Godbless Lema amlilia Freeman Mbowe kwa waraka mzito

Godbless Lema amlilia Freeman Mbowe kwa waraka mzito

Mbowe keshamaliza ngwe yake ya uongozi ndani ya chama, mwacheni apumzike na harakati badala yake kijiti mnacho ninyi endelezeni mapambano. Nampenda sana MZee Mizengo Pinda, yupo kimya kabisa keshamaliza nafasi yake kama kiongozi kawaachia wengine waendeleze pale wao walipoishia
Sasa kama kamaliza ngwe yake kwanini anapambana na mwenzake aliye muachia kijiti?kwanii naye asitulie nankuungana na chama chake? Hii tagsiri yake hakurudhika na bado ana ubinafsi na roho mbaya
 
tunataka mabadiliko bila sisi kuhusika , yani ni chadema, act, bunge la ulaya, tec, mpina, gwaji , na sasahivi tumemuweka mbele slowslow huku tukisubiri miujiza ipige kazi --- hatari sana hii mkuu
Wengi hawatakuelewa

But this is the whole truth
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Yani after all you have done to him pamoja na huyo Lissu mlitaraji ataendelea moja kwa moja na harakat za chama ???
Yan moja kwa moja ?
Mtu mshasema mwizi, kanunuliwa, dhaif , mzembe, dikteta, af Aje aendelee kufanya kaz na nyie ??

MÑAWAZIM.
 
WARAKA WA GODBLESS LEMA KWA MBOWE!Mhe. Godbless Lema amemuandikia waraka Mhe. Freeman Mbowe. Kwa kuwa waraka huo umebeba maudhui yenye maslahi mapana, sisi tunauweka hapa kusudi kupanua wigo wa fikra.Je, nini kimekushangaza?

Je, nini maoni yako?Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula Itunge, Dar es Salaam; 17 Julai 2025; saa 2:50 usiku.Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe!Kwa heshima, huzuni na uzito wa dhamira, nakuandikia barua hii si kwa hasira, bali kwa mwangwi wa historia inayolilia uaminifu.

Sisi tulisimama nyuma yako kwa gharama kubwa kipindi chote ambacho tulikuamini kuwa wewe ni kiongozi wa matumaini ya kizazi kilichojitoa kwa ajili ya Tanzania mpya wakati ulipokuwa Mwenyekiti wetu.Leo hii umetazamwa ukihudhuria mkutano wa Serikali kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa, huku Mwenyekiti wetu,

Tundu Lissu, akiwa gerezani akikabiliwa na mashtaka ya uhaini na chama chetu hakiruhusiwi kufanya siasa na wanachama wetu wanapotea, wanateswa, wengine wameuawa na bado hujatokea hata mara moja mahakamani, wala kutoa neno la kukemea udhalimu huu unaoendelea mbele ya macho ya Watanzania.

Tulikuwa pamoja nawe wakati ulipokamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi na changamoto mbalimbali nyingi katika uongozi wako. Tulilia. Tulipiga kelele. Tulivunjwa. Tukateswa. Lakini tuliendelea kusimama kwa ajili yako kwa sababu tuliamini ulikuwa kiongozi wa haki.

Leo, unajibu kwa ukimya. Ukimya usio na ujasiri. Ukimya unaogharimu damu nyingine isiyo na hatia.“Mungu hadhihakiwi; kwa maana apandacho mtu ndicho atakachovuna.”Wagalatia 6:7Kaka, imekuwa ikisemwa kwamba unayo hasira dhidi ya baadhi ya maneno yaliyotamkwa na wanachama wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama. Lakini je, unaweza kweli kuwa na hasira dhidi ya maneno hayo ya kawaida kuliko kuwa na hasira dhidi ya waliokufunga kwa kukuita gaidi?

Je, unaweza kuwa na uchungu kwa wakosoaji wako wa ndani, lakini ukaishi kwa amani na wale ambao walikutesa na tunao washutumu kwa utekaji, mateso, vifo na dhuluma dhidi ya haki na utu?Ulikuwa Mwenyekiti kwa zaidi ya miaka 20.

Siwezi kuandika hapa majina ya watu waliopoteza maisha kwa sababu waliamini kuwa uongozi wetu ulikuwa na dhamira ya kweli. Tumewazika karibu kila mkoa wa nchi hii, tumewasaidia majeruhi. Tumewaokoa wachache gerezani.

Na wengi wao walipigania jina lako. Waliamini katika mfumo uliouongoza. Leo hii, je tuseme nini kwa familia zao? Wakati wao bado wanalipa gharama ya mapambano . Wakati huo huo, hujawahi hata siku moja kusema au kuandika hadharani kuhusu mateso haya yanayoendelea kwa CHADEMA na viongozi wake haswa kesi mbaya inayo mkabili Mkti wetu Tundu Lissu.“

Kama sauti ya damu ya Abeli ililia kutoka ardhini, ndivyo sauti ya mashujaa wa haki inavyolia kila siku ikitafuta si kisasi, bali uaminifu wa dhamira.” Mwanzo 4:10Kama tuliweza kuamka kwa ajili yako, ulipokuwa kiongozi wa Chama chetu , kwa nini sasa usiweze kusimama kwa ajili ya haki, maana hata kama unapumzika siasa lakini binadamu mwema hawezi kupumzisha dhamira yake juu ya haki na utu.

Unafikiri ni sahihi kukosekana kwa andiko au sauti na uwepo wako mahakamani toka Lissu amekamatwa na kwa ajili ya wengine wengi ambao sasa wako katika hatari kubwa ? Chama ambacho wewe ni Mjumbe wa Kamati Kuu hakiruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara. Vijana wake wanapigwa. Mwenyekiti wake yuko jela na viongozi wake wanateswa.

Na bado, hakuna neno kutoka kwako. Hakuna kilio na bado unaweza kushiriki hafla za Serikali bila aibu. Nini kiko nyuma?“Dhamira safi huwa haipumziki katika meza ya heshima, ikiwa vunjiko la haki linapiga kelele mlangoni.”

- Nelson MandelaKwa heshima na unyenyekevu wa historia, tunakuomba, usijitenganishe na damu ya mashujaa waliokuamini. Usikubali jina lako kuwa ukuta wa kusahau damu ya wale waliochinjwa kwa jina la mabadiliko. Usikubali kusimama upande wa utulivu bandia unaozima sauti ya walalia haki.Huu si mwaliko wa ugomvi.

Hii ni sauti ya dhamira. Kilio cha kizazi kilichoumizwa, lakini bado kinabeba matumaini kwamba kuna waliotumwa kusimama kwenye ufa wa taifa.“Haki haipotei, hata ikizikwa kwenye vumbi la kisiasa huibuka tena kwa sauti ya waliojeruhiwa.”

Na hata kama haukumbuki vilio vya waliopotea, kumbuka hili ,mahali ambapo Tundu Lissu anateseka leo Mahakama Kuu ya Tanzania si mbali sana kama Dodoma ulipokuwa ukishiriki kwenye mkutano wa Serikali. Ni safari ya dhamira tu inayotenganisha hatua zako na hatua ya hakika.Godbless Lema, 17 Julai 2025
Akina Lema wajifunze kujitegemea waache kumlilia Mbowe.
 
kutoka anakoishi Mbowe na kisitu ni nusu saaa tu ameshindwa kwenda hata mara moja. ila Kutoka Anakoishi Mbowe na Dodoma ni masaa 3ila Mbowe ameenda haaaa Akili za kuambiwa changamya na zako
Aende Kisutu Lisu akijikwaa akaanguka mseme ni Mbowe!!Tutumie akili za watu wazima jamani.Lisu alimtuhumu Mbowe kwa mengi bora akae kimya
 
Yaani lisu pamoja na mawakili wake wote wale bado pia ana muhitaji mbowe aliekamuita mla rushwa akasikilize kesi yake? Ili atoe maamuzi au akifika yeye mahakamin lissu ataachiwa?
No TAL hamhitaji FM kwenye kesi. Matarajio ya wengi ilikuwa ni Mjumbevwa kudumu wa kamati kuu ya Chadema kuonekana mahakani only for solidarity sake.
 
Mbowe ndiye aliamua Lissu asipelekwe kutibiwa Muhimbili baada ya kushambuliwa na akina Makonda Sep 7, 2017 pale Dodoma.

Kisha akapelekwa Aga Khan Nairobi kwa ndege iliyokodiwa na Mbunge Murki huku Mbowe akimsindikiza na akiwa ameshika drip la damu/ ringer lactate.

Mtu aliyenusuru maisha yako unamdhalilisha kwa maneno ya uwongo, ili tu upate UWENYEKITI wa CHADEMA, hicho ni kiwango cha juu kabisa cha UHAYAWANI wa Lissu.

Nasimama na FAM
 
Leo ndio anatambua umuhimu wa Mbowe? Mtu ambae alihesabiwa kama sehemu ya jamii yake lakini aliangalia tu wakati Mbowe anatukanwa, anasingiziwa uongo, anafitinishwa na chama chake. Si huyu huyu ndie aliyetoa tamko kuwa Lissu hataki vikao vya gizani mara baada ya Mbowe kumtembelea Lissu gerezani? Leo hii anajifanya kumhitaji Mbowe. Huu ni inafik wa kupitiliza.

Amandla...
Kipindi cha uchaguzi January, Mambo yalikuwa mengi. FAM alitukanwa na TAL pia alitukanwa. Team FAM walipoitwa bagamoyo kwa ajili ya maridiano hawakutokea, obviously ni kwa sababu ya kushindwa.
Sasa maisha yanaendelea.
 
Mbowe ni msaliti na kaonyesha usaliti wake waziwazi. Historia itamhukumu si kwa jinsi alivyoanza bali anavyomaliza!
 
Naamini Mbowe ana nguvu bado na hata akifanya mkutano na waandishi wa habari akakemea hata namna kesi inavyoendeshwa nadhani italeta tofauti kidogo. Ila kibinadamu namna alivyoshughulikiwa na viongozi hao na wafuasi wengine walioamua kusimama na viongozi hawa walio madarakani sidhani kuandika waraka mzrefu kutoka kwake leo ukambadilishe Mbowe msimamo wake. Lugha zilikuwa ngumu sana na wakashawishiwa hadi wafuasi wengine kwenda kinyume nae.Walikosa Imani na utendaji wake Ila walikoseana kambi zote.Kama wangetibu majeraha kwanza au kukemea kejeli na kuwaunganisha wanachama nadhani hata Mwamba angeweza kupata nguvu ya kujitokeza. Pengine hakuwaza kushindwa na ni kama aibu kuja kupangiwa majukumu na vijana aliowapika na wakamkebehi wakati wa uchaguzi
freeman+malasusa vs tundu+kitima
 
Kipindi cha uchaguzi January, Mambo yalikuwa mengi. FAM alitukanwa na TAL pia alitukanwa. Team FAM walipoitwa bagamoyo kwa ajili ya maridiano hawakutokea, obviously ni kwa sababu ya kushindwa.
Sasa maisha yanaendelea.
Mbowe aliwaambia wakina Ntobi waache kumtukana Lissu. Lissu hakufanya hivyo.
Mtu ambae ana nia ya maridhiano asingekata tamaa baada ya kikao kimoja. Pana njia nyingi za kuponya majeraha. Angeweza kuunda kamati ya watu wanaoheshimiwa kuchunguza shutma zote za matusi na kuvunjiana heshima. Kila upande ungepata nafasi ya kuweka wazi machungu yake.

Angeweza kuhakikisha kuwa anawasikiliza upande wa pili hata kama hakubaliani nao.

Angeweza kuwakemea hadharani wale wote wanaoendekeza lugha za matusi dhidi ya wanachama wengine.

Kitu pekee kilichofanywa ni kuwa summon kwenye kikao kimoja tu Bagamoyo.

Na mpaka sasa hivi wakina Lema wanashindwa kuchukua responsibility ya mchango wao katika yote haya. Hawako serious.

Amandla...
 
Back
Top Bottom