Godbless Lema amlilia Freeman Mbowe kwa waraka mzito

Godbless Lema amlilia Freeman Mbowe kwa waraka mzito

Mtasema yote na kutubu Kwa Mwamba.

Yes tunasubiri amnyonge simba, anachelewa nini sasa kuondoa hii kero wakati sisiemu kuna UTULIVU na kapita bila kupingwa??

Wajumbe watakua youtube wanamsikiza soon wametulia ile mbaya
 
Chadema mtajutia kumuacha Mbowe na kumchagua Lissu..!! Mtamlaumu Mbowe sana tu, ila alisema atawaachia Chama yeye anapumzika, afanye biashara zake, sasa kelele za nini?
 
Dah! Watu Bhana! Leo Wanamlilia Mbowe Pamoja Na Yale Yote Waliyoyasema Kipindi Cha Uchaguzi? Yaan Kwa Zile Kashifa Ambazo Hamkuleta Ushahidi Bado Mulitarajia Aendelee Kuwa Na Nyinyi? Kosa Lake Lipi Kuunga Mkono Dira Ya Maendeleo Au Kukaa Kmya?
Umegonga point kubwa, walimtukana,wakamsuta,wakamkebei,wakamwita kila aina ya kitu kibaya.
Leo hii bila haya watu walewale walioshangilia anguko la Mbowe.
Kwa kuwa wamekosa dira,wamekosa kiongozi imara wamebakia na "Wanafunzi wa Mwalimu sio Mwalimu mwenyewe".
Bwana Lema katajwa na Mwenyekiti mstaafu kuwa Lema hakuwai kufanya mikutano ya uongozi kanda ya kaskazini.
Mwenyekiti aliongeza pia kuwa hakufuata program za chama,alikigeuza kama mali yake binafsi.
Au kubali kula matapishi yenu,kamlambe miguu,vunja uongozi,mrudishe Mbowe kama Mwenyekiti hata kwa kipindi hiki kifupi Chadema inaweza kwenda Uchaguzi Mkuu na kupata ushindo wa kishindo. .
 
Umegonga point kubwa, walimtukana,wakamsuta,wakamkebei,wakamwita kila aina ya kitu kibaya.
Leo hii bila haya watu walewale walioshangilia anguko la Mbowe.
Kwa kuwa wamekosa dira,wamekosa kiongozi imara wamebakia na "Wanafunzi wa Mwalimu sio Mwalimu mwenyewe".
Bwana Lema katajwa na Mwenyekiti mstaafu kuwa Lema hakuwai kufanya mikutano ya uongozi kanda ya kaskazini.
Mwenyekiti aliongeza pia kuwa hakufuata program za chama,alikigeuza kama mali yake binafsi.
Au kubali kula matapishi yenu,kamlambe miguu,vunja uongozi,mrudishe Mbowe kama Mwenyekiti hata kwa kipindi hiki kifupi Chadema inaweza kwenda Uchaguzi Mkuu na kupata ushindo wa kishindo. .
Sikuwahi kufikiria kama utakuwa na akili ndogo hivi
 
WARAKA WA GODBLESS LEMA KWA MBOWE!Mhe. Godbless Lema amemuandikia waraka Mhe. Freeman Mbowe. Kwa kuwa waraka huo umebeba maudhui yenye maslahi mapana, sisi tunauweka hapa kusudi kupanua wigo wa fikra.Je, nini kimekushangaza?

Je, nini maoni yako?Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula Itunge, Dar es Salaam; 17 Julai 2025; saa 2:50 usiku.Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe!Kwa heshima, huzuni na uzito wa dhamira, nakuandikia barua hii si kwa hasira, bali kwa mwangwi wa historia inayolilia uaminifu.

Sisi tulisimama nyuma yako kwa gharama kubwa kipindi chote ambacho tulikuamini kuwa wewe ni kiongozi wa matumaini ya kizazi kilichojitoa kwa ajili ya Tanzania mpya wakati ulipokuwa Mwenyekiti wetu.Leo hii umetazamwa ukihudhuria mkutano wa Serikali kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa, huku Mwenyekiti wetu,

Tundu Lissu, akiwa gerezani akikabiliwa na mashtaka ya uhaini na chama chetu hakiruhusiwi kufanya siasa na wanachama wetu wanapotea, wanateswa, wengine wameuawa na bado hujatokea hata mara moja mahakamani, wala kutoa neno la kukemea udhalimu huu unaoendelea mbele ya macho ya Watanzania.

Tulikuwa pamoja nawe wakati ulipokamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi na changamoto mbalimbali nyingi katika uongozi wako. Tulilia. Tulipiga kelele. Tulivunjwa. Tukateswa. Lakini tuliendelea kusimama kwa ajili yako kwa sababu tuliamini ulikuwa kiongozi wa haki.

Leo, unajibu kwa ukimya. Ukimya usio na ujasiri. Ukimya unaogharimu damu nyingine isiyo na hatia.“Mungu hadhihakiwi; kwa maana apandacho mtu ndicho atakachovuna.”Wagalatia 6:7Kaka, imekuwa ikisemwa kwamba unayo hasira dhidi ya baadhi ya maneno yaliyotamkwa na wanachama wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama. Lakini je, unaweza kweli kuwa na hasira dhidi ya maneno hayo ya kawaida kuliko kuwa na hasira dhidi ya waliokufunga kwa kukuita gaidi?

Je, unaweza kuwa na uchungu kwa wakosoaji wako wa ndani, lakini ukaishi kwa amani na wale ambao walikutesa na tunao washutumu kwa utekaji, mateso, vifo na dhuluma dhidi ya haki na utu?Ulikuwa Mwenyekiti kwa zaidi ya miaka 20.

Siwezi kuandika hapa majina ya watu waliopoteza maisha kwa sababu waliamini kuwa uongozi wetu ulikuwa na dhamira ya kweli. Tumewazika karibu kila mkoa wa nchi hii, tumewasaidia majeruhi. Tumewaokoa wachache gerezani.

Na wengi wao walipigania jina lako. Waliamini katika mfumo uliouongoza. Leo hii, je tuseme nini kwa familia zao? Wakati wao bado wanalipa gharama ya mapambano . Wakati huo huo, hujawahi hata siku moja kusema au kuandika hadharani kuhusu mateso haya yanayoendelea kwa CHADEMA na viongozi wake haswa kesi mbaya inayo mkabili Mkti wetu Tundu Lissu.“

Kama sauti ya damu ya Abeli ililia kutoka ardhini, ndivyo sauti ya mashujaa wa haki inavyolia kila siku ikitafuta si kisasi, bali uaminifu wa dhamira.” Mwanzo 4:10Kama tuliweza kuamka kwa ajili yako, ulipokuwa kiongozi wa Chama chetu , kwa nini sasa usiweze kusimama kwa ajili ya haki, maana hata kama unapumzika siasa lakini binadamu mwema hawezi kupumzisha dhamira yake juu ya haki na utu.

Unafikiri ni sahihi kukosekana kwa andiko au sauti na uwepo wako mahakamani toka Lissu amekamatwa na kwa ajili ya wengine wengi ambao sasa wako katika hatari kubwa ? Chama ambacho wewe ni Mjumbe wa Kamati Kuu hakiruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara. Vijana wake wanapigwa. Mwenyekiti wake yuko jela na viongozi wake wanateswa.

Na bado, hakuna neno kutoka kwako. Hakuna kilio na bado unaweza kushiriki hafla za Serikali bila aibu. Nini kiko nyuma?“Dhamira safi huwa haipumziki katika meza ya heshima, ikiwa vunjiko la haki linapiga kelele mlangoni.”

- Nelson MandelaKwa heshima na unyenyekevu wa historia, tunakuomba, usijitenganishe na damu ya mashujaa waliokuamini. Usikubali jina lako kuwa ukuta wa kusahau damu ya wale waliochinjwa kwa jina la mabadiliko. Usikubali kusimama upande wa utulivu bandia unaozima sauti ya walalia haki.Huu si mwaliko wa ugomvi.

Hii ni sauti ya dhamira. Kilio cha kizazi kilichoumizwa, lakini bado kinabeba matumaini kwamba kuna waliotumwa kusimama kwenye ufa wa taifa.“Haki haipotei, hata ikizikwa kwenye vumbi la kisiasa huibuka tena kwa sauti ya waliojeruhiwa.”

Na hata kama haukumbuki vilio vya waliopotea, kumbuka hili ,mahali ambapo Tundu Lissu anateseka leo Mahakama Kuu ya Tanzania si mbali sana kama Dodoma ulipokuwa ukishiriki kwenye mkutano wa Serikali. Ni safari ya dhamira tu inayotenganisha hatua zako na hatua ya hakika.Godbless Lema, 17 Julai 2025
Mbowe huwa ana Roho mbaya, alimwekea Sumu zito kabwe akamuua chacha Wangwe kisa hataki wawe wenyeviti chadema, hata Lisu anamchukia sana kisa ni Uenyekiti na yeye ndiyo kala njama na ibirisi wa ccm wamkomoe Lisu , kwa kumbambikia kesi za uongo ili avute pesa ccm na pia fungu la kuidhoofisha chadema kwa kuuza G55 kwa chauma ubwabwa na sasa mbowe ni chawaccm, kawa mtu wa hovyo sana,
 
Mbowe anatamani Lisu afie jela ili arejee chadema kwa njia haramu za kishetani kama Lipumba alivyofanya
 
Mbowe anatamani Lisu afie jela ili arejee chadema kwa njia haramu za kishetani kama Lipumba alivyofanya
Mkuu Kama amefanya yote Kama hayo tuache Karma IPO na itafanya Kazi yake Don't Complain about that .

Kwakuwa the more mnamuongelea Mbowe ndo mnampa Umaarufu na Kama alikuwa anatumiwa na Ccm ataendelea kutumia zaidi.

So we have to ignore him completely kwakuwa we have so many things to do iweje MTU mmoja awe anaongelewa everyday
 
Mbowe ni mwizi ana Roho mbaya na sasa ni Dalali wa siasa kuchukua watu chadema kuwauza chauma ubwabwa, Mbowe ni mtu wa hovvo sana
 
Si akamuombe kwanza msamaha? Mbowe Mzee wa watu aliambiwa akapunzike . Mhe Maria Sarungi mwenye anasemaje?
 
Dah! Watu Bhana! Leo Wanamlilia Mbowe Pamoja Na Yale Yote Waliyoyasema Kipindi Cha Uchaguzi? Yaan Kwa Zile Kashifa Ambazo Hamkuleta Ushahidi Bado Mulitarajia Aendelee Kuwa Na Nyinyi? Kosa Lake Lipi Kuunga Mkono Dira Ya Maendeleo Au Kukaa Kmya?
Chama walicho ng'ang'ani kimewafia.
 
Chadema Bila MBOWE inawezekana (ilisikika sauti toka kwa wageni)
 
Back
Top Bottom