambasador wa Pepsi???


Yaani Haji ni afisa habari wa Simba, ambayo ina dhaminiwa na bidhaa za Metl, hapo hapo ni balozi wa bidhaa za Asasi na GSM washindani wa Metl.


Haji ameitumia simba kupata umaarufu, kisha akautumia huo umaarufu kutangaza bidhaa za kampuni mshindani wa wadhamini wa simba......
Ni wakati sasa wa Simba kuhakikisha kuwa kuanzia sasa kila mfanyakazi anajaza fomu ya "conflict of interest" kuepuka matatizo ya migongano kama hii .
 

Sambusa kavu

JF-Expert Member
May 4, 2015
711
1,000
Ila simba nao wajinga sana, tangu lini afisa habari wa Coca cola akawa ambasador wa Pepsi???


Yaani Haji ni afisa habari wa Simba, ambayo ina dhaminiwa na bidhaa za Metl, hapo hapo ni balozi wa bidhaa za Asasi na GSM washindani wa Metl.


Haji ameitumia simba kupata umaarufu, kisha akautumia huo umaarufu kutangaza bidhaa za kampuni mshindani wa wadhamini wa simba......

Apo Haji hana makosa, ametumia loop hole ya madhaiu ya Simba ya kutompa mkataba wa kazi

Kama Simba wangempa mkataba wa kazi naamini kabisa kuna baadhi ya vifungu vingemfunga kufanya ubalozi na makampuni pinzani ya Metl
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom