Godbless Lema amlilia Freeman Mbowe kwa waraka mzito

Ukitulia jaribu kupitia kile ulichokiandika
Nakielewa kuliko ulivyoelewa wewe..

Ni bahati mbaya tu kuwa, hujataka kusema kuwa hujaelewa ili usaidiwe kuelewa badala yake unaniita mimi "mpumbavu".

Nami nikakuambia wewe huyo ndiye hasa "upumbavu" wenyewe na sio mimi...

Kwa heri šŸƒšŸƒ, usiku mwema
 
Mbowe wakati huo na sasa
20240419_121012.jpg
 
Nyie jamaa muna vituko sana, mumesahau matusi muliomrushia?
Kwani yeye na genge lake kasahau matusi aliowarushia wenzie, au siyo...?

Au umesahau kuwa alimwita mshindani wake Tundu Lissu masikini, asiye na fedha, asiye na shukrani (sijui zipi) wakati mwenzake alipigwa risasi 16 kwa ajili ya chama, akampigania akiwa gerezani mpaka akatoka na siku hiyo hiyo ya kutoka akawasaliti na kuwauza wenzake wote kwa kuibukia Ikulu ya Jezebel huku wenzake wakiwa wanamsubiri mahakamani...?

Hii ndiyo siku aliyobadilika na kudhihirika Mbowe ni alikuwa nani hasa..!!

Ngoja inyeshe tuone panapovuja. Ngoja dhuluma + unafiki upambane na HAKI tuone kipi kitashinda..

Kama Mungu tumwaminie sisi si Mungu wa HAKI, basi dhuluma na ishinde tu tujue kuwa ndiyo Iko hivyo...
 
Too late

Nilipoona Mzee Ruksa kamtembelea Tundu Lisu Nairobi hospital na kisha kuonana na Rais Kenyata nikajua kapeleka angalizo šŸ˜šŸ™šŸ‡¹šŸ‡æ
Unaijua maana ya "too late", au uo kwenye njozi!

"... angalizo"? Kama kuna angalizo litawamaliza wenyewe; haa sasa hakuna lelemama tena. Ulaghai kikomo chake kimewadia, na wewe anza kunyooka, achana na hizi konakona nyingi unazoyumba nazo kama mlevi.
 
Ndiyo siasa ilivyo.
Inatajiwa ujue when , where, whom.,What and how to play?
 
Kwani yeye na genge lake kasahau matusi aliowarushia wenzie, au siyo...?

Au umesahau kuwa alimwita mshindani wake Tundu Lissu masikini, asiye na fedha, asiye na shukrani (sijui zipi) wakati mwenzake alipigwa risasi 16 kwa ajili ya chama, akampigania akiwa gerezani mpaka akatoka na siku hiyo hiyo ya kutoka akawasaliti na kuwauza wenzake wote kwa akaibukia Ikulu ya Jezebel huku wenzake wakiwa wanamsubiri mahakamani...!

Ngoja inyeshe tuone panapovuja. Ngoja dhuluma + unafiki upambane na HAKI tuone kipi kitashinda..
Ukweli ni vizuri, hawa maadui wa nchi hii wakijiweka wazi namna hii ili kila mtu mwenye akili timamu ajue maadui wa nchi hii ni akina nani hasa.

Kinacho nishangaza mimi, ni huu ujuha (nilitaka kuuita ujasiri) anautoa wapi Mbowe bila ya aibu namna hii, tena wakati huu?
Ujuha wa kujitokeza mbele, kuungana waziwazi na watu waovu, wasiolitakia mema taifa hili.
Amejitokeza haa kumfurahisha nani, hawa wanaolihujumu taifa letu?
 
WARAKA WA GODBLESS LEMA KWA MBOWE!Mhe. Godbless Lema amemuandikia waraka Mhe. Freeman Mbowe. Kwa kuwa waraka huo umebeba maudhui yenye maslahi mapana, sisi tunauweka hapa kusudi kupanua wigo wa fikra.Je, nini kimekushangaza?

Je, nini maoni yako?Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula Itunge, Dar es Salaam; 17 Julai 2025; saa 2:50 usiku.Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe!Kwa heshima, huzuni na uzito wa dhamira, nakuandikia barua hii si kwa hasira, bali kwa mwangwi wa historia inayolilia uaminifu.

Sisi tulisimama nyuma yako kwa gharama kubwa kipindi chote ambacho tulikuamini kuwa wewe ni kiongozi wa matumaini ya kizazi kilichojitoa kwa ajili ya Tanzania mpya wakati ulipokuwa Mwenyekiti wetu.Leo hii umetazamwa ukihudhuria mkutano wa Serikali kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa, huku Mwenyekiti wetu,

Tundu Lissu, akiwa gerezani akikabiliwa na mashtaka ya uhaini na chama chetu hakiruhusiwi kufanya siasa na wanachama wetu wanapotea, wanateswa, wengine wameuawa na bado hujatokea hata mara moja mahakamani, wala kutoa neno la kukemea udhalimu huu unaoendelea mbele ya macho ya Watanzania.

Tulikuwa pamoja nawe wakati ulipokamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi na changamoto mbalimbali nyingi katika uongozi wako. Tulilia. Tulipiga kelele. Tulivunjwa. Tukateswa. Lakini tuliendelea kusimama kwa ajili yako kwa sababu tuliamini ulikuwa kiongozi wa haki.

Leo, unajibu kwa ukimya. Ukimya usio na ujasiri. Ukimya unaogharimu damu nyingine isiyo na hatia.ā€œMungu hadhihakiwi; kwa maana apandacho mtu ndicho atakachovuna.ā€Wagalatia 6:7Kaka, imekuwa ikisemwa kwamba unayo hasira dhidi ya baadhi ya maneno yaliyotamkwa na wanachama wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama. Lakini je, unaweza kweli kuwa na hasira dhidi ya maneno hayo ya kawaida kuliko kuwa na hasira dhidi ya waliokufunga kwa kukuita gaidi?

Je, unaweza kuwa na uchungu kwa wakosoaji wako wa ndani, lakini ukaishi kwa amani na wale ambao walikutesa na tunao washutumu kwa utekaji, mateso, vifo na dhuluma dhidi ya haki na utu?Ulikuwa Mwenyekiti kwa zaidi ya miaka 20.

Siwezi kuandika hapa majina ya watu waliopoteza maisha kwa sababu waliamini kuwa uongozi wetu ulikuwa na dhamira ya kweli. Tumewazika karibu kila mkoa wa nchi hii, tumewasaidia majeruhi. Tumewaokoa wachache gerezani.

Na wengi wao walipigania jina lako. Waliamini katika mfumo uliouongoza. Leo hii, je tuseme nini kwa familia zao? Wakati wao bado wanalipa gharama ya mapambano . Wakati huo huo, hujawahi hata siku moja kusema au kuandika hadharani kuhusu mateso haya yanayoendelea kwa CHADEMA na viongozi wake haswa kesi mbaya inayo mkabili Mkti wetu Tundu Lissu.ā€œ

Kama sauti ya damu ya Abeli ililia kutoka ardhini, ndivyo sauti ya mashujaa wa haki inavyolia kila siku ikitafuta si kisasi, bali uaminifu wa dhamira.ā€ Mwanzo 4:10Kama tuliweza kuamka kwa ajili yako, ulipokuwa kiongozi wa Chama chetu , kwa nini sasa usiweze kusimama kwa ajili ya haki, maana hata kama unapumzika siasa lakini binadamu mwema hawezi kupumzisha dhamira yake juu ya haki na utu.

Unafikiri ni sahihi kukosekana kwa andiko au sauti na uwepo wako mahakamani toka Lissu amekamatwa na kwa ajili ya wengine wengi ambao sasa wako katika hatari kubwa ? Chama ambacho wewe ni Mjumbe wa Kamati Kuu hakiruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara. Vijana wake wanapigwa. Mwenyekiti wake yuko jela na viongozi wake wanateswa.

Na bado, hakuna neno kutoka kwako. Hakuna kilio na bado unaweza kushiriki hafla za Serikali bila aibu. Nini kiko nyuma?ā€œDhamira safi huwa haipumziki katika meza ya heshima, ikiwa vunjiko la haki linapiga kelele mlangoni.ā€

- Nelson MandelaKwa heshima na unyenyekevu wa historia, tunakuomba, usijitenganishe na damu ya mashujaa waliokuamini. Usikubali jina lako kuwa ukuta wa kusahau damu ya wale waliochinjwa kwa jina la mabadiliko. Usikubali kusimama upande wa utulivu bandia unaozima sauti ya walalia haki.Huu si mwaliko wa ugomvi.

Hii ni sauti ya dhamira. Kilio cha kizazi kilichoumizwa, lakini bado kinabeba matumaini kwamba kuna waliotumwa kusimama kwenye ufa wa taifa.ā€œHaki haipotei, hata ikizikwa kwenye vumbi la kisiasa huibuka tena kwa sauti ya waliojeruhiwa.ā€

Na hata kama haukumbuki vilio vya waliopotea, kumbuka hili ,mahali ambapo Tundu Lissu anateseka leo Mahakama Kuu ya Tanzania si mbali sana kama Dodoma ulipokuwa ukishiriki kwenye mkutano wa Serikali. Ni safari ya dhamira tu inayotenganisha hatua zako na hatua ya hakika.Godbless Lema, 17 Julai 2025
Nilishasema huku kuwa Mbowe hana mali alizoanzisha yeye. Zote ni mali za baba yake kuanzia Aishi mpaka Bilicanas. Kuna kiwanja mzee Aikaeli alipewa na Nyerere moshi mjini mpaka leo hajakiendeleza. Mnasema huyu mtu hana njaa ? Kashanunuliwa huyo. Shule ni muhimu sana huko serikalini kumejaa wajinga sana. Lissu kupambana ni kwa sababu yeye ndiyo kiongozi mwenye shule Chadema nzima. Hata ukitaka tuendelee Mbunge awe na sifa ya kuandika master thesis kushirikiana na top international UNIVERSITIES. Kama hana hizo sifa hakuna kugombea. Tutafika mbali sana hauwezi amini.
 
Kuna mambo yanachagiza sana watu kutokuona umuhimu wa kwenda kupiga kura.
Mkuu, 'r2ga', hili siyo swala la watu kutojitokeza tu kuiga kura; kwa watu kama hawa tunaohangaishwa nao halitoshi.
WaTanzania sasa ni lazima wajizatiti kabisa kutafuta njia zote za kuzuia uchaguzi. Bila ya kufanya hivyo, watajitangazia ushindihata ikiwa ni kura za watu milioni moja tu.
 
Dah! Watu Bhana! Leo Wanamlilia Mbowe Pamoja Na Yale Yote Waliyoyasema Kipindi Cha Uchaguzi? Yaan Kwa Zile Kashifa Ambazo Hamkuleta Ushahidi Bado Mulitarajia Aendelee Kuwa Na Nyinyi? Kosa Lake Lipi Kuunga Mkono Dira Ya Maendeleo Au Kukaa Kmya?

Akili za mtanganyika ni shida sana kuzielewa.

Yaani Mbowe juzi na jana hafai Mwamba kakaa kimya bado hamtaki kumwacha salama.
 
Kama hadi huyu kakubali basi no hatari sana huyu FAMView attachment 3409205

NB: Mabadiliko ya kweli yatatoka kwa watanzania wenyewe kwa wingi wetu.

So far kwa sasa bado bado.
Aisee Mama aendelee apige hela mpaka machawa waanze kutekwa na kupotea. Aongeze shida mpaka watu wawe tayari kuandamana na kuua polisi. Kutegemea mabadiliko kwa njia amani ni kujidanganya. Watanzania tunapenda kuvumilia shida kwa kigezo cha uzalendo.Mama usiweke Reforms maana atakayekuja atafanya kama wewe. Shida ziongezeke zaidi tuwe kama Kongo Au Burundi. Mama mitano tena.
 
WARAKA WA GODBLESS LEMA KWA MBOWE!Mhe. Godbless Lema amemuandikia waraka Mhe. Freeman Mbowe. Kwa kuwa waraka huo umebeba maudhui yenye maslahi mapana, sisi tunauweka hapa kusudi kupanua wigo wa fikra.Je, nini kimekushangaza?

Je, nini maoni yako?Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula Itunge, Dar es Salaam; 17 Julai 2025; saa 2:50 usiku.Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe!Kwa heshima, huzuni na uzito wa dhamira, nakuandikia barua hii si kwa hasira, bali kwa mwangwi wa historia inayolilia uaminifu.

Sisi tulisimama nyuma yako kwa gharama kubwa kipindi chote ambacho tulikuamini kuwa wewe ni kiongozi wa matumaini ya kizazi kilichojitoa kwa ajili ya Tanzania mpya wakati ulipokuwa Mwenyekiti wetu.Leo hii umetazamwa ukihudhuria mkutano wa Serikali kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa, huku Mwenyekiti wetu,

Tundu Lissu, akiwa gerezani akikabiliwa na mashtaka ya uhaini na chama chetu hakiruhusiwi kufanya siasa na wanachama wetu wanapotea, wanateswa, wengine wameuawa na bado hujatokea hata mara moja mahakamani, wala kutoa neno la kukemea udhalimu huu unaoendelea mbele ya macho ya Watanzania.

Tulikuwa pamoja nawe wakati ulipokamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi na changamoto mbalimbali nyingi katika uongozi wako. Tulilia. Tulipiga kelele. Tulivunjwa. Tukateswa. Lakini tuliendelea kusimama kwa ajili yako kwa sababu tuliamini ulikuwa kiongozi wa haki.

Leo, unajibu kwa ukimya. Ukimya usio na ujasiri. Ukimya unaogharimu damu nyingine isiyo na hatia.ā€œMungu hadhihakiwi; kwa maana apandacho mtu ndicho atakachovuna.ā€Wagalatia 6:7Kaka, imekuwa ikisemwa kwamba unayo hasira dhidi ya baadhi ya maneno yaliyotamkwa na wanachama wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama. Lakini je, unaweza kweli kuwa na hasira dhidi ya maneno hayo ya kawaida kuliko kuwa na hasira dhidi ya waliokufunga kwa kukuita gaidi?

Je, unaweza kuwa na uchungu kwa wakosoaji wako wa ndani, lakini ukaishi kwa amani na wale ambao walikutesa na tunao washutumu kwa utekaji, mateso, vifo na dhuluma dhidi ya haki na utu?Ulikuwa Mwenyekiti kwa zaidi ya miaka 20.

Siwezi kuandika hapa majina ya watu waliopoteza maisha kwa sababu waliamini kuwa uongozi wetu ulikuwa na dhamira ya kweli. Tumewazika karibu kila mkoa wa nchi hii, tumewasaidia majeruhi. Tumewaokoa wachache gerezani.

Na wengi wao walipigania jina lako. Waliamini katika mfumo uliouongoza. Leo hii, je tuseme nini kwa familia zao? Wakati wao bado wanalipa gharama ya mapambano . Wakati huo huo, hujawahi hata siku moja kusema au kuandika hadharani kuhusu mateso haya yanayoendelea kwa CHADEMA na viongozi wake haswa kesi mbaya inayo mkabili Mkti wetu Tundu Lissu.ā€œ

Kama sauti ya damu ya Abeli ililia kutoka ardhini, ndivyo sauti ya mashujaa wa haki inavyolia kila siku ikitafuta si kisasi, bali uaminifu wa dhamira.ā€ Mwanzo 4:10Kama tuliweza kuamka kwa ajili yako, ulipokuwa kiongozi wa Chama chetu , kwa nini sasa usiweze kusimama kwa ajili ya haki, maana hata kama unapumzika siasa lakini binadamu mwema hawezi kupumzisha dhamira yake juu ya haki na utu.

Unafikiri ni sahihi kukosekana kwa andiko au sauti na uwepo wako mahakamani toka Lissu amekamatwa na kwa ajili ya wengine wengi ambao sasa wako katika hatari kubwa ? Chama ambacho wewe ni Mjumbe wa Kamati Kuu hakiruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara. Vijana wake wanapigwa. Mwenyekiti wake yuko jela na viongozi wake wanateswa.

Na bado, hakuna neno kutoka kwako. Hakuna kilio na bado unaweza kushiriki hafla za Serikali bila aibu. Nini kiko nyuma?ā€œDhamira safi huwa haipumziki katika meza ya heshima, ikiwa vunjiko la haki linapiga kelele mlangoni.ā€

- Nelson MandelaKwa heshima na unyenyekevu wa historia, tunakuomba, usijitenganishe na damu ya mashujaa waliokuamini. Usikubali jina lako kuwa ukuta wa kusahau damu ya wale waliochinjwa kwa jina la mabadiliko. Usikubali kusimama upande wa utulivu bandia unaozima sauti ya walalia haki.Huu si mwaliko wa ugomvi.

Hii ni sauti ya dhamira. Kilio cha kizazi kilichoumizwa, lakini bado kinabeba matumaini kwamba kuna waliotumwa kusimama kwenye ufa wa taifa.ā€œHaki haipotei, hata ikizikwa kwenye vumbi la kisiasa huibuka tena kwa sauti ya waliojeruhiwa.ā€

Na hata kama haukumbuki vilio vya waliopotea, kumbuka hili ,mahali ambapo Tundu Lissu anateseka leo Mahakama Kuu ya Tanzania si mbali sana kama Dodoma ulipokuwa ukishiriki kwenye mkutano wa Serikali. Ni safari ya dhamira tu inayotenganisha hatua zako na hatua ya hakika.Godbless Lema, 17 Julai 2025
Au Mbow3 ndiye shahidi wa siri!šŸ¤”
 
Mkuu, 'r2ga', hili siyo swala la watu kutojitokeza tu kuiga kura; kwa watu kama hawa tunaohangaishwa nao halitoshi.
WaTanzania sasa ni lazima wajizatiti kabisa kutafuta njia zote za kuzuia uchaguzi. Bila ya kufanya hivyo, watajitangazia ushindihata ikiwa ni kura za watu milioni moja tu.
watanzania tunapenda miujiza mkuu -- hatutaki kuhusika tunataka watu wachache + miujiza ndo wafanye mabadiliko
 
Aisee Mama aendelee apige hela mpaka machawa waanze kutekwa na kupotea. Aongeze shida mpaka watu wawe tayari kuandamana na kuua polisi. Kutegemea mabadiliko kwa njia amani ni kujidanganya. Watanzania tunapenda kuvumilia shida kwa kigezo cha uzalendo.Mama usiweke Reforms maana atakayekuja atafanya kama wewe. Shida ziongezeke zaidi tuwe kama Kongo Au Burundi.
tunataka mabadiliko bila sisi kuhusika , yani ni chadema, act, bunge la ulaya, tec, mpina, gwaji , na sasahivi tumemuweka mbele slowslow huku tukisubiri miujiza ipige kazi --- hatari sana hii mkuu
 
Back
Top Bottom