It is sad day for legal society in Tanzania. Nafikiri lengo lilikuwa ni kutenguliwa matokeo na mahakama ya chini ili mahaka ya rufaa ikaya-upheld kwa muda wanaotaka wao whether ni 2014 au 2015. Kwa kuwa Lema kakataa kukata rufaa, maana yake ni kwamba the precedence stands and will be our new case law in the land. Hii inaua demokrasia na uwezo wa watu kujenga hoja na kuchaza politics. Ila kwa kuwa CCM ni mabingwa wa kutukana majukwaani nimependa hukumu hii kwani inarudisha civility majukwaani na watu sasa watajenga hoja kuombea kura badala ya personal issues.
Kwenye hoja nina hakika CCM haiko salama kwani upepo hauvumii kwao ukiangalia na hali ngumu ya watanzania. Ni njia nzuri kwa CCM kujifariji baada ya kupoteza jimbo la Arumeru ila pia ni njia nzuri kwa CCM kujipigilia misumari kwenye chaguzi zijazo. Ila kibaya zaidi ni kuendelea kuondoa imani ya wananchi dhidi ya mahakama zetu.
Ujumbe kwa Mheshimiwa Lema (Mimi bado ninaamini ni mheshimiwa kwa sababu atashinda uchaguzi wa marudio) ni kwamba hii hukumu ni sehemu ya mapambano dhidi ya ukombozi kamili wa watanzania. Usijisikie unyonge sana kwani mamlaka hutoka kwa mungu, Jipange upya fuata mchakato wa chama wa kuomba uteuzi tena nina imani kuwa chama kitakupatia ridhaa kwa mara ya pili, ni haki yako kikatiba kugombea.