Haji Manara amtuhumu Barbara kuwa na chuki dhidi yake. Amuahidi ataondoka Simba kwani amemkuta

mozilla

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
522
1,000
Nilipenda san hamasa zake. Lakini tatizo la watanzania mafanikio kidogo anajiona ana uwezo sawa au kuliko taasisi. Haji amekuwa kama limbukeni wa umaarufu. Nadhani muda wa kutafuta changamoto sehemu zingine ni sasa...
Na kashaipa sababu bodi kumfukuza kazi, conflicts za ofisini anazipeleka Instagram.

Weledi na uswahili havikai pamoja

Na tuone Haji bila Simba kama hao kina Asas, GSM, Bakhresa kama watamthamini
 

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
2,335
2,000
'
1626928921-picsay.jpg
 

Curtis G

Senior Member
May 4, 2015
144
250
Hili saga linachanganya naona mapema Sana kusema kitu. Nakumbuka Shafii Dauda aliwahi kumwambia Haji kipindi kile wana kaugomvi.
 

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
2,825
2,000
Kuna wakati inabidi tuwe wakweli
Pamoja na mengi mazuri ambayo Manara ameifanyia Simba nafikiri umefika wakati wa kumuacha aende.. Manara ana mapungufu mengi ya kiweledi tena mapungufu ambayo hata mtoto form 1 anaweza kuyazuia.

Manara anapenda kukimbilia mitandaoni ili apate huruma ya mashabiki. Manara anahisi Simba inamuhitaji yeye kuliko yeye anavyoihitaji Simba

Nadhani ni wakati wa kumuacha manara aende iwapo tuna waadhibu kina Mkude pia tusiwaache kina Manara
 

mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,676
2,000
Kati ya Manara na Barbra nani boss? nmesikia Manara anatishia kumfukuza kazi boss wake
Manara chizi kweli. Toka Ile press kabla ya mechi ya tarehe 25 mi nikaona ana connection na upande wa pili na anatumia sana coded language. Ukimsikilizaga kama anaiongelea Simba lakini hua anawapaga ujumbe mahsusi tena kwa msisitizo utopolo, wapo wanaomuelewa na huwa wanafanyia kazi hasa. Kwa Simba ifike sehemu wafanye nae makubaliano ya pande mbili waachane kiustaarabu tu
 

Jjmwaipopo

Senior Member
Jan 11, 2020
169
250
Barbara anaupiga mwingi sana

Manara toka huwezi kushinda vita ya kifamilia kwa akili yako unafikiri Barbara ni rahisi kutoka ukabaki wewe tuliwaambia kwamba hiyo timu ni ya kifamilia zaidi kuliko unavyofikiria kwanza hujiulizi huyo CEO aliingiaje hapo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom