Godbless Lema avuliwa ubunge

Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
hayo ni maneno ya losers...
CDM inatia huruma sana, juz tu mmeshangilia kuongeza mbunge, leo tena mnaomboleza kumpoteza mwingine!!!Ama kweli ng'ombe wa maskini hazai!!


Aha aha kumbe uko hai,mara zote uhai wako unategemea habari mbaya za aadui yako,unapigana vita kwa hila na kinyongo,kila saa unajiuliza why not u,kumbuka tunapigania nchi yetu na sio jamii fulan peke yake,change ur attitude,heshimu kitu ambacho wezanko wameshakifanya and join them
 
nchi ipo kwenye transition. pambana.
Kama watu wakiielewa kauli hii wala hakuna shida kabisa kuizika CCM, mimi nawasubili jimbo la Segerea, halafu hivi Majaji kama hawa hawalogeki hata kwa majini?.....nina babu yangu ana majini ya kutosha kabisa!!
 
Wana JF,

Nimesikia sasa hivi kupitia TBC 1 radio kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliyokuwa ikisikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) imeshatoa hukumu asubuhi hii na kwamba Mhe. Gobbless Lema amenyang'anywa Ubunge mezani na Jaji Gabriel Rwakibarila.

Hivyo kuanzia leo Mhe. Godbless Lema si Mbunge tena na Jimbo la Arusha Mjini liko wazi.My take: Hukumu hii itaacha maswali mengi sana ndani ya mioyo na vichwa vya Watanzania. Kwamba hukumu ya Kesi hii ilikuwa imepangwa kimkakati na Chama Cha Magamba kwa kuitumia Mahakama kumnyang'anya Lema na CHADEMA jimbo hili kwa makusudi ili Uchaguzi urudiwe.

Inasikitisha kuwa sababu zilizotolewa na upande wa walalamikaji ambao ni WANACHAMA 3 WA CCM hazikuwa na uzito wa kutengua matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Arusha mjini. Ikumbukwe kuwa mgombea wa Ubunge wa CCM Bi Matilda Buriani aliyebwagwa chini na Godbless Lema hakufungua kesi hiyo wala hakuwahi kutokea kwenye Mahakama hiyo kutoa ushahidi kwamba Lema alitoa kauli za udhalalishaji, matusi na kashfa kwa Bi Buriani. Kwanini mgombea wa CCM asemewe na watu wengine ilhali mwenyewe kakaa kimya??

CCM wamecheza rafu katika hili. Hata hivyo hata kama Uchaguzi utaitishwa leo hii WEMBE NI ULEULE ULIOMNYOA SIOI SUMARI KULE ARUMERU EAST. CCM wasifurahie kuwa wamepata mteremko wa kurudisha jimbo hilo mikononi mwao. Wasahau. Kama wanabisha waitishe Uchaguzi waone kilichomzuia kuku kukojoa. CCM kimedhihilisha kuwa ni Chama Cha Mafisadi na Chama Cha Mahakama-CCM. Hakika Tanzania bado tuna safari ndefu ya kufikia Demokrasia ya kweli!!

Nawasilisha.
 
jimbo la arusha hata kama kikwete akisimama na lema , bado ccm itapigwa chini.
 
Mtajivua mpaka damu nyie magamba.Unadhan maendeleo huja kwa upuuzi huu.
 
Ndio maana alikua anampigia shavu nassari kwasababu alikua najua ashapotea na atavuliwa ubunge hata iweje ,sasa bwana mdogo anaingia mjengoni yeye kapigwa benchi na watu wake aliowaleta arumeru wote kushnehi CCM ndio malegendary na watachukua Arusha mjini na baadae tutarudi arumeru..

Anacho.kojolea mama yako mzazi.
 
Nadhani hakim haijui A
.Town vizur ameleta ulaji pasipo kuombwa. Magamba anzen kutenga hayo Makaisari Yale A.East yameisha!!!!!
 
Watengue na yale ya Segerea ili muvie liwe tamu zaidi! tunataka tuchukue majimbo mawili kwa mpigo bila kupiga kampeni


Hakika nawaambieni tena CDM haina haja ya kupiga kampeni Arusha.. na hapa haijalishi imemsimamisha nani au kitu gani
 
Mhhhhhhh kwa hyo pesa zingine tena zinaenda kuchezewa tena ?? au hakutakuwa na kampeni tena?? Hivi kweli tutafika kwa mtindo huu??

Uko sahii mkuu wangu.Inasikitisha kuwa ni ukweli politician wetu hawajali wala kutoa vipaumbele kwa wananchi wake!Wako tayari kufanya loolote hilimradi kujihakikishia wanakaa madarakani.Inauma sana.Tunaona walimu,afya na kwingineko watz wanavyo taabika,lakini serikali iko tayari yote hayo yaendelee kuliko kuacha kuingia gharama za uchaguzi zisizo na kichwa wala mkia!Mbaya zaidi iko tayari hata kuaribu credibility ya wataaramu wake ilimradi tu,wanaendelea kuwa madarakani.INAUMA SANA!Kuna kamsemo kamoja ka kizungu wanasema blessing in disguise,nafikili nimeeleweka.cdm itumie anguko hili kama njia ya kawaelimisha wananchi kinacho endelea kwenye nchi yao,kwa maneno mengine wamepata plattform nyingine ya kuwafikia wananchi kupitia uovu huu wa wazi kabisa unaoonyesha na jinsi gani hawajari matakwa ya wananchi wao!du!
 
Lema anasema kuwa ameshakuwa anashawishiwa sana agombee kwa tiketi ya ccm, lakini amekuwa anakataa, ndiyo maana hasira za Ikulu zimemshukia kwa nguvu zote!
 
Chadema msijazane ujinga bana ,bwana Lema ameona asikate rufaaa kwasababu anauhakika ashapoteza hivyo na kweli alifanya upuuzi kutoa lugha chafu, ,mbunge gani anafujo namna hiyo na kuutukana mkono uliomlisha toka akiwa mdogo, sasa kakua anajikuta na yeye anamabavu ya kuleta fujo na matusi sasa imemcost...
 
Lazima tuangalie wapi tulifanya makosa tuweze kujikosoa na tuweze kulirudisha jimbo letu la Arusha. Wao wananguvu za kimahakama na dola kiujumla sie hatuna ila for the name of 'PEOPLE'S POWER' pamoja tutashinda.
 
Ni funzo kwa wanasiasa wetu-Nadhani hakuwa ametulia hata baada ya ushindi. Lugha za matusi ilikuwa ada yake. Nadhani sasa katika mchakato wa katiba unaendelea kuwepo kipengele cha kuzua wabunge na viongozi wa kitaifa wastahafu (isipokuwa wenyeviti wa vyama) kushiriki katika kampeni za chaguzi ndogo. hawa waitwe ni viongozi wa kitaifa:

maslahi ya chama yawe kando ili kulinda heshima ya nchi na matumizi sahihi ya utaifa. hata hivyo namtakia LEMA ushindi kama ataruhusiwa tena kugombea au yeyote katika upinzani -not CCM -SIIPENDI KWA DHATI YA MOYO WANGU
 
Jaji Gabriel Rwakibarila siwezi kuamini umeuza utu wako,taalumu yako kisa Pesa!

Kumbuka Haki haidhulumiwi bali inachelewesha, Damu yeyote itakayomwagika Arusha..itakuwa ya mikono yako!

Kumbuka malipo ni hapa hapa duniani...,leo cheka na mafisadi na hao hao ndio watakaokumaliza, GODBLESS LEMA uliyemdhulumu haki yake ndiye atayekutetea samba samba na mwenzako MAGESSA MULONGO
 
Kama watu wakiielewa kauli hii wala hakuna shida kabisa kuizika CCM, mimi nawasubili jimbo la Segerea, halafu hivi Majaji kama hawa hawalogeki hata kwa majini?.....nina babu yangu ana majini ya kutosha kabisa!!

umenichekesha kidogo.!? Babu yako anafuga majini?
Fanya basi wapoteze wale mahakimu.!?
 
Cha haraka ninachojifunza hapa ni muda muafaka kwa Chadema kuangalia aina ya Mawakili wanaowaweka kwenye kesi.Baadhi ya Mawakili siyo bana!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom